Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
1. Nyumba bora kwa kila mwanalibya. SA bado mamilioni ya watu wanaishi kwenye slum.

2. Kusomeshwa bure kwa kila mwanalibya. SA kila kitu ni kulipia.

3. Umeme wa bure kwa kila mwanalibya . SA unalipia kila kitu.

4. Apartments kwa kila graduate na kuozwa mke/Mme na utaanza kulipa rent ukipata ajira. SA hakuna hili.

5. Libya ilikuwa ikifadhili kwa pesa AU. SA haifanyi hivyo.

6. Libya ilikuwa inakopesha nchi za kiafrika bila riba na misaada ya kimaendeleo isiyo mikopo. SA haifanyi hivyo.

7. NK.
Hivyo sio vigezo vyakua kiongozi bora.ata ivyo unaongelea kufanyika kwa hizo huduma wakat enzi za gadafi libya watu walikua hawazid milion 7.acha hisia.
 
Acha kumfananisha tata madiba na vitu vya ajabu

1.Madiba hajawahi kuchukua majeshi kwenda kuvamia ardhi ya nchi nyingine lakini gadafi (lanatullah) alitoa majeshi yamsaidie idd amin (lanatullah) kuivamia Tanzania

2.Madiba kama Nyerere na Nkuruma walitaka muungano wa afrika nzima bila kuingilia dini wala mila za watu lakini gadafi alitaka afrika iwe na dini moja na alikuwa anaendesha operation za wazi na za siri kufuta dini nyingine

3.Madiba alikuwa anaheshimu mataifa mengine na dini zao lakini gadafi alitinga roma akiwa amekodisha makahaba zaidi ya 500 wakiwa wamebebeshwa kitabu cha dini yake na kuzunguka navyo kwa maadamano lengo ni kuchokoza dini nyingine
 
Gaddafi alikuwa mpenda kiki zaidi, baada ya Warabu wenzake kumstukia ndipo alipogeukia huku Sub Saharan Africa ambapo alitumia umasikini wetu kujijengea "Cheap Popularity".

Pamoja na Libya kuwa na uchumi imara wakati wake lakini hakuna chochote Afrika ilinufaika nalo kiuchumi toka kwake.

Alichochea vurugu ktk nchi kadhaa kama Tchad, Sudan, Uganda nk, hata kule Liberia alichangia civil war iliyompachika Charles Taylor madarakani pia alikuwa na jukumu ktk mauaji ya Anuar Sadat kule Misri.

Gaddafi kamwe hatasahaulika kwa kupanga na kufadhili mauaji ya Lockabee kule Scotland na bila kusahau maelfu ya Walibya waliyokimbia utawala wake hali iliyopelekea kufa kifo cha aibu kwa kuopolewa toka kwenye culvert ya maji taka na kuuliwa kinyama.

Wapo wachache watakaomkumbuka labda kwa kuwajengea majengo ya ibada na kushiriki ktk propaganda za kueneza imani ya kidini.

Lakini Mandela labda sifa yake kubwa ilikuwa ni kutokulipiza kisasi dhidi ya makaburu na kutokuwa na tamaa ya madaraka kama Gaddafi na wengine, ila alishindwa kukemea uimla wa ma-dikteta wa Kiafrika.
 
Muamar gadafi....huyo Mandela "ushujaa" wake ni kukaa jela mengine aliyoyafanya ni ya kawaida sana, tena yalifanywa na wapigania Uhuru wenzie
Tafadhali usimlinganishe huyo gaidi Gadafi na Icon wa dunia Mandela! Sheeee

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Gadaf yule aliwauwa vijana wetu vita ya Kagera au mwingine au kwasababu kawajengea misikiti ndio kawa shujaa labda shujaa wenu kwangu mimi huyu ni gaidi sawa na Osama.

Gadaffi namfananisha na MFALUME WA SOKA KUWAHI KUTOKEA HAPA ULIMWENGUNI.Argentina/Barcelona

Mandela namfananisha na BEKI WA BARCELONA MBOVU KUWAHI KUTOKEA HAPA ULIMWENGUNI,,,JEREMY MATHIEU
 
gadAFI kwasababu aliitoa nchi kwenye umaskini na kuipeleka katika maisha bora

baada ya kifo chake libya haijawah kuwa na maisha bora kama mwanzoni
ila kwa madiba hali ni ilele tu hata alipokufa
 
Baadhi ya mambo Ghadafi alifanya kwa Afrika

1. Kufinance vikundi vya wapigania uhuru, ANC ikiwemo

2. Kulipia Satellite ya kwanza ya Afrika, hii ilirahisisha mawasiliano ndani ya Afrika, gharama zikawa nafuu, Zamani ilikuwa ukipiga simu, ilikuwa kwanza iende ulaya kisha ndo irudi Afrika, sasa hivi ni direct tu.

3. Kufinance Africa Union ( AU) kifedha ili iweze kusimama

4. Kuinvest katika mataifa ya Africa, Hata sisi hapa Tanzania tulikuwa na hoteli zinazomilikiwa na serikali ya Libya mfano Bahari beach.

5. Kutoa pesa ndefu kwa ajili ya Africa development Bank ( ADB) ambapo nchi kibao za Afrika hukopa

6. Alikuwa na mpango wa kufinance uanzishwaji wa Africa Monetary Fund ( AMF) kama ilivyo IMF, wazungu wakamuona tishio wakamtengenezea Zengwe!!
 
MWARABU kamwe hawezi kua SHUJAA WA AFRIKA WALA WA DUNIA.
INYESHE MVUA, LIWAKE JUA..

Waafrika acheni kuichafua Historia Tukufu ya MTU MWEUSI. Huyu ndiye shujaa WA Dunia Nzima.

Hakuharibu nature ya uumbaji
Hakuigawa afrika wala dunia na kui colonize.
Hakuleta ugaidi,
Hakuleta Ukimwi.
Hakuleta Utumwa
Hakua Mlawiti
Hakua mnyonyaji
Hakua mpenda Vita.
Hakua muuaji.

Mpaka sasa yeye sio anayechangia Uharibifu wa hali ya hewa kwenye Sayari yetu.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom