Tetesi: Polisi wazingira Keys Hotel Kwenye Mahafali ya CHASO Kilimanjaro

Tetesi: Polisi wazingira Keys Hotel Kwenye Mahafali ya CHASO Kilimanjaro

Siyo kwamba watu hawatakiwi kukutana. Ni wakati wa kupiga marufuku vyama vingine vya siasa tofauti na CCM maana inaelekea CCM inataka ibaki peke yake kwa nguvu ya dola. Maana kama lingekuwa suala la kukutana tu mbona wanaCCM wao wanakutana, na hayo mahafali yamefanyika? Nimesikia jana CCM wametangaza kufanya mkutano mkuu maalum mwezi ujao tarehe 23 wakati tumeambiwa mikutano ya kisiasa imepigwa marufuku. Hapa utasema nchi hii ina uongozi?
Sasa tufanyeje mkuu?
 
Mkuu hata hapa chuoni wamefika, wameingia chuoni Mwenge, wamezunguka ndani tunawaangalia tu maana wanafunzi wengi hawakuwepo, wamekaa kama dakika ishirini hivi wakaenda zao, Yaani nimeshindwa hata kuelewa tunakoelekea siko sasa.
Za mwizi ni arobaini tu
 
Polisi wawili tu wanafunzi wanawakimbia Watanzania nao tumezidi uoga

Uoga wa watanzania unachangiwa na kutokujua haki za mwananchi hususani wakati wa migomo na maandamano dhidi ya askari.

Pili,haki za mwananchi hazilindwi na polisi wala mahakama hapa Tanzania. Bali watawala wanatumia muhimili wa mahakama kwa haja zao binafsi.
 
Lakini wanaofanyiwa hivyo sio mbuzi ni binadamu, hivyo ukifanya hivi yeye atafanya vile, serikali iwe na maamuzi ya busara, mbona ccm sijaiona ikifanyiwa fujo kwenye hayo mahafali, mnasema mikutano ya hadhara mumekataza na ndani napo mumekataza, halafu mnasema mkutano wenu wa tarehe 23 july utakuwa sio wa hadhara, haya fanyeni tu mnachokitafuta mtakipata
 
Kwan wale walioteka kijiji ngara wamepatikana???
Mi labda nachelewa kuelewa kwan graduu ni mkutano wa hadhara??
Wadau nisaidien hapo
N swali tu..
#nchiyamwendokasi hii
 
kiukweli wadau wa elimu wakemee hii tabia iliyozuka katika vyuo vyetu inayoonyesha kushindwa kuelimika kwa wanaopata elimu. hivi msomi unawezaje kuishusha thamani degtee yako na kufanya mahafali ya kukipigia debe chama kana kwamba ulikuwa unasomea falsafa ya chama husika? watanzania ni wamoja hatuna sababu ya kubaguana.
 
Back
Top Bottom