Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni kawaida, hakuna mtamzania aliyetegemea kwamba Policcm itaruhusu.

Hata hao CDM kabla ya kutoa tamko walijua fika, yaani CCM irihusu maandamano ya CDM kupinga utekaji.

Kwa hiyo hii si habari.
Ni kweli hii sio habari ni taarifa
hata mimi nilijua polisi hawawezi kuruhusu haya maandamano.
 
Chadema wana haki juu ya kupatikana kwa wanachama wao ila wamekosa busara ya kusubiri majibu ya kiutekelezaji aliyoagiza mh.Rais......

#Nchi Kwanza!
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.

Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.

Soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"
Hizi ndizo episode wanazozitengeneza TanPol kuonekana si jeshi linalosimamia usalama wa raia.

Ni kichefuchefu kikubwa kusikiliza hii kauli. Kwa mantiki hiyo, polisi wamejipanga kuua tena raia wanaolilia haki yao ya kuishi dhidi ya mauaji yanayoratibiwa na TanPol na TISS kwa pamoja?

Mimi nitakuwepo barabarani. Wajaze magazin zao waje kutuua ili wajisifu wamepambana na uhalifu.

Tokea lini jeshi la polisi likajihusisha na siasa wakati Katiba imewakataza?

Watoe ulinzi kwa waandamanaji na siyo kuwaua
 
Najaribu kuwaza kwa sauti SOKA na wenzake muda huu watakua hai au wamekufa?

Najaribu kuwaza Maumivu ya sativa ambayo katusimulia ni ukatili na unyama wa MAFWELE kutajwa na sativa..

Baada ya mateso na Maumivu makuu uhai ukitoka hautosikia Maumivu tenaa..

"THE ONLY THING WE NEED TO FEAR IS JUST A FEAR ITSELF" Quoted from F.D. ROOSEVELT.
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.

Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.

Soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"
Uchunguzi gani wewe mnaofanya? Mkuu anayeongoza genge la uhalifu na utekaji ni MAFWELE ,sativa alipelekwa kituo cha Oysterbay kwa kuteswa ,mbona hamumkamati MAFWELE au yupo juu ya sheria?
 
Watanzania walio wengi wako Bize na Yanga na Simba mtu wa namna hiyo ni kazi sana kumkomboa.

Yale Maandamano ya juzi juzi wengi walikuwa wanashangaa tuu wamekaa kwenye Vijiwe vyao vya Kahawa.
Yale yaliachiwa kwasababu yalihusu maswala ya ndani ya chama hayakuwa na athari....huoni haya yenye athari juu ya serikali wameanza kuyaropokea bila haya
 
Maandamano ni njia mojawapo ya wenye dukuduku juu ya watawala wao au juu ya haki yao collectively kupaza sauti na kuleta attention na usikakaji wa hoja zao kwa wahusika na wale wasiojua chochote kujua..ila njia hii ni ngumu sana kwa nchi zetu na pengine hata duniani kote..police huingilia kati hata kama hakuna taarifa mbaya nyuma ya maandamano..ila watasema kuna taarufa mbaya, wangepaswa kuwepo kwenye maandamano ili kuzuia KENGE wa kwenye msafara..ila wenyewe wanazuia KENGE na mamba pia wenye haki ya kuandamana. Nadhani uwepo wa police kwenye maandamano unakuwa safi na lengo la maandamano linaweza timia..kazi yao kuweka amani ktk msafara husika. Ila kwakuwa ipo hivyo sisi waoga tunaona tusiandamane kwakuwa hata buku lako unaweza liharibu kesho ukaamka na taarifa za kusikitisha jamii yako..inahitaji uthubutu wa kujitoa kweli mana unaweza chezea virungu na mabomu..MUNGU AISAIDIE NCHI YETU..ASHUGHULIKE NA WOTE WANAOTEKA NA KUUA BINADAMU WENZAO KWA KISINGIZIO CHOCHOTE
 
Yale yaliachiwa kwasababu yalihusu maswala ya ndani ya chama hayakuwa na athari....huoni haya yenye athari juu ya serikali wameanza kuyaropokea bila haya
Yale yenyewe hayakupata Watu wengi Watanzania hawako Serious mambo ya kipuuzi puuzi ndio wako mstari wa mbele.
 
Mwaka 2007,Laila Odinga wa Kenya aliulizwa na Mbowe kuwa:Kwa nini Kenya ukikaribia uchaguzi au baada ya uchaguzi kunakua na maandamano na vurugu? Odinga alijibu kuwa:Hapa Tanzania mnaona kuna amani kwa sababu CCM haijaona kama kuna chama cha upinzani ambacho kinaweza kukiondoa madarakani. Akaendelea kusema siku CCM itakapojiridhisha kuwa kuna chama ambacho kinaweza kuwaondoa madarakani basi wanachama wa chama hicho wataanza kutekwa na kuuawa. Pia akasema wapinzani watachoka na wataanza kujibu mapigo na huo utakuwa mwanzo wa maandamano na vurugu Tanzania. Nb:CCM ndiyo wanateka na kuua watu chini ya ulinzi wa mapoliccm
 
Sidhani kama tanzania ndio nchi ya kwanza au ya mwisho ambayo vyombo vya usalama vinaingilia siasa hii imejitokeza mara kwa mara..

Shida hapa ni upinzani wa hii nchi hauna upinzani wenye mvuto na ubunifu kwa wananchi wengi wanaona ni kama hakunaga upinzani.
Vyama vya upinzania hasa chadema fanyeni utafiti wa kina kwenye nchi nyingine duniani vyama vyao vilifanyaje na vilitumia mbinu gani kujikwamua dhidi ya vyombo vya usalama ambavyo vilikuwa vinaingilia siasa..
"We were forced to form a Paramilitary Wing of uMkhonto we Sizwe (MK) within the ANC because the Government of Whites Minority of South Africa was terrorising us ANC by using the State Security Forces."
Oliver Reginald Tambo, a former President of African National Congress (ANC) from 1967 to 1993.
 
Bado imekua kama fumbo kwa wale wasadikio na wale wasio sadiki, ni sababu ipi kwamba inayopelekea swala la utekaji na mauaji kipindi uchaguzi mkuu unapokaribia hapa nchini kwtu, je, ndio imani potofu inayosukuma swala hili, je, ni sehemu za upinzani kupunguza nguvu ya upibzani wakati wa kampeni?, je, niskendo za wahusika baina yao kupambania vyeo na madaraka ndani ya chama husika?

Na ni kwann kila kipindi wapoteao ni kambi ya wapinzani nasio washikio dola?, je ni ipi sababu juu ya haya yote, na je hii ndiyo tanzania tuitakayo hapo baadae, wanafalsafa waandikapo maandiko yao je uwepo wao kuwa huru na salama upo??? Je watawezaje kuifanya kazi yao??

Ni chachu yangu kuona nyanja ya uongozi bora inafanyiwa kazi kwa wakati sahihi ili kuepusha haya yoyte
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.

Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.

Soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"
Kabla ya Samia kusema walikuwa wamejikalia tu....
 
Back
Top Bottom