Ponda afungwa mwaka mmoja Jela wengine waachiwa huru

Status
Not open for further replies.
kwa kweli Ponda ni mwana haki wa kikweli hata kama angefungwa miaka mia lakin bado angekuwa ni mwanaharakati wa waislam ndo maana mahakama imaeamua kuchukua kifungo kama hiki cha style yake kwa heshima ya mzee Ponda.......na kuifungulia mashataka serikali...
 
ALLAH katuhaidi kuwa Kiama haitafika hadi Islam idominate the World, sidhani kama other people created religion mungu wao kawapa ahadi yeyote.. And Soon, Allah's promise will be fullfilled, no one to stop.. In Shaa Allah,
 
ni wakati wa ponda kuangalia nyendo zake za maisha na kuanza mfumo mpya wa maisha yake.
Maisha ya Shekh Ponda si lolote kwa Allah, Sema sasa ni muda mzuri wa Shekh Ponda kuendeleza harakati zake za kutetea na kulinda Uislamu.. In Shaa Allah
 
May Allah swt grant shekh ponda issa ponda good health and give him lots of shifa inshaAllah
 
Karibu uraian Sheikh..hope kesho tutakua pamoja katika swala ya ijumaa pale kichangani..Allah Akbar
 
kifungo cha nje ndio nini?

Kuwa nje ya gereza lakini kwa masharti maalum, mfano, kusalimisha pasi ya kusafiria, mahakamani, kutokufanya kosa jingine kama hilo au lolote ndani ya muda huo,kutosafiri nje ya mkoa bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa hakimu, au kituo cha jirani cha polisi, kila wiki, au siku..huo ndio mfano wa kifungo cha nje,
 
ALLAH katuhaidi kuwa Kiama haitafika hadi Islam idominate the World, sidhani kama other people created religion mungu wao kawapa ahadi yeyote.. And Soon, Allah's promise will be fullfilled, no one to stop.. In Shaa Allah,

Mkuu ulikua umejificha wapi mda wote, huo, naona kamradi kako sasa kamefufuka upya,
 





ndugu yangu hiyo quote nimeifurahia sana ungekuwa karibu ningekupa vocha ya tigo hata 500/= ila nakuombea kwa allaah akupe mafanikio ktk maisha yako
 
Kumbe hata majaji wakati mwingine uwa wanatumia busara zaidi kuliko sheria!!
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Law na Justice, Equality na Equity.
 
Allah Akbar........am more dan happy.....usiishie hapo Sh Ponda ni mwendo wa Mchaka Mchaka hatutak Masheikh Ramri wanaotumika na Serikal kuwakandamiza na kuwanyonya Waislam kupitia Bakwata ambacho ni chombo cha Serikal kwa kivuli cha Uislam
 
Hivi,kwanini vibaka wa kuku hawafungwi kifungo cha nje?kiukweli kifungo cha nje si maarufu Tanzania.Ila huu ni usenge yaani fujo zote ponda anapewa mwaka mmoja nje ya jela?mahakama haziko huru,kama hazitumikishwi na serikali na dini zinazipelekesha,kila kitu tunasikia iwe funzo kwa wengine,kwa nini isiwe funzo kwa ponda wakati ataendelea kuchochea vurugu?
 
Wafuasi wa Ponda jela
Ijumaa, Machi 22, 2013 05:46 Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam


*Ni kwa kuandamana kwenda kwa DPP kulazimisha Ponda apewe dhamana
*Yeye aendelea kujitetea mahakamani Kisutu, adai hakuchochea Waislamu


MAHAKAMA jijini Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja, watu 54 walioandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wakitaka Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aachiwe kwa dhamana.Hukumu hiyo iliyotolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Sundi Fimbo, kwa Salum Makame na wenzake 53 baada ya upande wa mashtaka na utetezi kufunga ushahidi mwanzoni mwa wiki.

Ponda na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kuingia kwa nguvu, kujimilikisha uwanja wa Markaz uliopo Chang’ombe na kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 59, mali ya Agritanza Limited.

Kesi dhidi ya Ponda na wenzake inaenedelea kusikilizwa katika Mahakama hiyo ya Kisutu wakati Ponda akiwa mahabusu baada ya kunyimwa dhamana.

Akisoma hukumu dhidi ya watu hao 54 jana, Hakimu Fimbo alisema, “Upande wa mashtaka ulileta mashahidi 10 mahakamani, mashahidi walitoa ushahidi wa kuonyesha kwamba washtakiwa walikula njama kutenda kosa la kuandamana, walikusanyika na kufanya maandamano, walikaidi amri halali ya polisi iliyowakataza kufanya hivyo na shtaka la mwisho ni kwa ajili ya mshitakiwa wa kwanza hadi wa tatu ambao wanadaiwa kufanya uchochezi.

“Katika shtaka la kula njama upande wa mashtaka umethibitisha bila kuacha shaka kwamba washtakiwa walikutana, wakakubaliana kufanya maandamano hivyo mahakama inawatia hatiani kwa kosa hilo.

“Shtaka la pili la kukusanyika na kuandamana pia limethibitika ingawa washtakiwa walijitetea lakini utetezi wao ulikuwa unajikanganya hivyo mahakama inawatia hatiani kwa kosa hilo.

“Mahakama iliangalia ushahidi kwa kosa la tatu la kukaidi amri halali ya polisi na imeona kwamba washtakiwa walipeleka maombi ya kufanya maandamano ya amani.

“Polisi waliyazuia kwa sababu hawakuwa na polisi wa kutosha lakini maandamano hayo yalifanyika baada ya kutoka msikitini kama barua yao ilivyokuwa ikijieleza… shtaka hilo limethibitika nawatia hatiani washtakiwa wote.”

Hakimu Fimbo alisema kwa shtaka la nne la uchochezi washtakiwa hawana hatia kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha shataka bila kuacha shaka.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Ladislaus Komanya uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Hakimu Fimbo akisoma hukumu alisema kwa kosa la kwanza la kula njama washtakiwa watakwenda jela mwaka mmoja, shtaka la pili pia watakwenda jela

mwaka mmoja na shataka la tatu watatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

“Adhabu hiyo itakwenda kwa pamoja na kama kuna mshtakiwa anaona hakutendewa haki anaruhusiwa kukata rufaa,” alisema Hakimu fimbo.

Washtakiwa walikamatwa Februari 15 mwaka huu na kufikishwa mahakamani wakituhumiwa kufanya maandamano haramu.

Wakati huohuo, KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Ponda Issa Ponda amedai kwamba hajawachochea Waislamu kuvamia kwa nguvu uwanja wa Markaz ulioko Chang’ombe.

Alidai mijadala yake na polisi ilianza tangu enzi za uongozi wa Hayati Mwalimu Nyerere.

Ponda alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa akiongozwa na Mawakili wake, Juma Nassoro na Yahya Njama.

Ponda na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kuingia kwa nguvu, kujimilikisha uwanja wa Markaz Chang’ombe na kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 59, mali ya Agritanza Limited.

Kwa mujibu wa Ponda, yeye na wezake, walifika katika uwanja wa Markaz Chang’ombe kwa ajili ya kujenga msikiti wa muda kwa ridhaa ya Agritanza Limited ambaye pia alichangia Sh 500,000.

“Tulitumia diplomasia kumaliza mgogoro wa uwanja baada ya kusikia Agritanza walibadilishana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)… tulikuna na Hafidh Suleiman wa Agritanza tukazungumza na kukubaliana ndani ya siku saba tuwatafutie uwanja mwingine Mkuranga, na eneo la Markaz tuendelee kujenga msikiti wa muda.

“Tulikubali kutafuta eneo tukifikiria kutatua mgogoro, taarifa za kujenga msikiti wa muda tulizitoa misikitini na waumini walijitokeza kwa wingi kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kushiriki ujenzi,”alidai Ponda.

Alidai ujenzi ulifanyika kuanzia Oktoba 12 na kumalizika Oktoba 14 mwaka jana na kwamba ujenzi huo ulikuwa unafanyika asubuhi hadi jioni na kuondoka.

Ponda alidai wakati washtakiwa wengine wakikamatwa hakuwapo eneo hilo lakini alisikia walikuwapo waumini ambao walifika eneo hilo kwa ajili ya kufanya ibada ya Itikafu.

“Shtaka la wizi hilo halipo kwa sababu hata Suleiman alipofika mahakamani alidai hakukuwa na wizi. Ili kuthibitisha huo wizi Jamhuri ilitakiwa kutumia busara kwa kuhamisha mahakama hadi eneo la tukio kisha Agritanza waangalie matofali yaliyoibwa kwao na kujengewa msikiti wa muda ni yapi.

“Suala la kuingia kwa nguvu katika uwanja wa Markaz halipo. Tuliingia vizuri, kila mtu aliruhusiwa kuingia, hakuna aliyekataliwa kuingia katika eneo hilo na kushiriki ujenzi,”alidai Ponda.
 
Wataalam wa saikolojia wanaweza kufahamu uwezo wa mtu kwa kupitia maandishi yake!
 

Alifanya fujo gani? Acha kukariri hata hicho kifungo cha nje ni dhulma tu, We mtu anunue Hecta 4 za Ardhi chang'ombe dsm kwa kubadilishana na pori la hecta 40 kisarawe ( thamani ya hkt 1 kwa sasa kisarawe ni tsh laki moja ikimaanisha hkt 40 ni 4 Million) unaona sawa? au nyie ndo Anti Islam kupitia Intelijensia yenu ya kudhoofisha uislam kwa Kifupi Bakwata!Katu hatusubiri ruhusa yenu kupigania Mali za Wakfu kama mnaipenda sana Bakwata igeuzeni kuwa Jumuiya ya Chama!
 
Baada ya Mahakama kuu ya Kisutu kumuhuku kifungo cha mwaka mmoja nje Shekhe Ponda... na kuwaachia huru wafuasi 49 wa Shekhe ponda baada ya Upande wa mashtaka kushindwa kuwasilisha Ushahidi wa kutosha kumtia hatiani ilikua ni furaha kubwa sana sio kwa Ponda na wafuasi wake pekee bali kwa Wapenda haki wote.

Akiongea na waandishi wa Habari Shekhe Ponda alisema kwamba vyombo vyetu vya usalama na Dolla havina uwezo wa kugundua mambo na badala yake wamekua wakiwabambikia watu Kesi za kutunga kwa Mashinikizo ya Viongozi kwa Maslahi ya Kisiasa.

Alichosema Shekhe Ponda ni Ukweli tena usiopingika. Ushindi wa Shekhe Ponda ni kitu nilitegemea kutokana na Jinsi najua kwamba Kesi iliyokua ikimkabili Ponda na Wafuasi wake hakukua na kosa la kumnyima Dhamana.lakini kwa kua Vyombo vyetu vya Usalama Vinatumika Kisiasa na sio Kisheria basi viliweza kufanya walichofanya.

Tulishuhudia hapo jana kufutiwa kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Wilfred Lwakatare kesi inayoitwa ya Kigaidi baada ya Mahakama kuona kwamba hilo kosa halipo na hakuna ushahidi wa uhalisia wa jambo lenyewe.

Huu ni ushahidi tosha kwamba Kesi ya Lwakatare ni ya Kisiasa na kwamba vyombo vya Dola vinafanya kazi kwa Mashinikizo ya viongozi wa SERIKALI NA CCM kama ambavyo alisema Shekhe Ponda.
 
Naunga mkono kauli ya Ponda bila kuhofia kwamba naweza kuudhi watu fulani.

-Nilishasema haikuwepo mantiki ya kumpa Lema dhamana kesi ya uchochezi na kumnyima Sheikh Ponda kwa kesi hiyo hiyo.Ni uonevu tu.Huu ndiyo msimamo wangu

NB:Mods acheni hii thread ijitegemee
 
ukweli na uongo ni vitu viwili tofauti hivyo haviwezi kukaa pamoja hata siku moja. ukweli ukidhihiri uongo hujitenga kama mafutaa na maji.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…