Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupatie kaushuhuda kidogo mkuu, mimi nimetoa ushuhuda wangu huo.Sitaki kabisa kukumbuka madhira ninayo yapataga baada ya kutwika mtungi.
Achana na mitungi fanya ishu zingine.....Nianzie mbali kidogo. Moja ya maazimio yangu kufikia January 1 mwaka huu ilikuwa ni kuacha kabisa pombe na kampani ya walevi. Pombe imenisababishia madhila kibao katika maisha ikiwamo kushusha heshima yangu kazini na jamii inayonizunguka huko mtaani, kunitenga na Mungu wangu kiroho, kunirudisha nyuma kiuchumi, mafarakano na Mke wangu na aibu nyingine kede kede.
Ilifika January mosi na kweli nilifanikiwa kuacha pombe kwa takribani mwezi mzima wa January. Kimbembe kilikuja ilipofika mwezi February tarehe ya kuazimisha siku yangu ya kuzaliwa! Hapo ndo kama nilizaliwa upya na pombe huko uchagani nikiwa na kina Shirima, Lyimo, Shayo, Minja, Urassa na Mshana. Toka siku hiyo nimekuwa mraibu mkubwa sana wa haya mapombe ila naamini ipo siku nitaacha, ngoja kwanza nianze kujitenga na kampani za wanywaji kina Mshana Jr
Niende moja kwa moja kwenye point sasa.
Jana majira ya saa6 mchana nilitua uwanja wa ndege wa JNIA nikitokea bara Uropa kwa kazi fulani iliyochukua kama wiki moja. Nilipokelewa airport na rafiki yangu Bwana Lyimo na tukaenda moja kwa moja katika mghahawa fulani maeneo ya external kupata ugali nyama choma kabla ya kuanza kupiga vyombo. Baada ya msosi tuligonga vyombo viwili vitatu kusogeza muda.
Majira ya saa 12 hivi jioni tulihamia Julliana maeneo ya Africana Mbezi huku nikiwaalika wanywaji wengine 6 jumla tukawa nane.
Kiufupi nilikuwa na vidola kadhaa nilivyolipwa kwa safari ile nikaona sio mbaya tukinywa na marafiki huku tukipiga story mbili tatu za maisha. Watu walilewa vya kutosha kufikia saa8 usiku kila mmoja akaanza kutoroka bila kuaga.
Majira ya saa11 kasoro alfajiri tulikuwa tayari tumeshapauka vya kutosha mimi na Bwana Lyimo hivyo tukaona ni wakti muafaka wa kurejea nyumbani kulala.
Kwa kuwa kwa Bwana Lyimo ni maeneo jirani tu amepanga katika moja ya apartments fulani Mbezi Makonde niliona sio mbaya nikipumzika kwake then mchana nikishakaa sawa niondoke kuelekea Kigamboni.
Lyimo alinionesha chumba cha kulala nikaingia kupumzika. Dakika chache niliamka kwenda kuchukua simu niliisahau kwenye gari.
Mle kwenye gari kulikuwa pia na chupa kadhaa za vyombo tulivyoshindwa kumaliza tukavibeba. Uroho wa pombe nikaanza tena kuvipiga pale pale. Eh kidume kichwa kikawaka nikasahau hata nyumba ya Lyimo ni ipi nikajikuta nimeenda kuingia nyumba nyingine ambayo mwenyeji wake alisahau kufunga mlango kwa kuwa naye alikuwa vyombo.
He he he! Ishu iko hivi, mwenye nyumba niliyoingia ni mwanamke, mama mtu mzima kidogo ila anaishi na dada wa kazi na wanae wawili wadogo.
Huyu mama huo usiku alikuwa ametoka kwenye shughuli ya harusi, na huko naye alipiga vyombo vya kutosha akawa ndwiii! Alipofika kwake kwa hali ya ulevi alijibwaga chumbani akaacha milango bila kuilock na funguo. Mimi huyooo hata sijitambui, nikafungua wa sebuleni, nikafungua wa chumbani nikakuta jimama jeupe, limenona vyema. Eh pombe sio chai wakuu, nikapanda kitandani nikamvuta na yeye bila hiyana akanikumbatia tukalala fofofo! Saa 1 dakika 40 asubuhi simu yangu inaita nikashtuka, mama naye akashtuka.
Eh tukabaki tunaangaliana tumeduwaa. Mimi sijijui nipo wapi, yule mwanamke simjui, nashindwa kukumbuka imekuwa kuwaje mpaka tupo pale pamoja.
'Wewe! Umeingia ingiaje kwangu? We ni nani? He wewe?'- Aling'aka yule mama akiwa ameduwaa. Akiwa ameshashuka chini kasimama pembeni ya kitanda anatetemeka alinifokea nitoke ndani kwake haraka sana.
Hapo akili zikiwa zimeanza kurudi moja moja nilimjibu kwa upole kuwa mi mgeni wa Lyimo, na hapo nipo kwa Lyimo, ninachokumbuka ni kuwa nilikuwa nimelala mwenyewe, nikaamka kwenda kwenye gari kufata simu, nikaongeza na pombe na hapo ndo mwisho wa kumbukumbu zangu hata nashangaa imekuwaje nipo tena ndani na mwanamke. Akaniuliza kama tumesex nikamjibu sidhani, akajikagua kuhakikisha.
Hapo bado nina pombe, Lyimo ameshaamka, mkewe ameshaamka yupo hapo nje, watoto wameshaamka, kiufupi ni aibu!
Yule mama akatoka akaenda kuongea na Lyimo na mkewe, sijui waliongea nini Lyimo akanifata ananicheka hana mbavu.
Basi bwana nikatoka nayumba yumba na wenge la pombe. Kwa aibu na fedheha nikamsalimia mke wa Lyimo, nikamwambia "Shemeji utanisamehe sana kwa hili, sikuwa na nia mbaya ni matokeo ya mapombe tu haya, hatujafanya kitu. Naomba kwanza niende, pombe zikiniisha tutazungumza."
Basi Bwana nikaenda chumbani kuvaa shati na viatu kisha tukaondoka na Lyimo Kwenda pub fulani jirani kutia vyombo viwili vitatu huku nikimueleza kuwa nilitoka kufata simu kwenye gari na baada ya kunywa tena ndipo nilipojikuta naamka nyumba nyingine tena nikiwa na mwanamke kitandani na wakati hapo awali nilikuwa mwenyewe.
Lyimo akaniambia nimechanganya nyumba, na huyo mama ni mjane, mumewe alifariki kwa ajali mwaka jana. Huwa hatumii sana vilevi ila huo usiku inaonekana alionja viwili vitatu kwenye harusi.
Nilimueleza kuwa sijagonga na akirudi home anisaidie kuniombea msamaha kwa shemeji asinielewe vibaya, sikudhamiria.
Mkuu, hiyo kuacha pombe watu tunatamani sana.Achana na mitungi fanya ishu zingine.....
Mitungi waachie wengine.....
Unywaji ni formula....ni kama pai D square over four....Sitaki kabisa kukumbuka madhira ninayo yapataga baada ya kutwika mtungi.
Kwanza niweke wazi pombe sio Dhambi....Mkuu, hiyo kuacha pombe watu tunatamani sana.
😅😅😅😅Pombe pombe pombe nakuita Mara tatu
The best han'g over is the promice of never drinking againTunapata sana fedheha kwenye pombe, tukiamka asubuhi tunaapa kuacha ila ikifika jioni tumo tena tunapiga vitu. Dah hii kitu ni utumwa sana.
Halafu sijui kunakuwaga na uhusiano gani kati ya giza na kulewa.Unanikumbusha kuna miaka ya nyuma nilienda kwenye party ya ubatizo wa mtoto wa mshikaji.
Tulipiga sana kinywaji siku hiyo unajua nikawa maji ile ya ndembe ndembe.
Sasa kuna mke wa mshikaji mojawapo aliyekuja kwenye party. Mimi naenda zangu kumwaga reserve kwenye bustani na yeye akanifata.
Akaja mbele yangu akashusha jeans yake akaanza kushusha mkojo shwaaaaaaaaaaaah .
Nikaropoka khaaaaaah wewe, sasa mbona mbele yangu tena [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Akanijibu kwani wewe hadi umri huu kuna nini cha ajabu kwa mwanamke haujawahi kiona hadi ushangae kwangu?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah nikacheka sana akanambia shiiiiiiiiiiiiiiii [emoji2958] siri yetu usimwambie mtu. Huku anaendelea kukojoa. Akanambia usiondoke hadi nimalize tuondoke sote nisije nikang'atwa na nyoka.
Dah nikikumbuka nacheka sana. Yaani imagine anapandisha fulana na kufungua jeans mbele yangu huku naona anashusha jeans na chupi na kuchuchumaa mbele yangu.
Nikasema pombe aiseee unatakiwa uwe makini sana aiseee. Ile siku ndio siku ambayo niliendesha gari kwa kutumia akili kuliko siku zote hapa Duniani. Maana mida ya saa nane usiku, mwenyeji wangu baada ya kufunga sherehe tukaagana nikajimwagia maji ya baridi kichwani, nikaingia kwenye gari nikalock milango yote, nikavaa mkanda kwanza, nikawasha gari, nikashusha vioo vya mbele tu kidogo sana.
Nikaanza kurudi reverse taratibu na kwa umakini kwa msaada wa mwenyeji wangu, hadi nikatoka getini. Aisee niliposhika lami. Nilikuwa naendesha huku nasali ile sala aliyotuelekeza mwokozi isemayo, "baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike Duniani kama huko mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe na sisi wale waliotukosea, usitutie katika kishawishi, lakini utuokoe maovuni, Amina".
Nikatia ishara ya msalaba halafu nikalamba lipsi,ili kutoa wenge halafu macho mbele, speed ya msiba yaani siendi above 40. Macho yanapapasa kama camera ya ulinzi kila upande ili nisije chomeka gari akatokea mlevi mwenzangu tukapeana kubum kubam ya mabampa. Ila MUNGU ni mwema , nilifika salama salimi hadi kuingia ndani nikalala na kuamka asubuhi sana kutafuta supu.