Polisi yazuia maandamano ya ACT Wazalendo

Nawapongeza ACT na Nondo Kwa kudiriki kuandamana ingawa Kuna watu wabupinzani wanaAMINI ni staged.

Ngoja tusubiri maandamano ya chama kikuu Cha upinzani kikiongozwa na Lissu kuwataka walioguswa na Ripoti ya cag wakae pembeni Ili uchunguzi wa kurudisha pesa zetu uendelee.
 
Hilo halibadilishi udikteta WA MAGUFULI. Mbona enzi ya jakaya maandamano mengi tu yalizuiwa. Mkuu MAGUFULI alikuwa DIKTETA Tena hatari kusini mwa jangwa la sahara
Udikteta wa Magufuli ni kuwatumbua vyeti feki, wakwepa kodi, wadhulumaji, mafisadi, wezi, walamba asali, majizi, wauza ngada
 
Safi sana watu wafate utaratibu ndio msingi w sheria.
Wamekosa kazi tutawapatia kazi
 
ACT si mnajionaga ni chama kikuu cha upinzani? Hivi kweli polisi wanakuwa wengi kuliko waandamanaji halafu useme una chama hapo? chadema itakuja mpango mkakati wa nn kifanyike na sio maandamano... Level ya maandamàno walishaivuka

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Lakini kuwawajibisha wezi wa fedha za umma kunakosababisha maisha kuzidi kuwa magumu kwa "wanyonge" sio kipaumbele?
Wao kipaombele chao nikuwawajibisha wezi wakuku ili iwe fundisho kwa wengine. Kwao hawataki iwe fundisho
 
Mkakati huo kabambe una baraka za wananchi?

Au una baraka ya the So called "Maridhiano"?
 
Bravo ACT Wazalendo!!
 
Yaani kabisa, walitegemea wanaandamana mpaka ikulu? Hata adabu hawana....who can allow such nonsense. Kila mtu akiruhusiwa kuandamana kwenda Ikulu heshima ya ikulu itakuwaje. Mambo ya kutazama kwenye movie wanadhani ni uhalisia
Heshima ipo hiyo unayoizungumzia ilhali wakwepa Kodi wakuu na wahuni wanakwenda kula futari huko??

Hapo palikuwa na heshima yake miaka ya 60-84 ila sio Sasa.
 

CAG ni kama wakaguzi wengine.wanapotoa ripoti ya ukaguzi haimanishi kuwa kila kilichoandikwa mule ni ukweli mtupu.zile ni hoja ambazo zinatakiwa kujibiwa .so kusema eti hasara ya wizi ule ni zaidi ya trillion 30 siyo kweli.subirini wahusika wajibu hoja then ndipo tuandamane.sawaaa???/
 
maandamano ya Ngome ya Vijana wa ACT-Walendo yakishindwa kufanyika, Mwenyekiti wa Ngome hiyo Abdul Nondo amesema wanajipanga kufanya maandamano siku nyingine.

Nondo amesema maandamano hayo ya amani yalipangwa kuanzia Manzese hadi Ikulu kuonana na Rais Samia Suluhu Hasaan na kumfikishia ujumbe wa kutokukubaliana na ubadhilifu wa fedha za umma uliofanywa, kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ya kila mwaka.

Aprili 5 Mwaka huu, (CAG), Charles Kichele aliwasilisha ripoti yake mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ikionyesha ubadhilifu wa mali za umma kiasi cha kuwaibua wananchi wanaotaka hatua stahiki zichukuliwe.
 
Huyu zitto kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo si kila siku wewe na majuha wenzio mnasema amelambishwa asali? Leo kawa mwema????
Unafiki jambo baya sana! Yaani kulwa jilala umepandisha uzi bila kumnanga zitto seriously?
 
Huyu zitto kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo si kila siku wewe na majuha wenzio mnasema amelambishwa asali? Leo kawa mwema????
Unafiki jambo baya sana! Yaani kulwa jilala umepandisha uzi bila kumnanga zitto seriously?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…