Polisi yahimiza Wananchi wote kuwa waangalizi wa Watoto

Polisi yahimiza Wananchi wote kuwa waangalizi wa Watoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
photo_2024-07-28_16-20-09.jpg
Mkaguzi kata ya Ngara Mjini Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Olipa Chitongo amewaomba wananchi kutambua kuwa Jukum la ulinzi wa Watoto ni la watu wote huku akiwataka wananchi wa kata hiyo kuwajibika kwa pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi katani hapo katika ulinzi wa watoto.

Mkaguzi huyo amewambia wananchi wa kata yake kuwa anatambua namna wanavyojitahidi kuwalinda watoto huku akiwataka kutambua kuwa yeye kama Mkaguzi wa kata hiyo apendi kusikia mtoto kapotea akisisitiza kila mtu awe mwangalizi wa mtoto ili kusitokee matukio kama hayo.

Aidha amebainisha kuwa kila mtu anapaswa kuwa mlinzi wa watoto ambapo amewataka kutoangalia kuwa uyu ni mtoto wanani na badala yake kuhusika na ulinzi kwa kila mtoto katani hapo.
photo_2024-07-28_16-20-08.jpg
Vilevile amesema kuwa endapo watafanya jitihada hiyoo vitendo vya kupotea kwa watoto vitakwisha katika kata yake huku akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
 
Binafsi ninasifu ubunifu wa kuwa na Askari Polisi kila kata.wanasaidia sana kuliweka Jeshi la Polisi karibu na wananchi.Tatizo ni CCM sasa.wanawayumbisha kiasi cha kuwafanya tuwaone ni wehu na majuha tu kama huyu..Anasisitiza ulinzi wa watoto, tatizo ambalo wakuu wake wa kazi wanasisitiza kabisa halipo,kwamba ni uzushi, drama na taharuki inayozushwa na watu wenye nia ovu na Jeshi hilo.
 
Kama wAziri amesema hakuna utekaji kwa nini watoto walindwe
 
Kwenye payroll je jukumu ni la Nani...........
 
Back
Top Bottom