Pombe ya viroba sasa inaitwa "visungura", Serikali ichukue hatua haraka vijana wanapotea kwa kasi

Pombe ya viroba sasa inaitwa "visungura", Serikali ichukue hatua haraka vijana wanapotea kwa kasi

Watu wazima kufundishwa kulinda afya zao kweli? Mtu makitu hayo ni makali, yana ladha kali unayanywa utadhani yanakupa virutubisho mwilini ile hali yanakuletea maradhi mwilini siku za baadae kwasababu ya kuchosha viungo muhimu vya mwilini.

Nadhani ifike muda hili jukumu la kukemea matumizi ya bidhaa haramu libakie ngazi ya familia, nyumba za ibada na hata mitaala ya elimu iwaelimishe watoto juu ya madhara ya hizi vitu kama wataanza mazoea ya kujihusisha navyo.
Really? hivi unadhani wahusika/wahanga wakubwa kwenye hili ni nani kama si vijana? Tumeambiwa kwenye sensa ya hivi karibuni kwana zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ni vijana.

Tukisema tuache hivi hivi bila kukemea taifa litaenda wapi? Sasa hivi tuna shida kubwa sana kama taifa la kuparomoka kwa maadli.

Bodaboda unakuta anapiga hizo smart gin anachanganya na energy drinks halafu akitoka hapo anaenda kubeba abiria, tena mishikaki na kushindwa kufuatilia sheria za usalama barabarani.
 
Mi nafurahi sana watu wakifa kwa ujinga wao wenyewe.
Nafurahi sana

Nasikitika mtoto mdogo kufa sababu hajui kitu chochote.
Mtoto kuanzia 0-5 kufa naumia sana.
 
Ngoja twende Muhimbili tufanye utafiti tuone waliolazwa kwa magonjwa tajwa hapo juu kama walikuwa wanatumia kitu kama "Visungura" au ni story tu!
Hivyo kwa vijana matokeo yataonekana miaka 20 ijayo, ila waendesha boda boda matokeo yaweza kuwa ndani ya dakika 01
 
Maeneo mengine vinaitwa Bomu na mwingine vinaitwa chaji ya kichwa.
 
Mkuu kwa comment yako hii unaingia mbinguni moja kwa moja! Kuna watu wanajitwisha mapombe ya Russia kila siku lakini sijaona wanakemewa lkn huyu mkombozi wa mnyonge wananza kumwandama.
Swala sio pombe ya wapi,hapa watu wanapigia kelele unywaji wa hizo pombe,unakuta mtu tokea asubuhi anakunywa kila baada ya masaa mawili.

Nakumbuka jamaa mmoja miaka ya nyuma kutokana na frustrations za ndoa alipiga zinga la JohnWalker lote,yule jamaa alizimia kwa muda wa wiki 2 huku akipatiwa matibabu ya gharama sana, bahati nzuri siku yake naona ilikuwa haijafika akapona.

Kwahiyo nadhani kunahitajika elimu ya unywaji wa hizo pombe na madhara yake kwa jamii na hasa vijana.
 
Back
Top Bottom