Polisi yazuia maandamano ya ACT Wazalendo

Polisi yazuia maandamano ya ACT Wazalendo

Maandamano ya kweli hayawezi kuzimwa na polisi ,maandamano ya kweli polisi hawawezi kuwa wengi kuzidi waandamaji,hau walikuwa ni kikundi Cha vijana wahuni wa mitaani wasiyo na kazi.
Tena walitakiwa watandikwe na warudi ndani!
 
Mimi thread zangu ni check an balance kati ya awamu ya sita na ile ya tano,leo ngome ya vijana ya Act wazalendo ilipanga kufanya maandamano hadi ikulu kwa mama yao kipenzi rafiki wa demokrasia, diplomasia na maendeleo aliyekuja kuwapa uhuru walio ukosa kwa miaka sita ya Magufuli.

Wamekutana na na kukabiliana na polisi wakiwa bado eneo la ofisi zao , polisi walijihami kwa siraha , mabomu ,virungu na pingu wakawambia wasithubutu kuvuka eneo lao,yako wapi ya kusema Magufuli alikuwa dikiteta

USSR View attachment 2591863

===
Dar es Salaam, Tanzania - Maandamano ya amani yaliyokuwa yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Ngome ya Vijana, Abdul Nondo, kuelekea Ikulu kwa Rais Samia Suluhu Hassan, yamekabiliwa na zuio la polisi katika ofisi za chama hicho zilizopo Magomeni Jijini Dar es Salaam leo.

Maandamano hayo yaliyoandaliwa na vijana wa ACT yalilenga kuonesha hisia zao dhidi ya wabadhirifu wa fedha za umma waliotajwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Abdul Nondo, aliongoza maandamano hayo akiwa na vijana wengine.

Hii ni mara ya kwanza kwa vijana wa ACT kufanya maandamano ya aina hii, na tukio hili limezua mjadala mkubwa katika jamii kuhusu suala la ufisadi na uwajibikaji wa watumishi wa umma. Rais Samia Suluhu Hassan hajatoa tamko lolote kuhusu maandamano hayo hadi sasa.
Bora ACT wamejaribu

 
Maandamano yameanzia ofisini yakaishia sebuleni. Kiswahili kimekuwa kigumu sana. Kwanini wasiandike polisi yawazuia vijana wa ACT waliokuwa wanajiandaa kuandamana. Sasa hapo wameandamana wapi hawajatoka hata getini.
 
Wamepata milliage ya kisiasa nchini!!

Good move!!

Hadi 2025 wataongeza idadi ya wabunge Bungeni!

Mungu ibariki Tanzania yetu!!
 
IF YOU USE THIS ENERGY FOR YOUR LIFE, THEN YOU WILL NOT BE BEGGING FOR FOOD

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Wasalaam
Kwa Sasa
+267
...And this is my life. I never visited you and your wife to beg for anything

So, stay calm dude!!
 
Back
Top Bottom