Pongezi kwa Mkenya aliyemwandikia Raila hotuba hii

Mkuu Iconoclastes unajitahidi sana kutumia kiswahili kama cha kibongo. Nahisi unaishi au uliishi mazingira ambayo wanazungumza kiswahili kwa kiasi kikubwa kuliko maeneo mengi ya Kenya.
 
Mkuu Iconoclastes unajitahidi sana kutumia kiswahili kama cha kibongo. Nahisi unaishi au uliishi mazingira ambayo wanazungumza kiswahili kwa kiasi kikubwa kuliko maeneo mengi ya Kenya.
Nashukuru.

La hasha. Mimi ninajitahidi tu kuandika Kiswahili katika uhalisia wake.
 
Wakenya wengi tu wana uwezo wa kuandika kiswahili aina hicho, mimi nikiwemo mmoja wa magwiji wa lugha hili huku Kibera.
Lakini waulize waKenya wengi wakwambie rangi ya blue inaitwaaje kwa kiswahili nakwambia 80% - 90% hawawezi toa jibu sahihi.
 
Lakini waulize waKenya wengi wakwambie rangi ya blue inaitwaaje kwa kiswahili nakwambia 80% - 90% hawawezi toa jibu sahihi.

Kweli kabisa.

Wakenya wengi hata hutaja majina ya wanyama kwa kingereza hata wanapozungumza kwa kiswahili, hasa vijana.
Mf: lion badala ya simba, elephant badala ya ndovu, python badala ya chatu ama rhino badala ya kifaru.

Sasa hebu muulize mkenya akutajie crocodile, cheetah, leopard, antelope, wildbeests, ostritch wanaitwaje kwa Kiswahili.....

Nimetoka sasa hivi kuwauliza baadhi yao humu 'nyumbu' ni kitu gani, wote wamebaki wameduwaa tu.

Wengi wetu kama ulivosema hapo pia hatujui majina ya mengi ya marangi, tumebaki kutohoa tu majina ya rangi na vitu vingine kama wanyama kutoka kingereza ama hata kutoka kwa vilugha vyetu wakati mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…