Polisi watakuja na kisingizio gani? Walisema hawawezi kumhoji Lissu kwasababu hayuko nchini

Polisi watakuja na kisingizio gani? Walisema hawawezi kumhoji Lissu kwasababu hayuko nchini

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Polisi walisema hawawezi kuchunguza kwasababu wameshindwa kumhoji Lissu.

Na kisingizio cha kutokumhoji Lissu ni kwasababu alikuwa nje nchi.

Sasa Lissu amerejea Tanzania. Natarajia jeshi litamhoji na kuwakamata mara moja waliohusika.

Au wataleta kisingizio kingine?
 
Je Lisu amefika kuripoti swala lake? Yupo tayari kushirikiana na mamlaka?

Hilo suala liko Polisi tayari, halihitaji kuripotiwa.

Polisi walishafika eneo la tukio. Waziri wa Mambo ya ndani alishalizungumzia Bungeni.

Kwa msingi huo, taarifa za tukio tayari zipo Polisi na ktk wizara ya mambo ya ndani.

Kinachotakiwa kufanyika ni Polisi kumpatia Tundu Lissu WITO wa kwenda kuhojiwa ktk kituo cha Polisi.

Je, jeshi la Polisi litatoa wito huo?
 
Hapa naona tume huru ya uchunguzi ikiundwa ndio inaweza kutuletea majibu ya uhakika, hasa kama haitaingiliwa na wanasiasa.

Lakini kuwaamini polisi, kisa wameanza kuchekeana na wapinzani kwenye picha zinazosambaa mitandaoni naona ni kujidanganya.

Kwasababu lile tukio la kushambuliwa Lissu naamini lilihusisha system nzima, hivyo sio rahisi kuwaamini polisi, au mwingine yeyote aliyekuwa na mahusiano nao wakati ule, kwenye kufanya uchunguzi wa haki kuhusu lile tukio.
 
Hao police hadi leo hawajatoa maelezo ya awali nini kulitokea pale kwenye crime scene, hawana hata clue washambuliaji walikua wangapi?

Silaha zilizotumika,risasi ngapi zilipigwa pale, cctv je ilikamata tukio au hapana, security guards nini maelezo yao etc etc, tuelewe inavyotakiwa hasa kwenye hizi security estate ni LAZIMA full time kuna mtu anaye monitor hizi cctv, sasa why hili halikufanyika ?,maana wale washenzi wangekamatwa in the act kama hizi cctv zingekua monitored
 
Hapa naona tume huru ya uchunguzi ikiundwa ndio inaweza kutuletea majibu ya uhakika, hasa kama haitaingiliwa na wanasiasa..
Mahusiano gani unazungumzia mkuu Serikali ndio hiyohiyo, hebu fafanua hayo mahusiano.
 
Watasema aliyesema hayo hayupo nchini, yupo ubalozini nchini Zimbabwe.
 
Tanzania hakuna idara ya police Bali Kuna kikundi Cha ulinzi Cha CCM chenye uniforms za polisi.
 
Lakini tulivyoshitaki kwa mungu kuwa atuondolee muuwaji na mtekaji kwenye nchi yetu. Mungu alimtoa haraka Sana, mauwaji na utekaji ukakoma.
 
Back
Top Bottom