Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama mwandishi wa habari na nguli katika tasnia hii, ningekupongeza sana kwa makala kama ungeandika kipindi uchafu unatokea na si kupongeza sasa wakati mamia na maelfu ya watu wameumia
View attachment 1802098
Hili jambo, tumelipigia Sana kelele, tumepandisha ma thread na mathreads, makala na makala hatimaye Leo kimefanyika kitu.View attachment 1825109
Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...
Wanabodi, kama kawaida yangu, kila nipatapo nafasi, huwa nawaletea zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huandikwa kwa swali, na kukuachia wewe msomaji uhuru wa kuchangia na kutoa jibu lolote. Makala hizi zitakuwa zinatoka kwenye Gazeti la Nipashe, kila siku za Jumapili. Makala...www.jamiiforums.com
Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
Wanabodi, Kila siku za Jumapili, huwa ninaandika makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", makala ya wiki hii ni kuhusu hoja ya "Haki sio hisani, ni stahiki". Japo hakuna binaadamu yoyote anayefurahi kifo cha mtu yoyote, kifo chochote kinapotokea, kinahesabika ni mpango wa Mungu, na kama kawaida watu...www.jamiiforums.com
View attachment 1825142Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
Wanabodi, Jumatatu ya leo, naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinachapishwa kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili, makala ya leo ni swali la ushauri wa Bure kwa DPP, kwa vile Rais Samia, ameishaonyesha nia njema ya kutaka Watanzania watendewe haki, Jee...www.jamiiforums.com
View attachment 1825139
View attachment 1825143
wa kilichofanyika leo, Ile Nolle ya Mbowe, hongera Sana DPP, utabarikiwa, aliyekutuma atabarikiwa, Tanzania tutabarikiwa. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana na haki ikaonekana imetendeka.
Mungu ibariki Tanzania,
Pasco
Hili jambo, tumelipigia Sana kelele, tumepandisha ma thread na mathreads, makala na makala hatimaye Leo kimefanyika kitu.View attachment 1825109
Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...
Wanabodi, kama kawaida yangu, kila nipatapo nafasi, huwa nawaletea zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huandikwa kwa swali, na kukuachia wewe msomaji uhuru wa kuchangia na kutoa jibu lolote. Makala hizi zitakuwa zinatoka kwenye Gazeti la Nipashe, kila siku za Jumapili. Makala...www.jamiiforums.com
Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
Wanabodi, Kila siku za Jumapili, huwa ninaandika makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", makala ya wiki hii ni kuhusu hoja ya "Haki sio hisani, ni stahiki". Japo hakuna binaadamu yoyote anayefurahi kifo cha mtu yoyote, kifo chochote kinapotokea, kinahesabika ni mpango wa Mungu, na kama kawaida watu...www.jamiiforums.com
View attachment 1825142Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
Wanabodi, Jumatatu ya leo, naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinachapishwa kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili, makala ya leo ni swali la ushauri wa Bure kwa DPP, kwa vile Rais Samia, ameishaonyesha nia njema ya kutaka Watanzania watendewe haki, Jee...www.jamiiforums.com
View attachment 1825139
View attachment 1825143
Mamlaka hayo ya mtu kutoulizwa kitu, bado yako kwa DPP, katika uendeshaji wa kesi zote za jinai, ni DPP ndio huanzisha mashitaka. DPP ana mamlaka ya kuingilia kesi yoyote ikiwa hatua yoyote kabla ya hukumu, kuibadili, kuifuta, kupunguza washitakiwa na hata kuifuta kesi kwa Nolle, na DPP hapaswi kutoa sababu yoyote wala kuulizwa na yoyote hata rais wa JMT hana mamlaka ya kuulizwa chochote kwa DPP!. Mtu mwingine mwenye mamlaka ambayo
Sote tumemsikia rais Samia alichosema kuhusu kuhusu ofisi ya DPP na kilio cha haki. Rais Samia ameonyesha nia ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki kwa kauli na matendo, ikiwemo kumuondoa DPP aliyekuwepo na kumteua DPP mpya ili tuanze upya. Jee DPP mpya ataweza kuanza upya kutenda haki, huku amezongwa na lundo la uchafu wa uvundo mkali uliotokana na machozi, jasho na damu, au aanze kwanza na usafi wa kusafisha uozo aliokuta?, au kwa vile DPP hatakiwi kuingiliwa hivyo tumuache tuu?. Ns mwisho jee kumshauri DPP kama nifanyavyo kwenye makala hiyo, ni kumuingilia?
Wasalaam
Jumapili Njema.
Rejea za Mwandishi Kuhusu DPP.
1. https://www.jamiiforums.com/threads/kagoda-kamwe-haitafikishwa-mahakamani.169015/
2. Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.
3. Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o!
4. Wito kwa DPP: Japo ni Ushauri wa Rais kuwasamehe, Tafadhali tumia Nolle kufuta kesi zao, Makubaliano yawe siri ili wapokelewe na Jamii kama Watu Wema
5. DPP atumie madaraka yake kisheria ipasavyo, asisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi
6. Utabiri wa Good News kwa CHADEMA: DPP Ataifuta Kwa Nolle, Ile Kesi ya Ugaidi ya Lwakatare!
7. DPP wa Tanzania: Ni Kihiyo wa Sheria, Msanii au Mbabaishaji?
8. Baada ya kukamilika siku 14 za msamaha kwa wahujumu, Je Rais Magufuli atumie busara za Harun El Rashid kuwasamehe ambao hawakuandika barua? Au...!.
Paskali.
Watu wanasubirì hadi madudu yafukunyuliwe ndipo waseme!, sisi tulioyaona yakifanyika, tulipigia kelele na haikusaidia kitu!, sijui kama hiyo barua itasaidia kitu maana post aliyopo sasa has a security of tenure, anaweza kuteuliwa tuu, hawezi kutenguliwa!, na post iliyotangulia ya DPP ina kinga ya kutohojiwa na yeyote au kushitakiwa!.Hii ndio Taarifa mpya ya leo ya Gazeti la Raia Mwema , Kwamba kutokana na kuvuja kwa Taarifa nyingi kuhusu unyama uliotendwa kwenye kilichoitwa Plea Bargain , iliyosimamiwa kikamilifu na DPP wa wakati ule aliyeitwa Biswalo Mganga Wadau wamemkumbusha Mh Rais kuhusu Makando kando ya Mtu huyo na kumuomba Amng'oe haraka.
Ngoja tusubiri majibu ya barua hiyo .
Chanzo : Raia Mwema
TOKA MAKTABA :
6 February 2020
Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli, rais wa TLS atoa nondo kali:
Mfumo wa sheria za jinai ulioko sasa nchini Tanzania , hauna tofauti na sheria za kikoloni, zilizotumika kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji.
Kauli hiyo imetolewa na Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo tarehe 6 Februari 2020, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.
Dk. Rugemeleza Nshala ameishauri serikali ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya sheria katika mfumo Haki Jinai, ili kuondoa sheria kandamizi zinazonyima watuhumiwa dhamana.
18 September 2021
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu .Rais mstaafu TLS - Mfumo wa Haki Jinai Tanzania uundwe upya, haki ipatikane
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu . Azungumzia mazito kuhusu Nolle prosequi / kufutiwa...www.jamiiforums.com
Azungumzia mazito kuhusu
- Nolle prosequi / kufutiwa mashtaka bila kuelezwa sababu za msingi zaidi ya ofisi ya DPP kusema imeamua kutoendelea na mashtaka
- Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP
- Makubaliano kati ya raia na kitu kinachotisha kikubwa yaani raia asiishitaki serikali akiachiwa pia asidai fidia
- Marekebisho ya sheria yanahitajika ili mahakama iweze kusikiliza haki ya dhamana na ikiwa inafaa mahakama ipewe mamlaka ya kumuachia mtuhumiwa wakati Polisi na waendesha mashtaka wakiwa wanaendelea kusaka ushahidi
- Watuhumiwa wengi wanaozea ndani ya mahabusu gerezani kwa muda mrefu wakati inadaiwa vyombo vinaendelea na upelelezi
- Mtuhumiwa siyo mhalifu mpaka hapo atakapo pata haki yake kwa kuhukumiwa na Mahakama.
- Hii ya mtuhumiwa kuhukumiwa na Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka au kiongozi yeyote ni uvunjifu wa haki za raia na katiba.
- Wenye jukumu la kurekebisha mfumo huu Jinai Haki, ni serikali iliyopo madarakani kwa kutumia wataalamu wake na bahati kuna wasomi bobezi waliopo ofisini , ni kama Mwanasheria Mkuu Jaji Dr. Feleshi, Waziri wa Sheria Prof. Palamagamba na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Wadau wengine kama TLS, Kituo cha Haki za Binadamu, Vyombo vya Habari na wananchi ni kupaza sauti na kupigia kelele mfumo huu mbovu wa Haki Jinai uliopo sasa hivi.
- Polisi hawawezi kulaumiwa, wao Polisi hawana jukumu lolote bali kupiga saluti na kutekeleza amri na sheria hii mbovu inayoendesha Mfumo Haki Jamii ( Criminal Justice System) kama wanavyoelekezwa na viongozi wanaowaongoza jeshini na wanasiasa serikalini.
- Watanzania tuamke toka dhamira zetu zilizo mfu, tupiganie haki hii wote kabisa bila kujali vyeo vyetu, vyama vya kisiasa, itikadi n.k
Rugemeleza Nshala, holds Doctor of Juridical Studies (S.J.D) from the Ivy league Harvard Law School. He holds a Bachelors of Laws Degree (LL.B) from the University of Dar es Salaam, Tanzania (his home country), which he obtained in 1993; the Masters of Laws Degree (LL.M) from Harvard Law School and Masters of Environmental Management (MEM) from Yale School of Forestry and Environmental Studies that he obtained in 1997 and 2007, respectively. Source : Harvard African Development Conference
Haki Jinai / Criminal Justice System
SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI
Imewekwa: Wednesday 15, June 2022
SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI
View attachment 2471512
Serikali imejipanga kuboresha Mfumo wa Haki Jinai nchini kwa kubaini changamoto na kupendekeza maboresho katika mnyororo mzima wa haki jinai. Hayo yamebainishwa katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wadau wa Haki jinai nchini. Kikao kazi hicho cha siku tano kimefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu leo tarehe 13 Juni, 2022 Jijini Dodoma.
Dkt. Kazungu amewataka Wadau wa haki jinai kujadili changamoto zinazoukabili mnyororo mzima wa haki jinai na kupendekeza namna bora ya kuboresha mfumo huo ili kujenga mfumo madhubuti wa sheria unaoaminika na jamii katika utoaji haki.
Maoni yatakayotolewa katika kikao kazi hiki yatatumika kuboresha Andiko la Mapendekezo ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai Nchini kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi 2026/27.
Aidha, Dkt. Kazungu amesema mabadiliko ya mfumo wa haki jinai yamekuja wakati muafaka kwani hayo yamekuwa moja ya maono ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tangu alipoteuliwa kuongoza Wizara hiyo
Source : https://www.sheria.go.tz/news/serikali-yajipanga-kuboresha-mfumo-wa-haki-jinai