Serayamajimbo
Senior Member
- Apr 15, 2009
- 191
- 38
Hatimaye baada ya Polisi Mkoa wa Iringa kukataa kuruhusu maandamano ya Dr Slaa toka jana. Muda mfupi uliopita wameruhusu maandamano hayo yafanyike kesho jumamosi Mei 2, 2009 kuanzia saa 3 asubuhi. Maandamano hayo yataanzia uwanja wa Mwembetogwa.
Kwa mujibu wa barua ambayo waombaji wameiwasilisha kwa kamanda wa polisi maandamano hayo yanataka mishahara na maslahi ya viongozi wote wa umma wenye nyadhifa za kisiasa yajulikane kwa wananchi kama alivyosema Dr Slaa. Pia waandamanaji hao wanapinga nyaraka za wizi na ufisadi kuitwa za siri halali za serikali. Pamoja na mambo mengine wanalaani ufisadi na usimamizi mbovu katika mgawanyo wa mbolea ya ruzuku na kupanda kwa gharama ya pembejeo katika taifa hali inayoathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya wakulima. Mkoa wa Iringa ndipo ambapo kulitangazwa azimio la "Siasa ni kilimo" lenye lililolenga kuwakomboa watanzania ambalo watawala wa sasa wamelipuuza.
Katika tangazo lao, viongozi hao wameeleza pia kuwa mwisho wa maandamano hayo watanzania watakaoshiriki watasimama kwa ukimya kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu waliofariki katika milipuko ya mabovu katika mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Manispaa ya Iringa mjini Mchungaji Msigwa ambaue ni mmoja wa wajumbe katika kamati ya wananchi ya maandalizi ya maandamano hayo, ametoa mwito kwa wanachi wa Iringa kuhudhuria kwa wingi na kwa wale wenye kuhitaji maelezo zaidi wawasiliane nae kupitia namba yake ya mkononi 0754360996. Shime mtanzania, huu ni wakati wetu wa kuleta mabadiliko