Polisi yasikitishwa na kifo cha kada wa CHADEMA, Ali Kibao. Latoa wito kwa mwenye taarifa za kweli na uhakika awasilishe kwa mujibu wa taratibu

Kwani nimefanya kosa lipi kuweka taarifa zilizotolewa na jeshi la polisi? Mimi nimewasilisha taarifa kama ilivyo pasipo kuongeza neno lolote lile

Utakuja kututafutia ban, jaribu kuelewa nyakati na majira. Kwanini ume hariri/ edit post Yako ya awali kama haikua na nyongeza ya maneno Yako binafsi?

Hao waliotoa hiyo taarifa nao inamaana hawakupata taarifa kwamba mazingira ya ukamatwaji wa marehem ulihusisha askari wa barabarani?

Naona hii ni ukurupukaji baada ya kusikia kauli ya Mheshimiwa.
 
CCM? Acha ujinga, CCM inahusika vipi, shut up plz, hivi kwanini jambo likitokea tena baya unasema ni CCM? Ujue unakosea sana
Nadhani Kwa kuwa mazuri yote yanayofanywa na serikali huchuliwa kama yamefanywa na serikali na viongozi wa CCM hujinasibu kwa serikali yao kufanya, vivyo hivyo hata kwenye mabaya watu wakirusha makombora kwa CCM usihuzunike maana ndo mwenye serikali. Kikubwa tulaani watekaji
 
Nchi ngumu hii

Uteke wewe utese wewe halafu ujichunguze mwenyewe

Pumzika kwa amani mzee Kibao
 
Sema ndugu zangu CCM mnachofanya sio SAWA kabisa , hii nchi imewashinda?
Hii issue ingetakiwa watu tuandamane kama Kenya mpaka kieleweke
Tumefumbia macho huu upumbavu muda mrefu tangu enzi za jiwe ndiyo muasisi
 
Naunga mkono hoja
 


Hakuna siku CCM inaunga mkono utekaji au unyanyasaji wa mtanzania yeyote yule, sasa kuinyooshea kidole CCM ni kukosea sana, na CCM inaumizwa na mwananchi yeyote yule kuumizwa au kukosa uhuru wake kama Katiba ya nchi inavyosema..!!
 
Unaona ripoti ya polisi ni kawaida tu, maisha ya kawaida tu, kwa sababu aliyeuwawa ni kiongozi wa CHADEMA.

Majukumu ya polisi yameishia hapo mwenye taarifa ya kweli apeleke, basi. Na kwa ukada wako unaona kawaida kabisa, CCM mmepoteza ubinadamu mmekuwa kama wanyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…