Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Salaam
Kwanza nikiri wazi kwamba mimi sio mwanajeshi kuweza kuufahamu utendaji wa ndani kabisa wa CDF wetu wa JMT lakini kwa jicho la nje ningependa kutoa pongezi nyingi kwake kwa utendaji na uzalendo uliotukuka.
Mbali na utendaji wake ndani ya jeshi, Kiongozi huyu ameonekana sehemu mbali mbali akitoa mchango wake katika jamii katika kuhakikisha ustawi wa kifikra, kiuchumi,na maendeleo ya jamii kiujumla.
Kwa namna hii ya viongozi kujishusha na kuwa karibu zaidi na wananchi na kuweza kusaidia pale ambapo anahisi kwa kadri ya uwezo wake na nafasi aliyonayo anaweza kutoa msaada ni jambo la mfano na kuigwa na kiongozi yeyote. Na huu ni mfano Bora katika jamii.
Mbali na nafasi kubwa aliyonayo, Jenerali Mabeyo pia amekuwa akishiriki katika harambee mbalimbali kama ujenzi wa vituo vya watoto yatima, shule,mahospitali n.k
Pia Jenerali Mabeyo ameandika vitabu vingi ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimekuwa na mchango mkubwa katika kuielimisha na kuibadilisha jamii katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na jamii bora zenye misingi imara kifikra,kimaadili na kiuchumi kwa maslahi mapana ya taifa letu kiujumla.
Binafsi kinachonifurahisha zaidi ni kwamba amekuwa akifanya na kushiriki haya yote nje ya camera! Wala hakufanya kama wafanyavyo wanasiasa wengine kwa lengo la kujipatia umaarufu.Hakika unyenyekevu huu ni wa kipekee sana.
Kwa kiongozi wa aina hii, Sina shaka kabisa kwamba hata ndani ya jeshi la ulinzi hakika kutakuwa na mabadiliko mengi chanya na yenye tija kwa taifa.
Nimalizie kwa kumsihi na kumtia moyo Jenerali huyu, kwamba watanzania tunaona na kufurahishwa na kazi zako na tunazidi kukuombea Afya njema na maisha marefu ili uzidi kutoa mchango kwa taifa hili.