Pombe ya viroba sasa inaitwa "visungura", Serikali ichukue hatua haraka vijana wanapotea kwa kasi

Pombe ya viroba sasa inaitwa "visungura", Serikali ichukue hatua haraka vijana wanapotea kwa kasi

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Ni viroba katika chupa za plastiki zenye kilevi cha 40 kikiwa kidogo unaweka hadi mfukoni hata mtoto anaweka, wanasema havina harufu kali so unaweza ukawa na mtu karibu anaongea upuuzi usijue kama kalewa.

Boda boda, machinga, wapiga debe na walevi wa kiwango cha umaskini ndio chao kwa bei ndogo vijana wanapotea maana kinaunguza maini na mfumo mzima wa afya ya akili na uzazi.

Serikali ipige marufuku hivi vidude vitaua vijana.

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wazima kufundishwa kulinda afya zao kweli? Mtu makitu hayo ni makali, yana ladha kali unayanywa utadhani yanakupa virutubisho mwilini ile hali yanakuletea maradhi mwilini siku za baadae kwasababu ya kuchosha viungo muhimu vya mwilini.

Nadhani ifike muda hili jukumu la kukemea matumizi ya bidhaa haramu libakie ngazi ya familia, nyumba za ibada na hata mitaala ya elimu iwaelimishe watoto juu ya madhara ya hizi vitu kama wataanza mazoea ya kujihusisha navyo.
 
Malezi ya watoto toka wakiwa wadogo
 
Ikiitwa Valuer, Grants, Black label, Green label, Gordons, John Walker, Cîroc, Captain Morgan, Jack Daniels, Fireball, Hennessey, Vodka, ..e.t.c. inakuwa siyo shida?
Au tatizo vifungashio?
Babu zenu wamekunywa, gongo, nipa, lubisi n.k, hawakufa.
Acheni hizo mambo.
Kila mtu na anywe kwa upana wa mfuko wake.
Kwanza wana waunga mkono wenye viwanda vya ndani siyo kila siku kumchangia beberu na mrusi.

Kama kiwango cha alcohol hakijazidi kinacho ruhusiwa kwa matumizi ya vinywaji vikali hakuna shida. Ipo taasisi inayo pitia viwango na kuhakiki usalama wa watumiaji pombe.
 
Ikiitwa Valuer, Grants, Black label, Green label, Gordons, Joh Walker, Cîroc, Captain Morgan, Jack Daniels, Fireball, Hennessey, Vodka, ..e.t.c. inakuwa siyo shida?
Au tatizo vifungashio?
Bubu zenu wamekunywa, gongo, nipa, lubisi n.k, hawakufa.
Acheni hizo mambo.
Kila mtu na anywe kwa upana wa mfuko wake.
Kwanza wana waunga mkono wenye viwanda vya ndani siyo kila siku kumchangia beberu na mrusi.

Kama kiwango cha alcohol hakijazidi kinacho ruhusiwa kwa matumizi ya vinywaji vikali hakuna shida. Ipo taasisi inayo pitia viwango na kuhakiki usalama wa watumiaji pombe.
Mkuu kwa comment yako hii unaingia mbinguni moja kwa moja! Kuna watu wanajitwisha mapombe ya Russia kila siku lakini sijaona wanakemewa lkn huyu mkombozi wa mnyonge wananza kumwandama.
 
Back
Top Bottom