Ponda afungwa mwaka mmoja Jela wengine waachiwa huru

Status
Not open for further replies.
Nikisema eti amependelewa nitakuwa natumia akili ndogo ya kutaka binadamu mwenzangu ahukumiwe na kuteseka kwa kosa ambalo limeonekana kuwa kubwa, hivyo nikiri kwamba naheshimu maamuzi ya mahakama.
 

Serikali ikate rufaa kwa Rwakatare kwanza kwa kufutiwa kesi ya ugaidi wakati CD wanazo na kila kitu,
 
Allah alisha sema haki na batwili haviwezi kaa pamoja. Kafungwa japo mwaka mmoja ili BAKWATA na BARAZA LA MITIHANI NECTA wapate japo amani ya muda mfupi
Huko unakoelekea sio kuzuri, hata Waziri wako wa Mambo ya Ndani jana tu ameonya watu kama wewe waache kauli za uchochezi.
 
Serikali ikate rufaa kwa Rwakatare kwanza kwa kufutiwa kesi ya ugaidi wakati CD wanazo na kila kitu,
Hapo amelindwa mtu mwenye Migulu ya Chemba, unafikiri Lwakatare akishtakiwa kwa ugaidi yeye atapona.
 
Ha haa! maoni mengi humu yamenifurahisha,ila cha msingi ni ponda kuwa mpole maana hivi sasa serikali ina hasira na issue za ugaidi,akileta tena kelele watamkamata na atapotea moja kwa moja.
 
Sawa sawa mkuu, lakini unajua kuwa katika taasisi zinazoongoza kwa rushwa nchini, mahakama ipo juu?

KWa hiyo unataka kutuambia hata RWakatare jana aliachiwa kwa Rushwa? Kesi za kina Lema pia huwa wanapokea Rushwa ? hivi hii nchi inakwenda wapi? Rwakatare amekamatwa na CD zipo mmebadili na kusema ni software, ila kina Ponda wanastahili chuki ya udnini itawamaliza nyie na wakuu wenu, nimeshangaa sana jana kuona Pengo akitoa siri kuwa dharuba ile ya Arusha sio ya kidini lakini anatafuna maneno , kwanini asiseme ukweli anaojua? nimrule out kuwa anapenda chuki za kidini ziendelee, simply angetoa huo ukweli aloambiwa na mtu alompigia simu lakini akaishia tu kusema si shambulio la kidini hii nchi tunapokwenda sipo kabisa ! nadhani wachocezi wakubwa ni hawa hawa viongozi wa kidini !
 

Shehe Ilunga naye ameachiwa Huru au bado anapeta mitaani.
 
Ponda atakuwa zezeta soon hamtamsikia tena mbwembwe zote kwishneyyy
 
Naona watu wenye chuki wanatamani wapasuke kusika amepewa kifungo cha nje!!

Hata huyu mwandishi wa mada hii hapo kwenye kichwa cha habari ameandika ponda ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja JELA ilhali sio jela bali ni kifungo cha nje!!

Hongera mahakama kwa kutenda haki!
 
Kila mara nasisitiza Watanzania tupendane,tuheshimiane, na katu mmoja wetu asifurahie mwenzake anapopatwa na janga.Wapo wana jamvi ambao wao huweka mbele zaidi imani zao,tena kwa namna ya kuudhi imani nyingine,wakifiki kwa kufanya hivyo mama yetu Tanzania atadumu na kusimama,nao wapate nafasi ya kufanya wanayoyataka.WANAJIDANGANYA!!!Narudia,tusiposhikamana na kurudi enzi za Juma na Rosa,tunawatengenezea watoto wetu dimbwi kubwa la damu(Mwenyezi Apishie mbali)Mwislam ni lazima aheshimu matukufu ya Mkristu,na Mkristu pia ni lazima aheshimu matukufu ya Mwislam.Sisi sote ni Wana wa Ibrahim(amani iwe juu yake).Inanishangaza sana tunasahau asili yetu.Tukipendana Mwenyezi Mungu Atateremsha baraka Zake na nchi yetu itameremeta.Maadui wanajua Mwenyezi Ametupa mali asili nyingi,hali ya kua wao hawakupewa.Wamejaribu sana kutugawa wameshindwa.Sasa wanatumia dini.Sisi badala ya kushituka,bila kujijua tunashangilia.Tuamke leo maana huenda kesho ikatukuta tumechelewa.Tumsifu Yesu Kristu,Asalaam alaykum
 
Mahakama imetenda haki na kuwa na busara ya kuifichia serikali aibu. Ponda hana hatia ni msemaji mzuri wa waislam. Yeye hajachakachuliwa kama wengine hawa wanaopanda kwenye STK na kulipwa mishahara na serikali.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…