Hakuna taifa haramu duniani, waliofeli ni wale waliopewa dhamana ya kutunza amani ya dunia, kwa sasa naona kama hakuna taifa la Palestine kwenye ramani ya dunia.
Na hilo ndo ilikuwa lengo kuu, na imetimia tayari bila shida, muhimu waislam na taasisi zao zote duniani ikubaliane na hili na ionyeshe kushirikiana na Israel kwa maslahi mapana ya waarabu wale wabaki na wapewe haki ya kuwa raia wa taifa la Israel ok.
Lakini kuendelea kupambana wakati tayari mmeshamezwa na na tayari mipaka ya nchi iliokuwa yenu haijulikani na haitambuliki tena kimataifa ni kutafuta tatizo lingine.
Why nasema haya, Palestine sio nchi tena hapa duniani bali ni eneo lenye mamlaka ndani ya taifa la Israel, hivyo basi waarabu wale waamue kufuta hiyo eneo lenye mamlaka ili wachukue utaifa wa Israel waijenge Israel yao kwa pamoja.
Katiba iandikwe upya ya Israel baada ya waarabu kuamua kufanya mamuzi magumu itakayo watambua na kulinda haki yao kama raia wa taifa la Israel.
Ila najua wengi watapinga coz ni wafia dini, na wanao nufaika na waarabu wale wa Palestine najua hawawezi kukubali hili coz watakatiwa mirija yao ya ulaji.