Polisi yazuia maandamano ya ACT Wazalendo

Polisi yazuia maandamano ya ACT Wazalendo

Serikali ya CCM inapenda maandamano ya Machawa ya kinafiki yenye kupongeza tu.

Maandamano serious ya kudai HAKI zetu za msingi hayatakiwi. WHY?
 
Heshima ipo hiyo unayoizungumzia ilhali wakwepa Kodi wakuu na wahuni wanakwenda kula futari huko??

Hapo palikuwa na heshima yake miaka ya 60-84 ila sio Sasa.
Kama unadhani ikulu ni kama kwa hawara yako unaweza kwenda kwa style yo yote unayotaka, sawa. Kila la heri. Siku ukivunjwa miguu ndipo utajua viongozi wako ni wapuuzi walikudanganya.
 
Huyu zitto kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo si kila siku wewe na majuha wenzio mnasema amelambishwa asali? Leo kawa mwema????
Unafiki jambo baya sana! Yaani kulwa jilala umepandisha uzi bila kumnanga zitto seriously?
Jikite kwenye hoja
 
maandamano ya Ngome ya Vijana wa ACT-Walendo yakishindwa kufanyika, Mwenyekiti wa Ngome hiyo Abdul Nondo amesema wanajipanga kufanya maandamano siku nyingine.

Nondo amesema maandamano hayo ya amani yalipangwa kuanzia Manzese hadi Ikulu kuonana na Rais Samia Suluhu Hasaan na kumfikishia ujumbe wa kutokukubaliana na ubadhilifu wa fedha za umma uliofanywa, kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ya kila mwaka.

Aprili 5 Mwaka huu, (CAG), Charles Kichele aliwasilisha ripoti yake mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ikionyesha ubadhilifu wa mali za umma kiasi cha kuwaibua wananchi wanaotaka hatua stahiki zichukuliwe.
Nimesikiliza hoja za polisi wakijibizana na Nondo eti wanasema.raisi ameshachukua hatua kwahiyo hakuna haja ya maandamano. Yaani polisi wanaanza kujibia Wanasiasa hoja za msingi kwa ujinga ujinga.
 
Nimesikiliza hoja za polisi wakijibizana na Nondo eti wanasema.raisi ameshachukua hatua kwahiyo hakuna haja ya maandamano. Yaani polisi wanaanza kujibia Wanasiasa hoja za msingi kwa ujinga ujinga.
Inashangaza kwakweli. Hii nji ni siasa tu hadi majeshini
 
Jikite kwenye hoja
Una hoja ipi wewe zaidi ya kutetea wahalifu? Unaukesha kulalamikia ufisadi huku unataka watu waliifanya makosa kama kina sabaya wawe huru kisa walìteuliwa na shetani unayemtumikia ?
Unapiga kelele juu ya ufisadi kisha kiongozi fisadi kama magu akiandikwa ufisadi wake unawatukana waliomuandika?
Sasa nape ndiyo anateua mkurugenzi wa habar ikulu?
 
Shida ACT nao waoga. Wakabaki wamejibanza kwenye geti la ofisi yao. Ni Kama hawakuwa serious na maandamano.
 
Mimi thread zangu ni check an balance kati ya awamu ya sita na ile ya tano,leo ngome ya vijana ya Act wazalendo ilipanga kufanya maandamano hadi ikulu kwa mama yao kipenzi rafiki wa demokrasia, diplomasia na maendeleo aliyekuja kuwapa uhuru walio ukosa kwa miaka sita ya Magufuli.

Wamekutana na na kukabiliana na polisi wakiwa bado eneo la ofisi zao , polisi walijihami kwa siraha , mabomu ,virungu na pingu wakawambia wasithubutu kuvuka eneo lao,yako wapi ya kusema Magufuli alikuwa dikiteta

USSR View attachment 2591863

===
Dar es Salaam, Tanzania - Maandamano ya amani yaliyokuwa yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Ngome ya Vijana, Abdul Nondo, kuelekea Ikulu kwa Rais Samia Suluhu Hassan, yamekabiliwa na zuio la polisi katika ofisi za chama hicho zilizopo Magomeni Jijini Dar es Salaam leo.

Maandamano hayo yaliyoandaliwa na vijana wa ACT yalilenga kuonesha hisia zao dhidi ya wabadhirifu wa fedha za umma waliotajwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Abdul Nondo, aliongoza maandamano hayo akiwa na vijana wengine.

Hii ni mara ya kwanza kwa vijana wa ACT kufanya maandamano ya aina hii, na tukio hili limezua mjadala mkubwa katika jamii kuhusu suala la ufisadi na uwajibikaji wa watumishi wa umma. Rais Samia Suluhu Hassan hajatoa tamko lolote kuhusu maandamano hayo hadi sasa.
Uhuru bandia umeshangiliwa sana
 
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo mh Abdul Nondo amesema katika Barua waliyoandikiwa na polisi wameambiwa wasiandamane kwa sababu wabadhirifu Waliotajwa kwenye ripoti ya CAG Wameshachukuliwa hatua

Source ITV Habari
 
LABDA hawa wa Mfuko wa maafa wa JESHI la POLISI
JamiiForums1239065022.jpg
 
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo mh Abdul Nondo amesema katika Barua waliyoandikiwa na polisi wameambiwa wasiandamane kwa sababu wabadhirifu Waliotajwa kwenye ripoti ya CAG Wameshachukuliwa hatua

Source ITV Habari
Ndio wanasema eti wamewachamba inatosha ,watu wa pwani hovyo sana

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi Cha magu hata hiyo nia tu ya kutaka kuandamana nondo angekuwa hajulikani alipo muda huu.

Huo ndio utofauti Kati ya 5/6
 
Wamuache mama afanye kazi hayo maandamano hayana tija NAMWOMBA ndugu yetu MZALENDO ZZK
Amwache mama afanye Kaz maandamano hayana tija Kwa Sasa......

Nashaur jeshi la police litumie NGUVU zake kuwabzibiti na kuwasweka ndani Ili wamwache Mama Samia afanye kazi bila presha za wanasiasa uchwara.....

Mimi Huwa nafikiria badala vyama vyetu vya siasa viachane na siasa za majitaka na propaganda uchwara Kwa mwamvuli wa democrasia....

Ni muda Sasa CCM na vyama vingine kujitafakari sanaaa ni wakati sasa tupate mwarobaini wa kutibu matatizo yetu ya tangu Uhuru sio Kwa maandamano hayana tija....

Huu utoto ndio unacopy na kupaste kila uzi, acha utoto dogo.
 
Safi sana watu wafate utaratibu ndio msingi w sheria.
Wamekosa kazi tutawapatia kazi
Kuandamana kwa amani ni jambo lililopo kisheria boss. Au maandamano unayoyajua ww ni kwenda kusifia tu?
 
Back
Top Bottom