Polisi watakuja na kisingizio gani? Walisema hawawezi kumhoji Lissu kwasababu hayuko nchini

Polisi watakuja na kisingizio gani? Walisema hawawezi kumhoji Lissu kwasababu hayuko nchini

..Polisi walisema hawawezi kuchunguza kwasababu wameshindwa kumhoji Lissu.

..Na kisingizio cha kutokumhoji Lissu ni kwasababu alikuwa nje nchi.

..Sasa Lissu amerejea Tanzania. Natarajia jeshi litamhoji na kuwakamata mara moja waliohusika.

..Au wataleta kisingizio kingine?

Kwani ni mara ya kwanza Lissu kuja nchini toka lilipotokea tukio lile? Si alikuja na akagombea Urais, mbona mnasahau haraka? Kama hakuhojiwa kipindi kile unadhani kuna sababu gani ya kuhojiwa sasa? Hilo swala ndio imetoka...limezikwa na walioenda zao..
 
Ningekua Lisu ningetangaza msamaha au kukaa kimya kabisa.

Kufukua makaburi ukiwa Nje ya mfumo Wa kidola ni Hatari kubwa sana Kwa Katiba hii iliyoundwa na Wakoloni kusaidia Wakoloni na uhalifu wao.

Tukio lilifanywa na watu waliokula njama ya pamoja. Haiwezekani kuwa ni watu Wa chini au watu Wenye maslahi madogo .
Ni wazi kuwa ni watu wazito waliokuwa wanalinda maslahi Yao makubwa ambao tishio lao ni Tundu Lisu.

Ikumbukwe kuwa kama mfumo ndio uliofanya njama basi hakuna MTU atakamatwa ZAIDI ya kumweka Tundu Lisu kwenye target mbaya ZAIDI .
Serikali ni ya CCM na mfumo Kwa muda mrefu ulikua unafanya KAZI ya kulinda maslahi ya CCM Ili watu wao wabaki madarakani.

Lisu atangaze tu msamaha itamjengea Heshima kubwa sana.
Ni wazi kuwa Lisu ni Rais ajaye Wa Tanzania kama atajikita kwenye matakwa ya KIROHO . Utawala ni Wa Mungu.
Wanachama Wa Chadema waachane na mambo ya kitoto kitoto. CCM imefikia ukomo katika Ulimwengu Wa KIROHO. Upinzani uliopo ni Chadema na CUF.

Tumwache Tundu ajijengee Heshima kubwa ZAIDI Kwa Wananchi.
 
Mahusiano gani unazungumzia mkuu Serikali ndio hiyohiyo, hebu fafanua hayo mahusiano.
Polisi ndio walitakiwa kufanya uchunguzi wa lile tukio, lakini wakawa wanaleta ujanja ujanja tu, hawakuwahi kufanya chochote, naamini walifanya vile kwa kufuata maelekezo ya wanasiasa [serikali] waliohusika kupanga ule mpango.

Hiyo ndio system ninayoizungumzia.
 
Polisi walisema hawawezi kuchunguza kwasababu wameshindwa kumhoji Lissu.

Na kisingizio cha kutokumhoji Lissu ni kwasababu alikuwa nje nchi.

Sasa Lissu amerejea Tanzania. Natarajia jeshi litamhoji na kuwakamata mara moja waliohusika.

Au wataleta kisingizio kingine?
Watamuhoji ila wanaweza wasitoe press release kwamba wamemuhoji. Kumbukq kuwa uongozi wa juu ulishabadilika
 
Back
Top Bottom