Pombe ilikufanya kitu gani mpaka ukasema sasa rasmi naacha?

Kwa vile umeamua kunikumbusha basi haina shida lakini binafsi sitaki hata kukumbuka

Mara ya mwisho kugusa pombe ilikuwa ni mwaka 2015 sasa ilikuwa hivi

Jamaa angu alikuwa na kasherehe kakiaina basi akanialika kwa kuwa ratiba yangu




haikuwa ngumu sana na sikuwa nimebanana sana ikabidi niende

Basi bhana nimefika pale, nikakuta kuna kila aina ya vinywaji halafu mimi mda huo nilikuwa nina mda sijagonga vyombo

basi nikagonga bia ya kwanza,ya pili,ya tatu naona hata dalili ya kulewa hamna si unajua raha ya pombe ulewe

Basi nikaamua kugeukia za kienyeji {hapa ndo nilipobugi}

Basi nikaanza kuzifakamia kwa fujo

Nilipoona nimetosha nikasema ngoja ninyanyuke niende nyumbani nakuja kunyanyuka nashangaa mwili unaanza kuyumba nikajisemea enhheee kumekuchaaa na makucha yake

halafu mud a jhuo ukimuangalia mtu unaona kama wako wawili

Nakipiga hatua mbili mbele narudi hatua tatu nyuma nikajesemea leo kazi ipo


Kiufupi nilifika nyumban nishadondoka vya kutosha nadhani na ile kuchanganya vinywaji ikapelekea kutapika sana toka hiyo siku nikasema hapana

Halafu muda huo najiona nina nguvu nyingi maskini kumbe hata ukija upepo wa kisulisuli unapita na mimi
 
Hiyo ya kubolt usipende sana

Pendelea kwenda sehemu na mtu asiyeTumia sana

Mimi pombe siachi..

Ila tukio moja lilinifundisha kunywa kwa nyumba

Ilikuwa hivi :

Nimetoka home kwa kero zangu nikaona Ngoja nikajilipue nitulie.!😎

Khee kumbe wakati nakata vitu kwa hasira nahisi nilizidisha

Nikaona imetosha Ngoja nichukue boda anisogeze stendi huku chimbo sana

Nikahisi mkojo wakati kanibeba nikamzuia asinifikishe stendi nikataka kukojoa sehemu isiyo na mwanga (napajua)

Kidaraja fulani kina maji yanapita kwa chini na waswahili waligeuza jalala nikasema hapahapa🀭

Lilikuwa kosa kubwa la kiufundi sana ila nahisi vitu vilikuwa high.!

Babuu.! Ile nilikanyanga sehemu nikajua pagumu.! Kumbe fuko la takataka laini tu.! Wacha nibingilike kwenda chini.!

Ile najipata.. sijui kama niko kwa ardhi au bado napaaa.! 🀭

Nikaangalia kwa makini lile eneo nikao kweli nipo chini ila ajabu sikuumia

Toka siku hiyo niliapa kunywa kwa Nyumba
 

Mzee ww Pombe uache 😊😊😊😊.
Unajiaibisha sana
 
Hapo umepiga penyewe.... Kwenye issue ya pombe hasa tunaokaa usiku mnene... Bolt ndo suluhisho tosha na usalama ni uhakika zaidi
 
Mzee we ndo unatakiwa uache mkuu maana inakupeleka mputamputa na usipowaka unakuwa makini kweli au. 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…