Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 12,835
- 23,584
Nimeshangazwa sana na ongezeko kubwa la maelfu kwa mamia ya wahamiaji haramu kutoka Ethiopia ambao wanakamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama hapa Tanzania.
Sasa nataka tu nijue huko Kenya watu hawa wanapita pita vipi mpaka kuingia Tanzania bila kuonekana? Hapa kuna harufu ya rushwa tena iliyokithiri katika Serikali ya Kenya hasa Idara ya Polisi na Uhamiaji.
Nikuombe Rais Uhuru Kenyatta najua wewe si member hapa lakini kwa yeyote anayehusika na masuala haya naomba amfikishie Ujumbe Mh. Rais Uhuru kwamba Ofisi yake ya Polisi na Uhamiaji imeoza kwa rushwa hasa kwenye kuwapitisha Waethiopia katika njia za panya ili kuwasaidia kuingia South Africa.
Mnaitia aibu nchi yenu haiwezekani Polisi na Uhamiaji ya Tanzania ndio ifanye Jukumu kubwa la kudhibiti wimbi la wahamiaji wa Kiethiopia wanaopita katika mipaka yenu.
Sitaki povu najua Ujumbe umefika.