Polisi ya Kenya na Immigration mmeshindwa kuwadhibiti Waethiopia wanaokimbilia Afrika kusini?

Hivi hao omba omba wetu wanakamtwa kwenye mapori wakiwa njiani?
Hivi kuna nchi haina omb omba wake duniani.
 

Wengi sana hunaswa, lakini pia kuna baadhi ambao huweza kuikwepa mkono wa sheria. Tuseme wakiweza kuingia Kenya kihalali kisha kukaa huku kwa mda flani.

Halafu huku Kenya, wamegundua maarifa ya kutosafiri pamoja, bali kila mmoja wao kusafiri kivyake au katika kundi la watu wachache tu, mwishowe kujumuika baada ya kuvuka mipaka yetu na kuingia nchi nyingine, hasa Tanzania.

Kwa kweli, haitoleta picha nzuri kwa vyombo vyetu vya kiusalama kila mara kuwasimamisha waethiopia na kuchunguza ikiwa wako nchini kihalali. Hiyo sasa itakuwa ni hujuma. Hilo litawezekana tu, ikiwa watapatikana wakisafiri kundi kubwa pamoja.

Tazama mwaka huu pekee walivyonaswa

https://www.google.com/search?q=ill...enya&client=ms-opera-mini-android&channel=new
 
atleast umejaribu kutolea ufafanuzi.
 
polisi Kenya wanatumia busara wanajua fika hawa ni wapita njia wanatafuta maisha Afrika kusini. Sisemi kitu kuhusu polisi wetu vyovyote vile itasemekana uchochezi.
 
Rushwa imetamalaki huko kwa hao manyang'au.
 
Rushwa imetamalaki huko kwa hao manyang'au.
Sijui ni ipi bora, hela ya kung'arisha viatu kwa polisi wa Tz au 'chai' kama wanavoiita wenzao huku Kenya. Jombaa, nimepatana na polisi wa Tz, mara kadhaa, nikiwa kwenye shughuli zangu. Wanapenda mlungula, tena sawa tu na wenzao huku Kenya. Tofauti ni wao wanaitisha kwa ustaarabu, na usipokuwa makini utadhani umewapa kwa hiari yako.
 
Mbona unaanza kuweweseka na maneno mengii yakujitetea?
 
Hili tatizo la uhamiaji ni kubwa sana duniani kote
Watu wanakimbia madhila waliyokutana na matatizo ya vita na kukosa maisha ya kujikimu kwa siku hadi siku.
Hii inasababisha wengi wakimbie nchi
Eretria waliuwawa sana mpakani kwao tena na jeshi la polisi wakiwa wanaikimbia nchi yao.
Tatizo hili nililiona Calais ufaransa wakati wakimbizi wengi walikuwa wanakatisha kuingia Dover na serikali ya Uingereza ikijaribu kuwarudisha France na matokeo yake walibidi wapige kambi Calais na kuishi maisha duni kabisa.
Nafikiri ni kudhibiti borders na kuwe na patrol ili wasiweze kupenya na wakishikwa border warudishwe walikotokea
Ni suala pana sana hili ambalo linaweza kuzuilika kidogo sana
Je umoja wa Africa wanaliongeaje
 
Mbona unaanza kuweweseka na maneno mengii yakujitetea?
Kuweweseka kivipi? Kwasababu ya sentensi yako moja kuhusu wala rushwa? Come down to planet earth. Nani anapenda wala rushwa? Mimi nakupa uhalisia wa mambo. Mwaka wa pili sasa hivi tangu OSBP ifike Namanga, na polisi pale wanakula rushwa, wote watanzania kwa wakenya. Tena kwa ushirikiano wa pamoja, yaani hata huwezi amini. Kilichobaki tu ni wavishwe sare zinazofanana.
 
Sawa.
 
Na Magufuli kuwaruhusu ombaomba wake kuingia Kenya free.
🙁🙁
hizi akili bwana ombaomba atawezaje kuingia Kenya? kwa nauli gani? na je ameshindwa kuomba watu anaofahamu mpaka aje huko kwenu ambapo hata chakula kupatikana shida? Tumia akili kufikiri kama umeshindwa kujibu hoja ya [HASHTAG]#sir[/HASHTAG] John funga domo
 
sio kweli hili Mkuu,kwani Kenya hawana Life Books kwa raia wake ambazo namba zake zimo ndani ya central data sysytems?kuna walesotho wa Lesotho na sotho wa SA mbona wanatambulikana?kuna watswana wa Botswana na SA mbona wanatambulikana?na mifano kibao ipo tatizo nchi yetu ipo kama choo ,raia wake serikali yetu haitutambui,ndio maana ikiipinga kidogo wanakuzushia uraia!!
 

kuna ombaomba wa Tanzania wamekuja Kenya??hivyo polisi wa Kenya ni dhaifu hata ombaomba anafanikiwa kuingia huko nchini mwenu
Kumbe watz wengi hawajui kwamba omba omba kutoka Tz wametapakaa kwenye miji karibia yote ya Kenya? Ndio maana mnamparamia aliyewaletea ujumbe? Juzi juzi tu huku Kenya watanzania wawili wametupwa jela, tena si kwa miaka michache. Baada ya hakimu kule Kuria kuwapata na kosa la ulanguzi wa watoto walemavu kutoka Tz. Walikuwa wanaletwa huku Kenya ili watumike kwenye shughuli zao za kuchapa hela kwa kuomba omba. Mtu akijaribu kunieleza kwamba wanatoroka utajiri kwenye nchi yao, ntamzaba kofi!
 
Omba Omba wa kutoka TZ si kwa hiari yao. Wapo wakikuyu wanabiashara wanawaleta kutoka bongo, waokota pesa onbehalf of shrewed kikuyu brokers who paid their fare from TZ and house them. Kwani unaishi kenya gani hajui hii biashara ya viwete na omba omba nairobi?
 
Mbona kuna wengi wanakamatwa SA baada ya kupitia Kenya na Tanzania kabisa, ina maana na maafisa wenu wamelala hivyo wacha ushabiki.
Hawa hukamatwa wengi Kenya, tatizo ni kwamba kuna wakati inakua ngumu kuwathibiti maana wana asili ya Oromo hauwezi kutofautisha, Nairobi kumejaa Wamaasai wa kutokea Tanzania ambao huvuka mpaka bila stakabadhi, mbona hao super immigration, super cops, super JWTZ hawawakamati Wamaasai kabla hawajaingia Kenya......Tatizo kila nyuzi mnaleta kiushabiki mkijifanya nyie ni malaika lakini tunawafahamu nyie ni wale wale tu hamna jipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…