Polisi wasimama kijijini kutoa taarifa ya mwanakijiji aliyeshambuliwa na nyuki, wanakijiji wote wakimbia

Polisi wasimama kijijini kutoa taarifa ya mwanakijiji aliyeshambuliwa na nyuki, wanakijiji wote wakimbia

nyuki ni wapumbavu walishawahi kunidhalilisha katikati ya mji
walinishukia toka juu jengo nikakumbuka ile mbinu ya kulala chini ili wapite bhana kumbe walikua siwapitaji niliona swarm of killler bees linanishukia pale mavumbini nilipojilaza nikaona kukimbia napo ni mbinu ya kivita nilitoka nduki nikiwalenga bodaboda waliokua karibu yangu lengo likiwa kuwagawana nyuki ili mbinu ilifanya kaz nilivowapita tu wale bodaboda mimi nikapumua wana wakaanza kupambania uhai wao
Hadi nimecheka,ukawapunguzia bodaboda msala
 
Muziki wa nyuki usikie tu. Kuna mwaka tulienda kuzika pale kino makaburini, ghafla nyuki wakaibuka. Watu wengine wakasema tutulie hawafanyagi kitu, wale nyuki wakatuzunguka kwanza na ni kweli walikuwa hawang'ati ila wanakuzunguka tu.

Ghafla kuna baadhi ya watu wakaanza kung'atwa. Uvumilivu ulitushinda watu tulitoka spidi kali! Watu wakawa wanavuka lami kwa spidi kali bila kuangalia magari ikabidi yenyewe sasa ndio yasimame.
 
Umenikumbusha tulikuwa kwenye harusi moja Malangali shooter wa video akaenda sehemu ili apate picha nzuri za maarusi wakitoka kwenye gari kuingia kanisani, kumbe chini kwenye majani kuna siafu, bila kujua ametoka hapo kaingia kanisani wakaanza kumtafuna ndani kwa ndani akatelekeza camera kwenda kutafuta washroom akakuta kumefungwa, mwisho akakubali liwalo na liwe yaishe
alisaula!? 😁
 
Yaweza kuwa kweli.

Uhusiano wa polisi na binadanu ni kama haupo tu yaani siku hizi
Polisi ni vibaka waliorasimishwa. Naongelea kwa matendo yao kwa ujumla wake. Kuingia mahabusu bure kutoka mpaka hela hata kama huna kosa 🤔
 
Back
Top Bottom