Pombe kali za bei rahisi zinaliharibu taifa letu. Vijana wanahariba afya. Nguvu kazi ya taifa inatekeketea

Pombe kali za bei rahisi zinaliharibu taifa letu. Vijana wanahariba afya. Nguvu kazi ya taifa inatekeketea

IMG_0820.jpg
 
( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )

المائدة (90) Al-Maaida

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.

Ongezea na hii
Kumbe hilo likitabu kuna mda linasema vya maana
 
Hizi pombe ni kali zaidi hata ya gongo.

Zinaharibu afya ya vijana wengi. Nguvu kazi ya taifa.

Vijana wanakauka. Wanakunywa bila kula. Zinaharibu kila kitu maana wanashindwa hata kuperform kitandani.
Umeongea kwa uchungu sana hili jambo limenigusa hata mimi maana nina ndugu yangu kakauka vibaya mno maana anatumia hivi vilevi vya bei rahisi bila kula yani ata ongea ishabadilika ata kama hajanywa anakua kama kanywa yani kawa kama ndoige akinywa anakua kama kanywa au asipokunywa ni kama kanywa
 
Inabidi tu discuss solution ni nini na sio kuzitaja tu kinachowasumbua hapo ni kitu kinaitwa URAIBU. URAIBU Ni ile hali ya kuongozwa au kuwa chini ya kilevi flani ndio mambo yaende yaani ubongo unakuwa umeshazoea ukiweka kilevi ndo utafanya kazi, au kupata comfidance hata ya kuamua jambo,wengi wao ukiwakuta asubuhi ata kushika glass huwa hawawezi, wanakuwa wanatetemeka mikono, yaani mwanzo unakuwa unaiongoza pombe baada ya muda inaanza kukuongoza wewe, kifupi ni mateso na njia ya kumnasua mtu mwenye tatizo hilo ni kumpeleka vituo vinavyoshughulika na maswala ya URAIBU na pia muhusika awe tayari kuacha na kubadilika!
 
kifupi hata hizo pombe kali za bei ghali nazo nyingi zake ni fake labda ukazinywe new africa, hyatt nk ila huko kwingind eti unauziwa Jack D au Hainessy vingunguti au Tabata unatambaa mwenyewe umelipa 100k unajiona mwamba kumbe umeuziwa gongo ya mavi kutoka chanika....
 
Nenda kanunue kwa dealer wanakueleza ukweli kabisa hii famba na hii yenyewe kama kawaida hunuki mdomo na hangover huipati
 
Back
Top Bottom