Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Utekaji na mauaji havikubaliki Hata kidogo. Hata hivyo, tuheshimu Mamlaka, tulizozipa madaraka ya kufanya uchunguzi kwa mujibu wa sheria na taratibu zetu, zifanye kazi yake.

Zaidi, toka kukua kwangu na hasa kwenye ufuatiliaji wa mambo ya msingi kwa Taifa hili sijawahi kusikia Taasisi ya kisiasa iliyo Nje ya mfumo wa utawala wa nchi, ikiitisha maamndano ya kuwaambia serikali ikubali ushauri wa Taasisi hiyo iliyowapelekea kuhusu furusa za kiuchumi, kitenolojia na Hata kidiplomasia ambazo zingeweza kuwa kuwakwamua wananchi kutoka kwenye lindi la umasikini....! Mara nyingi ni maandamano yanayolenga kutengua serikali ili Taasisi hizo ziingie madarakani wakati zinajua hazijaimarika kwa kazi hiyo.

Povu ruksa!
 
Utekaji na mauaji havikubaliki Hata kidogo. Hata hivyo, tuheshimu Mamlaka, tulizozipa madaraka ya kufanya uchunguzi kwa mujibu wa sheria na taratibu zetu, zifanye kazi yake.

Zaidi, toka kukua kwangu na hasa kwenye ufuatiliaji wa mambo ya msingi kwa Taifa hili sijawahi kusikia Taasisi ya kisiasa iliyo Nje ya mfumo wa utawala wa nchi, ikiitisha maamndano ya kuwaambia serikali ikubali ushauri wa Taasisi hiyo iliyowapelekea kuhusu furusa za kiuchumi, kitenolojia na Hata kidiplomasia ambazo zingeweza kuwa kuwakwamua wananchi kutoka kwenye lindi la umasikini....! Mara nyingi ni maandamano yanayolenga kutengua serikali ili Taasisi hizo ziingie madarakani wakati zinajua hazijaimarika kwa kazi hiyo.

Povu ruksa!
Unashaurije katika hili? Inawezekana kisiasa lakini matukio hayo yapo..unashaurije au nini maoni yako kwenye hisia za matukio hayo?
 
....maoni yako kwenye hisia za matukio hayo?
Kama nitakuwa nimeelewa Maswali yako. Majibu yangu ni kuwa, Tutumie hisia za matukio haya vyema ili tuwabaini wahalifu wanaotekeleza unyama huu na kuwaleta kwenye Vyombo vya sheria wahukumiwe na kupewa adhabu wanayostaili.
 
Yaani Polisi hawa ni full kujikanyaga na kuweweseka.....!

By the way, hivi haya matamko yao hawa Polisi kama hili huyatolea chumbani au mbele ya waandishi wa habari...?

Kama huwa ni PC ya kawaida mbele ya waandishi wa habari, inawakuwaje hawa waandishi kina Pascal Mayalla au kina ChoiceVariable au Tlaatlaah au Lucas Mwashambwa au kina Stroke wameshindwa kumuuliza polisi huyu maswali muhimu na magumu Ili ajibu..?

Mfano;

1. Polisi inapigaje marufuku kitu ambacho wala hakipo mezani kwao? Bila shaka huku ni kupanic na kuweweseka kwa hali ya juu...

2. Sheria inasemaje kuhusu haki ya watu kuandamana kudai haki zao mbalimbali...?

3. Polisi ndiyo watuhumiwa, wanaweza vipi kujichunguza hata adai tusubiri uchunguzi wao. Ni uchunguzi upi huo na unafanyikia wapi na kina nani wanahusika? Au ni mwendelezo huuhuu wa kuchunguzia kwenye vyumba vyao vya utesaji, kuwalazimisha watu wakiri makosa kwa kipigo na kisha kuwaua....?

4. Kuna polisi wametajwa kwa majina kuhusika kwao, polisi imechukua hatua gani...?

##ALL IN ALL: SAMIA SULUHU HASSAN MUST GO....!
 
Mzee Mbowe ni genge lake kwisha habari yao ,mlipewa nafasi ya kufanya siasa za kiustaarabu baada ya kuona kuwa yale maandamano uchwara yalishindwa kuleta tija iliyotarajiwa sasa mmenza siasa za kutaka kuonewa huruma .
Kuna siku nawe utapotea, Mungu hamfichi mnafiki
 
{Copy and Pest}

WASIFU WA MKUU WA GENGE LA UHALIFU AMBALO LINATUHUMIWA KUTEKA,KUKAMATA,KUTESA NA KUUA WAKOSOAJI NA WAPINZANI WA SERIKALI YA CHAMA TAWALA CCM

Jina: Faustine Jackson Mafwele
Umri: miaka 47
Kabila : Mkerewe
Dini: Mkristo
Makazi : Mikocheni
Kazi: Afisa mwandamizi wa polisi
Cheo: Kamishina Msaidizi wa Polisi
Madaraka: Zonal Crime Officer
Tuhuma: Kuendesha genge la uhalifu dhidi ya binadamu.
Mawasiliano: +255 755 855 743
+255 787 922 913

1. ACP Faustine Mafwele kwa mara ya kwanza amethibitishwa hadharani na kutambuliwa na Edgar Edson Mwakabela (Sativa) kama afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye alitoa amri ya kubebwa kwake kisha kusafirishwa kwenda Arusha na katavi kupigwa risasi ya kichwa kabla ya kunusurika kuuawa.

2. ACP Faustine Mafwele amewahi kuwa OC-CID mwaka 2011-2015 wa kituo cha Polisi Arusha na baadae akawa RCO wa Mkoa wa Arusha

Wakati wa mauaji ya wanachama wa CHADEMA maandamano ya Arusha ya 04 January 2011 alikuwa OC-CID.

Wakati huo Faustine Mafwele akiwa na cheo cha ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi

Tarehe 05 January 2012 akiwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi Faustine Mafwele alipigwa risasi na Jambazi Jijini Arusha kati ya majibizano ya risasi baina yake na Jeshi la Polisi,hata hivyo askari mmoja wa Jeshi la Polisi aliuawa kwa risasi na Mafwele aliendelea kutibiwa hospitali ya Seriani.

3.Amewahi kuwa Zonal Crime Officer (ZCO) wa Kanda maalum ya MKIRU yani Mkuranga, Kibiti, Rufiji.

4.katika kesi za watu wanaolalamika kwangu ndugu zao kutekwa, kupotea au kukutwa wameuwawa asilimia 90 wanamtuhumu ACP Faustine Mafwele kama mtu ambaye ndiyo mtekelezaji wa shughuli hizi mbaya.

5.ACP Faustine Mafwele amekuwa ni Afisa wa Jeshi la Polisi ambaye hana madaraka makubwa sana ila anaogopwa hadi na viongozi wake wa Jeshi la Polisi kuanzia Kanda Maalum ya Dar es saalam hadi Makao Makuu ya Polisi,Dodoma

6.Kuna hisia ambazo hazijathibitishwa kuwa ni Penetrating Officer (PE) wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye anafanya kazi mbili kwa pamoja kiasi cha Viongozi wa Jeshi la Polisi kumuogopa wakiamini ni Mtu ambaye kazi zake zina baraka ya Idara ya Usalama wa Taifa.

7.Baada ya Kazi Maalum ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti Rufiji) kumalizika akiwa kama Crime zonal Officer (ZCO) alihamishiwa kwenda Kuwa RCO wa Mkoa wa Mwanza

Huko Dunia ilianza kufahamu ukatili wa ACP Faustine Mafwele baada ya 2021 Mzee William Sije kulalamika kuwa RCO Mafwele wa Mkoa wa Mwanza amemuua Mtoto wake James William Sije.

8.IGP Simmon Sirro alimuhamishia Mkoa wa Dar es Salaam kuja kuwa Zonal Crime Officer (ZCO) wa Kanda maalum ya Dar es saalam 06 April 2022 kwa kazi maalum dhidi ya Panya road na ujambazi wa kutumia Silaha.

9.Misheni na siri nyingi anazozijua ndiyo chanzo cha Viongozi wa Serikali ya CCM kumuogopa na kumlinda wakiamini anaweza kwenda kusema mambo mabaya zaidi anayoyajua.

Kupitia hoja hiyo, ACP Faustine Mafwele amelalamikiwa mara nyingi sana lakini Viongozi wizarani na serikalini wanamuogopa sana kuchukua hatua.

10. Mafwele pia anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao
kupotea kwa

1.Mfanyabiashara Musa Mziba
2.Kupotea kwa Deo Mugasa
3.Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi
4.Kupotea kwa Vijana watano wa Aggrey
5.kutekwa na Kupigwa risasi kwa Edger Edson Mwakabela.
6.Faustine Mafwele na genge lake tarehe 22 August 2024 alituhumiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuhusika kwake ktk Kupotea kwa Kina Godwin Mlay,Deusdedith Soka na Frank Mbise

11.Katika kuonyesha jeuri na kuogopewa na wenzake ACP Faustine Mafwele amejipa ukiranja wa kuwa mwenyekiti wa Ma-RCO wa Jeshi la Polisi Tanzania tofauti na utamaduni wa Jeshi la Polisi ulio zoeleka wa Ma-RCO kuwa chini ya usimamizi wa DCI

12.Nimeona niweke kumbukumbu hizi vizuri na wasifu mfupi wa ACP Faustine Mafwele mjue kazi kubwa iliyopo mbele yetu kuhakikisha Faustine Mafwele anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kujibu tuhuma zake

Bila kelele za kutosha hakuna Jambo litakalotokea kwa sababu nilizozitaja hapo juu

Boniface Jacob
Ex-Mayor Kinondoni & Ubungo
0712 239 595
The voice of the silenced Majority /
Ameshiba damu nyingi za wanachadema,ila ajue malipo ni hapa hapa duniani
 
Msemaji wa Polisi DCP David Misime amesema CHADEMA kutangaza maandamano wakati wao wamepewa agizo na Rais la kufanya upelelezi na kumkabidhi ripoti ni kutaka kuwatoa kwenye reli. Ina maana Mtu akilalamika na kutaka kesi ya mauaji ya ndugu yake iharakishwe ni kuwatoa wapelelezi kwenye RELI? Au Polisi wanatumia Narrow Gauge kiasi kwamba masuala mapana yanawashinda?
 

Attachments

  • 20240913_170923.jpg
    20240913_170923.jpg
    132.9 KB · Views: 1
Itakuwa meter-gauge railway kama ya TAZARA
 
Do not befriend a police man. Shirikiana nao pale tu penye ulazima. Lakini ukimweka kwenye inner circle ya marafiki zako, kuna price tabidi ulipe .
 
Jeshi la vilaza.
Wiki ya pili inakatika.hawaelewi wanafanya nini hata aliyewatuma nae hajui kawatuma nini.
 
Tamko la hovyo, warudishe vijana wetu kwanza. Halafu Chadema waje na mkakati mwingine, maandamano hayajawahi kuwa suluhisho kwenye jambo lolote nchi hii,watu wataumia tu na bado mambo yatabaki vile vile.
Nakubaliana na wewe "ni TAMKO LA HOVYO", lakini hapo hapo unawashauri CHADEMA "waje na mkakati mwingine" badala ya maandamano. Lakini huja pendekeza chochote cha mbadala!

Watu kuumia, tayari wanaumia, au hao wanachama wa CHADEMA siyo watu?

Kwa nini usitoe angalau ushauri wako kuuelekeza huko serikalini, maana wao ndio chanzo kikuu cha matatizo haya.

Waambie serikali na CCM waache kuwaumiza waTanzania wenzako, bila kujali wapo CHADEMA au CCM.
 
chama na serikali
Chama $
ugumu uko hapa kwa wapinzani


ova
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.


Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.

Soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"
Naunga mkono hoja,hatutaki vurugu wasije mlaumu kamanda Awadh
 
Tii ziro ni koloni la nani?
Nchi inaongozwa ki katiba au ki hisia za walio madarakani?
Wao wanafaidi mishahara na marupurupu makubwa wengine ni vilio na kuzika nduguzao kwa kutekwa,kuteswa na kuuwawa!!
VERY EASY;
ROMA NA DEWJI WAHOJIWE NA "INTERPOL" NINANI WALIOWATEKA NA KUWATUPA UNUNIO ILI KUPITIA WAO UCHUNGUZI UENDELEE TUJUE ALIOMTEKA MZEE WETU NA KUMUUA
 
Wazee wa maridhiano,Mama karudisha hiki na kile..
 
Daaah. Yani polisi wanafanya upelelezi kimagumashi harafu wanasema mambo ya kunya
 
Kumbe kupata daraja la IV kidato cha nne huwa sio bahati mbaya, na ndio waliojaa humo.

Kusoma kwao na kuchanganua hata mambo madogo ni suala gumu.
IMG-20240913-WA0000.jpg
IMG-20240913-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom