Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
Mkuu hoja ni kuhusu afrika sio tanzania hivi hta mnayemuita Baba wa taifa Mwl Nyerere mnasahau alituma wanajeshi nigeria waende kusaidia vita vya Biafra ili waigbo wajitenge???? Mistakes happen ila bado Haipotezi ukweli kuwa gadaffi ndio mwamba wa Afrika hasa kupinga ukoloni mamboleo ambao nchi karibu zote za afrika zimeshindwa
 
Gadafi kama alianza michakato ya kupigania Sub-Saharan African countries ni kuanzia miaka ya 90 ,maana gadafi toka mwanzo wazo lake kuu ilikuwa kuunganisha nchi za kiarabu kuwa state moja ( Pan-arab state),kwa hiyo alipigania sana hiyo kitu yake hadi lakini ikashindikana baada ya nchi nyingi za kiarabu za Africa kupenda zaidi muungano wa Afrika ambao ulianzishwa zamani (OAU) kuliko muungano ambao gadafi aliutaka, na baada ya Gadafi kupata misuko suko kibao kutoka UN/USA/UK kumuwekea economic sanctions miaka 92 baada ya ndege ya Scotland kuanguka na kuua abiria wengi na ikajulikana raia wawili wa Libya kuhusika katika tukio hilo la ugaidi , hapo nchi nyingi za Africa walipiinga vikali kuwekewa vikwazo gadafi, na baadae miaka 97 gadafi ndo akabadili gear angani akaachana na issue za kupigania Pan -arab state akaanza uhusiano kamili na PAN-African state na akatemebelea south Africa hapo mandela alishatoka gerezani mida kibao, na watu walishafight sana kupigania uhuru wa kwa nchi za kusini mwa African kina nyerere na Kaunda ,Nigeria etc, baada ya gadafi kuanza miaka hiyo ya 97, basi akaja na wazo la kuunda Union of African sates la kuweka nchi za Africa sasa kuwa kitu kimoja kisiasa na kiulinzi, ambalo wazo hilo lilikuwepo toka Enzi za kina nkwame nkurumah, ingawaje kwa kipindi cha gadafi kuungia lilipata msukumo mkubwa zaidi, na wakafanikisha kuanziasha AU kwa replace OAU, ndo maana ukiangalia waanzilishi wa AU basi gadafi yupo, lakini gadafi kuja kwake ni baada ya mission zake kukwama na amekuja akakuta Sub-Saharan countries zote zimeshajikomboa. Mimi sitaki kusema Gadafi na Mandela nani zaidi, uzaidi huu utakuwa kwa kipindi kipi? kama ni kipindi ya miaka ya 97 -2011 basi gadafi shujaa, lakini kama ni kuanzia 1950----1990 basi kuna wengi mashujaa zaidi ya gadafi hata mandela akiwemo.
Uchambuzi mzuri je mkuu unahisi nani alikuwa na impact zaidi kwenye kipindi chake yaani mandela wa 1950-90 na gaddafi wa 1997-2011...... yaani ukiassue vipindi vyao walipofanya makubwa vingekuwa sambamba nani ungempa credit zaidi
 
Hawa ndugu zangu zangu WA mama mdogo mtu akiwajengea msikiti na kuwapa tende na ubwabwa basi kawamaliza kbsaa. Hawajui kuwa Maisha ya binadamu dini na Maisha ya dunia ni vitu vinavyoenda pmj.
Mkuu udini wa nini tena hoja hapa ni kuwa nani ni pan africanist kuliko mwenzie hayo ya uislam na ukristo yanatoka wapi?? Unasema misikiti unasahau amedonate mpaka chuo hapa Tanzania pia alishatoa misaadana mikopo mingi sana kwa serikali yako ambayo imenufaisha dini zote kivp ssa unaanza kuwananga waislam
 
..waTz hatupaswi kumsifia mtu aliyetoa roho za askari wetu ktk vita vya Uganda.

..Ndiyo maana vijana wa kiTz mnadharaulika kwasababu mnakurupuka kujadili mambo mazito lakini hamsomi.
Kwahyo inatoa the fact kwamba gadaffi sio shuja wa kiafrika aliepinga ukoloni mamboleo???

Mbona serikali yenu imepokea mikopo na misaada yake??? Mbona walidonate chuo mkakubali??? Kma kudharaulika si ingeanza serikali sio wananchi!!!!!

Mtoa mada kauliza Afrika sio Tanzania hivyo mahaba ya uzalendo weka pembeni
 
Atakayekupinga ana MAPEPO makali sana, na ni mtu ambae ni MZITO SANA KICHWANI. Ukitaja Mchango wa Afrika utamtaja Hayat Nyerere, ubaya ni kwamba hakuna kumbukumbu zake muhimu.

Madiba ni nothing kwa Afrika ila kwa wazungu ni shujaa, jamaa aliamua kuikabidhi SA kwa wazungu baada ya kutoka jela.
Mkuu uko sahihi, umaarufu na ushujaa wa madiba upo kihusia zaidi, mapebari walimjaza sifa kibao kwa kuanza na kumpa tuzo ya Nobel! Kiukweli ulikuwa ni mkakati wa kuwanyamazisha mashujaa wa Africa kama nyerere kwa kivuli cha Mandela wasiendelee kuwabugudhi makaburu. Kila nikipitia maandishi ama hotuba za madiba, huwezi kuona falsafa ya upambanaji ndani yake bali ahadi nyingi za kukompromise na wale waliomtesa yeye na waafrika wengine. Majembe ya Africa yako wazi na wazungu wanawajua, historian zao vyombo vya habari huwa havizisemi kwa hofu ya kuamsha hisia na falsafa zao kwa kizazi kipya. Siku zote kwangu madiba si lolote, na kuna wakati nyerere nafikiri kwenye hotuba moja aliwahi kumuambia sema kiujanja ujanja
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
Mkuu , katika kulijadili hili usiengee upande mmoja. Siyo kwa sababu Mandela alikuwa rafiki yetu na Gaddafi alikuwa yupo upande wa Iddi Amin Dada kwenye vita kati ya Tanzania na Uganda basi asiwe na umaarufu.
Kwenye mchango huu iangaliwe.
(1) Ameifanyia nini nchi yake?
(2) Amefanya nini kwa Africa kwa ujumla wake
(3) Nini msimamo wake juu ya Ukoloni mamboleo barani Africa
(4) Alijishughulisha na kuifanya iwe mmoja Kiuchumi na Kisiasa.
Kwa kujaribu tu kutumia hizo hadidu za rejea na nyinginezo kama utakavyona ndipo utoe majumuisho kwamba yupi ni zaidi ya mwenzake. Mandela alitenda makuu lakini Gaddafi nafanya hivyo siyo haki kumfuta kwenye kumbukumbu kiurahisi hivyo.
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
Mkuu , katika kulijadili hili usiengee upande mmoja. Siyo kwa sababu Mandela alikuwa rafiki yetu na Gaddafi alikuwa yupo upande wa Iddi Amin Dada kwenye vita kati ya Tanzania na Uganda basi asiwe na umaarufu.
Kwenye mchango huu iangaliwe.
(1) Ameifanyia nini nchi yake?
(2) Amefanya nini kwa Africa kwa ujumla wake
(3) Nini msimamo wake juu ya Ukoloni mamboleo barani Africa
(4) Alijishughulisha na kuifanya iwe mmoja Kiuchumi na Kisiasa.
Kwa kujaribu tu kutumia hizo hadidu za rejea na nyinginezo kama utakavyona ndipo utoe majumuisho kwamba yupi ni zaidi ya mwenzake. Mandela
 
Wakati Mandela kafungwa jela Gadaffi alikuwa anamwaga hela kwenye chama cha ANC akikisaidia kwenye kampeni dhidi ya apartheid millions of dollars, south Sudan gadaffi ndiye aliyekuwa anawafadhili akina Garang na aliplay part kubwa mpaka inapata Uhuru.. Nimezitolea mfano nchi hizi mbili ila nchi kibao mpaka za south America ,Black movement wa USA nk
Source. Mandela kafungwa kabla Gadafi hajaingia madarakani. Weka source inayoonesha Gadafi katoa msaada kwenye ukombozi
 
Gaddafi sio mwamba wa afrika ungesema mwamba wa uislam na hakua kwa maslahi ya waumini wa imani zingine tofauti na Mandela ambae alikua mtu wa imani zote .... Ukifuatilia harakati za gaddafi nyingi zilikua kusaidia nchi za kiislam
 
Source. Mandela kafungwa kabla Gadafi hajaingia madarakani. Weka source inayoonesha Gadafi katoa msaada kwenye ukombozi
Unachotaka wewe nikuleta ubishi tu sasa tu ,kuna chalii hapo juu kaweka video ya Mandela akimchambua Gaddaffi hiyo inatosha tu ..
 
Gaddafi sio mwamba wa afrika ungesema mwamba wa uislam na hakua kwa maslahi ya waumini wa imani zingine tofauti na Mandela ambae alikua mtu wa imani zote .... Ukifuatilia harakati za gaddafi nyingi zilikua kusaidia nchi za kiislam
Vipi south Sudan

Alikuwa anawafadhili akina garang kwa pesa na silaha kwa miaka na AU alipigania Sudan ivunjwe

Huenda south nao ni waislam

Vipi kuhusu ufadhili wake wa black movement USA, nchi za Latin America kuna kisiwa jna limenitoka

Sent from my IK-644 using JamiiForums mobile app
 
Unachotaka wewe nikuleta ubishi tu sasa tu ,kuna chalii hapo juu kaweka video ya Mandela akimchambua Gaddaffi hiyo inatosha tu ..
Wakati anamchambua alikuwa keshazeeka.
 
history itawahukumu wote,ila huwezi kuwafananisha Madiba na Gaddafi kwangu mimi kuna gap kubwa sana btn them,kwangu Gaddafi alikuwa ni kiongozi kandamizi,aliminya demokrasi ndani ya nchi yake,chaguzi hazikuwemo,alichukua madaraka kwa mapinduzi ya kijeshi sio ballot box(kifaru bila risasi kumbuka),alileta maendeleo makubwa kwa nchi yake ila watu wanahitaji demokrasi zaidi ;Madiba elewa umaarufu wake sio wa kukaa jela tu ,alilinusuru Taifa la SA kuingia kwenye civil war hasa baada ya Chris Hani kuuliwa na wazungu wa mlengo wa kulia,Madiba alikuwa Rais kwa kipindi cha chini ya miaka mitano ambayo ilikuwa migumu mno kwa SA,lakini kwa hekima zake alimudu kuwafanya watu weusi ambao ndio wengi wasiwe na mawazo ya revenge kwa wazungukitu ambacho wengi wetu tusingeweza,angalia siasa zetu zimejaa visasi,Madiba ameacha legacy kubwa SA kama reconcilliations ya raia waliotenganishwa na tofauti kubwa ya kiitikadi.Madiba he is the best president ambaye bara hili limewahi kumtoa;
 
Gaddafi is the hero of age.
Huwezi ukamlinganisha na Mandela aliye-compromise na wazungu koko hadi leo watu weusi wanaishi Kama chokora kule Sauzi na ndiyo inayopelekea hadi xenophobia inajitekeza maana wamechoka.

Ila, tumpime Gaddafi Kwa projects za maendeleo alizokuwa ameweka Kwa ajili ya nchi yake na watu wake.

Mandela issues nyingi zinamilikiwa na wazungu koko.

Kwa hiyo, castes my vote for Gaddafi.

May His Soul Rest in Peace!!.
 
Back
Top Bottom