Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
Ninachojua Mandela kavuma sana kuliko hata wapigania uhuru wenzie, kisa tu ktk kutoka jela yee ndio wa mwisho! Na wapo waliokufa uwanja wa vita pia. Akina Solomon Mahlangu, Walter Sisulu, OR TAMBO et al.
Nadhani kitendo cha kuwatanbua makaburu ndio chanzo cha kuwa maarufu duniani. Nadhani kabla alikua gaidi kwa mujibu wa USA.
West wakiamua kukupandisha au kukushusha ni mara moja tu
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.

hayo yote tunayafahamu Acha kumfananisha Ghadaffi na vitu vya ajabu
 
Mandela ni zaidi.... Gaddafi tofauti kabisa na watu wanavyofahamu alikuwa mkandamizaji mzuri WA Demokrasia nchini Libya.
 
Mandela kafanya nini?upande mmoja wazungu wanaishi kama wako Europe upande mwingine watu wanaishi kwenye slums......
 
Mkuu OAU kwani msumbiji na angola hawakuwepo? Nachojua mimi tz ilipata majeshi kibao hizo nchi.
Sikuzungumzia msaada wa kijeshi. Halikuwa lengo la mwalimu kupigana vita, ndo maana akaomba nchi za OAU zikemee uvamizi wa Idd Amini, hakuna nchi ilikemea. Hiyo ilikuwa kabla Nyerere hajaamua kupeleka nchi vitani.
 
Sikuzungumzia msaada wa kijeshi. Halikuwa lengo la mwalimu kupigana vita, ndo maana akaomba nchi za OAU zikemee uvamizi wa Idd Amini, hakuna nchi ilikemea. Hiyo ilikuwa kabla Nyerere hajaamua kupeleka nchi vitani.
Okay.
 
Mandela ni zaidi.... Gaddafi tofauti kabisa na watu wanavyofahamu alikuwa mkandamizaji mzuri WA Demokrasia nchini Libya.
Mkuu ilikua lazima afanye hivo ili wengi wapate. Unajua western wanatumia njia nying hasa upande za upinzani kuiangusha seikali?
 
Nadhani kitendo cha kuwatanbua makaburu ndio chanzo cha kuwa maarufu duniani. Nadhani kabla alikua gaidi kwa mujibu wa USA.
West wakiamua kukupandisha au kukushusha ni mara moja tu
Wabongo hawajui western ni nan bado
 
Gadafi alitakiwa apambanishwe na kocha wa dunia Nyerere mandela was for his country gadafi and nyerere walikua kwa bara zima kura yangu kwa mwalimu
 
Nyerere pekee ndiye shujaa wa afrika ninayemfahamu.
 
Hao wote baba yao ni Nyerere Najua watu hawajui kuwa Nyerere ndie alietoa mchango mkubwa Sana kwa Mandela na Nchi zote za kusini mwa afrika. Gaddafi ktk sasa za afrika Na Dunia ni mtu mdogo Sana kwanza alikua mbinafsi dikteta muuaji mdini mpenda sifa. Mtu Ambae alikua na tamaa ya uongozi. Pia kwa watanzania Gaddafi alitupiga mwaka 79.tatizo la watanzina hatusomi kujua historia ugonjwa huu upo kwa viongozi wetu na hata waandishi wetu wa habari daima wanaandika habari kwa kufuata upepo tu. Nyerere na Mandela walikua ni viongozi lakn Gaddafi alikua ni mtawala tena mtawala dikteta Ambae hakuwa tayr kuiacha Libya itawaliwe na mtu zaidi ya ukoo wake.
 
ghadaf kafny nn mpk afananishwe na madiba?
Kajenga msikiti Dodoma...karibu Tanzania, nchi yenye wananchi wanaoamini kuwa Gadaffi alikuwa anagawa $50,000 kwa kila mtu aliyekubali kuoa kwa kuwa tu wanawake wa huko wana miiba
 
Mnalinganisha vp watu wawili walioishi maisha tofauti kabisa? Mandela alifungwa jela miaka mingi kwa jitihada za kutaka kujikomboa kwa Makaburu, wakati Gadaff alipindua Libya na maisha yake yote alikuwa anajiimarisha kiuchumi na kujenga misikiti kila alipopeleka misaada, sasa wanasuti vipi hawa wawili?
 
Kujenga msikiti au Kanisa Sio kigezo cha Mtu kufanya maendeleo. Moja ya udini wa Gaddafi ni huo Kujenga msikiti kila Mahali ili kueneza udini wake. Wako watu wamejenga makanisa na misikiti lkn hawakujikweza Kim Gaddafi. Hv mtu akijenga shule hospital na mtu Kujenga msikiti na Kanisa Yupi bora Hapo
 
Gadafi kama alianza michakato ya kupigania Sub-Saharan African countries ni kuanzia miaka ya 90 ,maana gadafi toka mwanzo wazo lake kuu ilikuwa kuunganisha nchi za kiarabu kuwa state moja ( Pan-arab state),kwa hiyo alipigania sana hiyo kitu yake hadi lakini ikashindikana baada ya nchi nyingi za kiarabu za Africa kupenda zaidi muungano wa Afrika ambao ulianzishwa zamani (OAU) kuliko muungano ambao gadafi aliutaka, na baada ya Gadafi kupata misuko suko kibao kutoka UN/USA/UK kumuwekea economic sanctions miaka 92 baada ya ndege ya Scotland kuanguka na kuua abiria wengi na ikajulikana raia wawili wa Libya kuhusika katika tukio hilo la ugaidi , hapo nchi nyingi za Africa walipiinga vikali kuwekewa vikwazo gadafi, na baadae miaka 97 gadafi ndo akabadili gear angani akaachana na issue za kupigania Pan -arab state akaanza uhusiano kamili na PAN-African state na akatemebelea south Africa hapo mandela alishatoka gerezani mida kibao, na watu walishafight sana kupigania uhuru wa kwa nchi za kusini mwa African kina nyerere na Kaunda ,Nigeria etc, baada ya gadafi kuanza miaka hiyo ya 97, basi akaja na wazo la kuunda Union of African sates la kuweka nchi za Africa sasa kuwa kitu kimoja kisiasa na kiulinzi, ambalo wazo hilo lilikuwepo toka Enzi za kina nkwame nkurumah, ingawaje kwa kipindi cha gadafi kuungia lilipata msukumo mkubwa zaidi, na wakafanikisha kuanziasha AU kwa replace OAU, ndo maana ukiangalia waanzilishi wa AU basi gadafi yupo, lakini gadafi kuja kwake ni baada ya mission zake kukwama na amekuja akakuta Sub-Saharan countries zote zimeshajikomboa. Mimi sitaki kusema Gadafi na Mandela nani zaidi, uzaidi huu utakuwa kwa kipindi kipi? kama ni kipindi ya miaka ya 97 -2011 basi gadafi shujaa, lakini kama ni kuanzia 1950----1990 basi kuna wengi mashujaa zaidi ya gadafi hata mandela akiwemo.
 
Hawa ndugu zangu zangu WA mama mdogo mtu akiwajengea msikiti na kuwapa tende na ubwabwa basi kawamaliza kbsaa. Hawajui kuwa Maisha ya binadamu dini na Maisha ya dunia ni vitu vinavyoenda pmj.
 
Back
Top Bottom