Ponda afungwa mwaka mmoja Jela wengine waachiwa huru

Ponda afungwa mwaka mmoja Jela wengine waachiwa huru

Status
Not open for further replies.
Muda si mrefu Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imemhukumu shehe Ponda kifungo cha Miezi kumi na miwili na wenzake wameachiwa huru.
Sasa kama alikuwa gaidi na akanyimwa dhamana na Serikali hii imeshindikana nini kumfunga?Hao walioachiwa huru yafaa walipwe maana wamekaa ndani huku wakiwa hawana makosa.
 
Toka tarehe 05 mi mwenzenu nimesahau hata jina la nchi yangu. Sijielewi sijui nipo Somalia
Maydei maydei .................Satelite ilipoteza signal kdg mkuu ila upo bng kwa ss!
 
Wamemhurumia sana huyo, wangempiga hata miaka miwili jela. Kazidi kutuvurugia amani. Kifungo cha nje ni sawa na kutokumfunga tu.

Kama unamuombea binadamu mwenzako mabaya kiasi hiki.....
Mmmmhhh
Aya
 
Something is wrong somewhere...PONDA, LWAKATARE, FARIDI:- Hawa ni Magaidi? Ponda anadai Mali ya Waislam kwa manufaa ya Waislam dhidi ya BAKWATA Taasisi ya CCM. LWAKATARE amefanikiwa kuweka ulinzi imara dhidi ya hujuma zote za kuidhoofisha CHADEMA. FARIDI ameamua kuanzisha vugu vugu la kuwaamsha Wazanzibar Wadai Nchi yao inayomezwa na Bara yenye MAFISADI PAPA ...Why UGAIDI?
 
makanisa yaliyochomwa serikali imeshalipa fidia?
 
sibora angeendelea kuwa mahabusu kwa miezi sita kuliko kumtoa kwa kifungo cha mwaka nje!
 
Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam, imemfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda, huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru

..mlitegemea mahakama itoe hukumu ya aina gani? sishangai

Mali zilizoharibiwa na wafuasi wake nani atalipa?
 
sibora angeendelea kuwa mahabusu kwa miezi sita kuliko kumtoa kwa kifungo cha mwaka nje!
akili shetani roho shetani na maneno ya kisheta-ndiyo maana kwa ushetani huu mnaua watu kwa mabomu-jambazi wa kilimanjaro weeee.
 
Msije mkajidanganya eti yuko huru!
hakuna kifungo kibaya kama kifungo ch nje!

kwanza atakuwa ànakwenda kutumikia àdhabu ziwe za usafi au kupiga deki kulingana na atakavyopangiwa!
na akithubutu kufanya kosa dogo hata la kumtukana mtu kabla ya kumaliza kifungo,
hiyo itakuwa imekula kwake vibaya..

kwa sababu atakwenda kuongezewa mvua alafu safari hii itakuwa ni jera moja kwa moja!

sasa fanyeni ushabiki na mtu wenu..
rukeni rukeni binukeni..
ila àsije akathubutu akàandaa maandamano yeyote!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom