Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukiwa na akili timamu na hofu ya Mungu, huwezi kuwa askari polisi.
 
Eti uhalifu. Wao wenyewe ndo wanatuhumiwa kuwafanyia wananchi uhalifu. Wakilindwa na hayo mwagwanda.
 
Mpumbavu mmoja huyu hapa. Uchunguzi gani mnaoufanya wakati mmeshaambiwa hamuwezi kujichunguza kwa sababu ninyi wenyewe ni watuhumiwa na hivyo Waziri Mkuu ndiye ameagizwa kuunda tume ya uchunguzi ni kwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu amekiri ninyi ni watuhumiwa hivyo nanyi ni sehemu ya mnaopaswa kuchunguzwa.
Jinsi tu mlivyolisoma hilo tamko lenu inadhihirisha dhahiri kwamba ninyi ni wahusika wakuu katika haya yanayoendelea.
 
Wametoa sababu zozote za kwanini?!😮‍💨😏😒

Ni kwanini wamepiga Marufuku maandamano yetu?!
Upepelezi gani unaoendelea wakati watuhumiwa wanatajwa waziwazi na hawakamatwi?
Patakuwa hapotoshi
Wanasemaje kuhusu wale waliyopotea

Ova
Hii mijitu mipolisi ya ajabu sana, yang'ang'ania kufanya uchunguzi wakati hata rais amelazimika kuamuru usifanywe na wao kwa kuwa wao pia ni watuhumiwa na rais akalihamishia kwa Waziri Mkuu aliyndie tume.
Jambo la ajabi pamoja na rais kutoa amri hiyo bado jeshi hilo kupitia msemaji wake wanang'ang'ania kuendelea na uchunguzi. Huu ni ukaidi wa dhahiri kwa rais.
IGP, DCI na Msemaji wa Polisi na Kamanda wa Operation na Mafunzo wanapaswa kuondolewa ofisini
 
Wanaongea as if wenyewe ndo wako juu ya rais kimamlaka.
 
Kweli kabisa, Chadema wanachotaka kufanya ni uhaini, naona haya mambo aliyaandaa marehemu wa Tanga, Mwenyezi Mungu akampenda, sasa nadhani aliowapa mafunzo ya kijeshi wanataka kujipima
Fracking idiot
 
Jeshi la polisi nchini limeonya kuwa litachukua hatua dhidi ya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema ) wanaopanga kufanya maandamano kuanzia September 23 mwaka huu.

Ovyo hilo limetolewa mjini moshi Leo na jeshi hilo kupitia kwa msemaji wake Naibu Kamishna wa polisi(DCP),David Misime katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye shule kuu ya polisi,zamani ikiitwa CCP.

Misime amesema septemba 11 kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,walisikika viongozi wa Chadema akiwamo mwenyekiti wao,Freeman Mbowe wakiwahamasisha wananchi wa Jijini Dar es salaam kuingia barabarani kuanzia septemba 23,2024.

Alisema viongozi hao waliendelea kuhamasisha wananchi wa kanda mbalimbali kukutana Dar es salaam Ili kuungana na wakazi wa Jiji hilo kuingia barabarani.

Misime amesema kuwa jeshi la polisi linatoa onyo kwa viongozi wa chama hicho kuacha kuendelea kuhamasisha wananchi kujihusisha katika uharifu huo na yeyote atakayeingia barabarani atakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za nchi na kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku.

"Jeshi la polisi linatoa ovyo kwa viongozi wa chama hicho kuacha kuendelea kuhamasisha wananchi kujihusisha katika uharifu huo na yeyote atakayeingia barabarani atakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za nchi kwa maana hiyo maandamano hayo yamepigwa marufuku".

"Jeshi la polisi linatoa katazo kwa yeyote atakayealikwa/kuelekezwa kufika Dar es salaam kutoka mkoa wowote ule kwa ajili ya maandamano hayo,asithuhutu kufanya hivyo kwani maandamano hayo ni haramu na hayatafanyika,hivyo,asipoteze muda na gharama yake".

"jeshi la polisi linatoa Rai kwa wananchi wapenda amani kutokubali kurubuniwa,kudanganywa au kushawishiwa kwa namna yeyote na badala yake waendelee kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani".

"Hatua hiyo waliyofikia tunajiuliza na tunaendelea kufuatilia na kuchunguza kwa nini wanataka kututoa kwenye reli ya hatua za kiupelepezi zinazoendelea baada ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amir jeshi mkuu,Mhe😀kt.Samia Suluhu Hassan kuelekeza vyombo vya uchunguzi vifanye uchunguzi Kisha kuwasilisha taarifa kwake.

Akahitimisha Afande Misime.

Onyo limetolewa,mwenye macho haambiwi tazama
 
hawa jamaa huwa siwaelewi kabisa mwishoni anamalizia kusema atakeyeingia barabarani atakabiliwa kwa mujibu wa sheria je ni sheria ipi hiyo
 
-
Ule wa Lissu mpaka leo umefikia wapi?
Hawawezi kujichunguza na wanawezeja kumchunguza Mwenyekiti wa ma RCO's nchi nzima?
Akili ya chadema nimekwisha ielewa, wanatumia formulae ya "" SUPU YA MBWA HULIWA YA MOTOMOTO"kwamba suala likingoja SUPU ITAPOA, sisi wahuni wa zamani tunayajua haya yote! Ha ha ha 😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…