Pombe sio chai. Nililala mwenyewe nimeamka na Mama mwenye nyumba, tunashangaana!

Achana na mitungi fanya ishu zingine.....

Mitungi waachie wengine.....
 
Unanikumbusha kuna miaka ya nyuma nilienda kwenye party ya ubatizo wa mtoto wa mshikaji.

Tulipiga sana kinywaji siku hiyo unajua nikawa maji ile ya ndembe ndembe.

Sasa kuna mke wa mshikaji mojawapo aliyekuja kwenye party. Mimi naenda zangu kumwaga reserve kwenye bustani na yeye akanifata.

Akaja mbele yangu akashusha jeans yake akaanza kushusha mkojo shwaaaaaaaaaaaah .

Nikaropoka khaaaaaah wewe, sasa mbona mbele yangu tena [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Akanijibu kwani wewe hadi umri huu kuna nini cha ajabu kwa mwanamke haujawahi kiona hadi ushangae kwangu?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah nikacheka sana akanambia shiiiiiiiiiiiiiiii [emoji2958] siri yetu usimwambie mtu. Huku anaendelea kukojoa. Akanambia usiondoke hadi nimalize tuondoke sote nisije nikang'atwa na nyoka.

Dah nikikumbuka nacheka sana. Yaani imagine anapandisha fulana na kufungua jeans mbele yangu huku naona anashusha jeans na chupi na kuchuchumaa mbele yangu.

Nikasema pombe aiseee unatakiwa uwe makini sana aiseee. Ile siku ndio siku ambayo niliendesha gari kwa kutumia akili kuliko siku zote hapa Duniani. Maana mida ya saa nane usiku, mwenyeji wangu baada ya kufunga sherehe tukaagana nikajimwagia maji ya baridi kichwani, nikaingia kwenye gari nikalock milango yote, nikavaa mkanda kwanza, nikawasha gari, nikashusha vioo vya mbele tu kidogo sana.

Nikaanza kurudi reverse taratibu na kwa umakini kwa msaada wa mwenyeji wangu, hadi nikatoka getini. Aisee niliposhika lami. Nilikuwa naendesha huku nasali ile sala aliyotuelekeza mwokozi isemayo, "baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike Duniani kama huko mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe na sisi wale waliotukosea, usitutie katika kishawishi, lakini utuokoe maovuni, Amina".

Nikatia ishara ya msalaba halafu nikalamba lipsi,ili kutoa wenge halafu macho mbele, speed ya msiba yaani siendi above 40. Macho yanapapasa kama camera ya ulinzi kila upande ili nisije chomeka gari akatokea mlevi mwenzangu tukapeana kubum kubam ya mabampa. Ila MUNGU ni mwema , nilifika salama salimi hadi kuingia ndani nikalala na kuamka asubuhi sana kutafuta supu.
 
Halafu sijui kunakuwaga na uhusiano gani kati ya giza na kulewa.

Kula pombe asubuhi mpaka jioni hauelewi, ila kula pombe jioni jioni tu uone, yaani ikifika saa4 saa5 tayari unapauka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…