antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Duh,.....maandamano hayo yamepigwa marufuku.
Kwa nini asipige marufuku utekaji na mauaji ya raia wasio na hatia badala ya kuzuia maandamano?!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh,.....maandamano hayo yamepigwa marufuku.
Unashaurije katika hili? Inawezekana kisiasa lakini matukio hayo yapo..unashaurije au nini maoni yako kwenye hisia za matukio hayo?Utekaji na mauaji havikubaliki Hata kidogo. Hata hivyo, tuheshimu Mamlaka, tulizozipa madaraka ya kufanya uchunguzi kwa mujibu wa sheria na taratibu zetu, zifanye kazi yake.
Zaidi, toka kukua kwangu na hasa kwenye ufuatiliaji wa mambo ya msingi kwa Taifa hili sijawahi kusikia Taasisi ya kisiasa iliyo Nje ya mfumo wa utawala wa nchi, ikiitisha maamndano ya kuwaambia serikali ikubali ushauri wa Taasisi hiyo iliyowapelekea kuhusu furusa za kiuchumi, kitenolojia na Hata kidiplomasia ambazo zingeweza kuwa kuwakwamua wananchi kutoka kwenye lindi la umasikini....! Mara nyingi ni maandamano yanayolenga kutengua serikali ili Taasisi hizo ziingie madarakani wakati zinajua hazijaimarika kwa kazi hiyo.
Povu ruksa!
Kama nitakuwa nimeelewa Maswali yako. Majibu yangu ni kuwa, Tutumie hisia za matukio haya vyema ili tuwabaini wahalifu wanaotekeleza unyama huu na kuwaleta kwenye Vyombo vya sheria wahukumiwe na kupewa adhabu wanayostaili.....maoni yako kwenye hisia za matukio hayo?
Kuna siku nawe utapotea, Mungu hamfichi mnafikiMzee Mbowe ni genge lake kwisha habari yao ,mlipewa nafasi ya kufanya siasa za kiustaarabu baada ya kuona kuwa yale maandamano uchwara yalishindwa kuleta tija iliyotarajiwa sasa mmenza siasa za kutaka kuonewa huruma .
Ameshiba damu nyingi za wanachadema,ila ajue malipo ni hapa hapa duniani{Copy and Pest}
WASIFU WA MKUU WA GENGE LA UHALIFU AMBALO LINATUHUMIWA KUTEKA,KUKAMATA,KUTESA NA KUUA WAKOSOAJI NA WAPINZANI WA SERIKALI YA CHAMA TAWALA CCM
Jina: Faustine Jackson Mafwele
Umri: miaka 47
Kabila : Mkerewe
Dini: Mkristo
Makazi : Mikocheni
Kazi: Afisa mwandamizi wa polisi
Cheo: Kamishina Msaidizi wa Polisi
Madaraka: Zonal Crime Officer
Tuhuma: Kuendesha genge la uhalifu dhidi ya binadamu.
Mawasiliano: +255 755 855 743
+255 787 922 913
1. ACP Faustine Mafwele kwa mara ya kwanza amethibitishwa hadharani na kutambuliwa na Edgar Edson Mwakabela (Sativa) kama afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye alitoa amri ya kubebwa kwake kisha kusafirishwa kwenda Arusha na katavi kupigwa risasi ya kichwa kabla ya kunusurika kuuawa.
2. ACP Faustine Mafwele amewahi kuwa OC-CID mwaka 2011-2015 wa kituo cha Polisi Arusha na baadae akawa RCO wa Mkoa wa Arusha
Wakati wa mauaji ya wanachama wa CHADEMA maandamano ya Arusha ya 04 January 2011 alikuwa OC-CID.
Wakati huo Faustine Mafwele akiwa na cheo cha ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi
Tarehe 05 January 2012 akiwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi Faustine Mafwele alipigwa risasi na Jambazi Jijini Arusha kati ya majibizano ya risasi baina yake na Jeshi la Polisi,hata hivyo askari mmoja wa Jeshi la Polisi aliuawa kwa risasi na Mafwele aliendelea kutibiwa hospitali ya Seriani.
3.Amewahi kuwa Zonal Crime Officer (ZCO) wa Kanda maalum ya MKIRU yani Mkuranga, Kibiti, Rufiji.
4.katika kesi za watu wanaolalamika kwangu ndugu zao kutekwa, kupotea au kukutwa wameuwawa asilimia 90 wanamtuhumu ACP Faustine Mafwele kama mtu ambaye ndiyo mtekelezaji wa shughuli hizi mbaya.
5.ACP Faustine Mafwele amekuwa ni Afisa wa Jeshi la Polisi ambaye hana madaraka makubwa sana ila anaogopwa hadi na viongozi wake wa Jeshi la Polisi kuanzia Kanda Maalum ya Dar es saalam hadi Makao Makuu ya Polisi,Dodoma
6.Kuna hisia ambazo hazijathibitishwa kuwa ni Penetrating Officer (PE) wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye anafanya kazi mbili kwa pamoja kiasi cha Viongozi wa Jeshi la Polisi kumuogopa wakiamini ni Mtu ambaye kazi zake zina baraka ya Idara ya Usalama wa Taifa.
7.Baada ya Kazi Maalum ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti Rufiji) kumalizika akiwa kama Crime zonal Officer (ZCO) alihamishiwa kwenda Kuwa RCO wa Mkoa wa Mwanza
Huko Dunia ilianza kufahamu ukatili wa ACP Faustine Mafwele baada ya 2021 Mzee William Sije kulalamika kuwa RCO Mafwele wa Mkoa wa Mwanza amemuua Mtoto wake James William Sije.
8.IGP Simmon Sirro alimuhamishia Mkoa wa Dar es Salaam kuja kuwa Zonal Crime Officer (ZCO) wa Kanda maalum ya Dar es saalam 06 April 2022 kwa kazi maalum dhidi ya Panya road na ujambazi wa kutumia Silaha.
9.Misheni na siri nyingi anazozijua ndiyo chanzo cha Viongozi wa Serikali ya CCM kumuogopa na kumlinda wakiamini anaweza kwenda kusema mambo mabaya zaidi anayoyajua.
Kupitia hoja hiyo, ACP Faustine Mafwele amelalamikiwa mara nyingi sana lakini Viongozi wizarani na serikalini wanamuogopa sana kuchukua hatua.
10. Mafwele pia anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao
kupotea kwa
1.Mfanyabiashara Musa Mziba
2.Kupotea kwa Deo Mugasa
3.Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi
4.Kupotea kwa Vijana watano wa Aggrey
5.kutekwa na Kupigwa risasi kwa Edger Edson Mwakabela.
6.Faustine Mafwele na genge lake tarehe 22 August 2024 alituhumiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuhusika kwake ktk Kupotea kwa Kina Godwin Mlay,Deusdedith Soka na Frank Mbise
11.Katika kuonyesha jeuri na kuogopewa na wenzake ACP Faustine Mafwele amejipa ukiranja wa kuwa mwenyekiti wa Ma-RCO wa Jeshi la Polisi Tanzania tofauti na utamaduni wa Jeshi la Polisi ulio zoeleka wa Ma-RCO kuwa chini ya usimamizi wa DCI
12.Nimeona niweke kumbukumbu hizi vizuri na wasifu mfupi wa ACP Faustine Mafwele mjue kazi kubwa iliyopo mbele yetu kuhakikisha Faustine Mafwele anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kujibu tuhuma zake
Bila kelele za kutosha hakuna Jambo litakalotokea kwa sababu nilizozitaja hapo juu
Boniface Jacob
Ex-Mayor Kinondoni & Ubungo
0712 239 595
The voice of the silenced Majority /
Nakubaliana na wewe "ni TAMKO LA HOVYO", lakini hapo hapo unawashauri CHADEMA "waje na mkakati mwingine" badala ya maandamano. Lakini huja pendekeza chochote cha mbadala!Tamko la hovyo, warudishe vijana wetu kwanza. Halafu Chadema waje na mkakati mwingine, maandamano hayajawahi kuwa suluhisho kwenye jambo lolote nchi hii,watu wataumia tu na bado mambo yatabaki vile vile.
Naunga mkono hoja,hatutaki vurugu wasije mlaumu kamanda AwadhMsemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.
Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.
Soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea
"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"