Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Zikiwa zimepita siku 29 tangu kada wa Chadema, wilayani Handeni mkoani Tanga, Kombo Mbwana (29) adaiwe kupotea, hatimaye leo Julai 14, 2024 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zacharia Bernard amesema wanamshikilia kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Julai 14, 2024 Kaimu kamanda Benard amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa vya kielektroniki pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zisizo na usajili wake katika kutekeleza uhalifu huo kinyume cha sheria za nchi.
Pia soma: Mke wa Kombo alivyosimulia jinsi Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana na juhudi zilizofanyika kumtafuta Julai 2, 2024
Amesema upelelezi wa matukio hayo umefikia hatua nzuri na wakati wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Anadaiwa kutenda makosa hayo kwenye mikoa tofauti na kuongeza Jeshi hilo linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo ni kosa kisheria.
Kombo Mbwana
Hata hivyo, Julai 2, 2024 Mwananchi lilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando kuhusu madai hayo ya kupotea kwa Kombo ambapo alisema tukio hilo lipo kwenye uchunguzi chini ya Jeshi la Polisi na amewaomba wanafamilia na wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikilishughulikia.
“Serikali haijawahi kushindwa jambo, nawaomba tuwe watulivu,” alisema Msando.