Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Sawa gyule, nami nakupongeza kwa kumpongeza Chacha
 
Aaamina, uko sahihi kabisa. Nadhani imetosha kama elimu nimetoa, wa kuelewa haya wa kutoelewa, Mungu ni mwema ataelewa wakati ukifika. Ngoja sasa nikapike kaugali na kisamvu changu natwanga mwenyewe😘🇹🇿
 

Nianze kwa kukushukuru mheshimiwa kwa kuchukua wakati wako kuijibu post yangu ambayo niliandika kwa nia njema.

Hii si post yangu ya kwanza kuhusiana na niyaonayo kupelekeshwa kisiasa huku maisha ya watu yakipotea bure.

Kwamba kuna sheria nzuri au mbovu zinazopelekea kupoteza maisha ya watu ambayo yangeweza kuepukika?

Kulikuwa na huu uzi humu:

Serikali ina wajibu wa kuzuia matangazo ya kibiashara ya kidini/imani kwenye vyombo vya habari kulinda raia wake

Na hii hapa ilikuwa post yangu kwenye uzi huo:



Sheria nzuri au mbaya isiyotusaidia ni ya nini?

Tunakupongeza sana tu kwenye mengi mazuri unayofanya kwenye wizara hii. Laiti kungekuwa na wizara mahsusi kwa ajili ya haki, hakika ungetufaa mno huko.

Ila hii ya kuachia miti shamba, maombezi, nk kwa sababu yoyote huku watu wakiangamia; kwenye karne hii, uhalali wake uko wapi?

Misahafu inasema: "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."

Hii ndiyo ilikuwa hoja yangu pekee ya dhati hapa.
 
Hongera sana mheshimiwa waziri kwa hili jambo la kumuokoa huyo binti!

Nafikiri kuna haja kubwa sana ya kutoa elimu endelevu kwa jamii kuhusu haya mambo ya haki na ulinzi wa watoto hasa kupitia vyombo vya habari (radio, television) ili ujumbe na elimu iwafikie walioko vijijini.
 
Kwanza ahsante Sana kwa kupokea chanya, haya ndiyo majadiliano yenye afya kwa ajili ya kujenga na siyo kubomoa. Uzuri mimi huwa pia Niko positive tu na napenda watu critical lakini critical chanya ya hoja. Kwanza ilikuwa vema tu ijulikane kuwa, tiba asili hiyo ya kujifukiza haikuwa ajenda yangu binafsi kwamba niliichukua bidhaa hizo private Bali ijulikane ni Mali ya baraza letu la tiba asili na ndiyo maana siku ile kulikuwa na mkurugenzi mwenyewe mtaalamu wa tiba asili pale ambaye naye ni Daktari pia na maafisa wengine. Wanatakiwa siku moja nao watoe elimu kuhusu utekelezaji huu wa kisheria.

Kuhusu Hawa waombeaji matapeli, mbona hata mimi nimeshiriki kwenye hatua za kufikia wengi tu leseni zao kufutwa ? Ila tu labda mambo mengi siweki online au watanzania ni wasahaulifu. La yule anajiita mungu kule Kanda ya ziwa nimeshiriki, la huyu kiboko ya washirikina, nimeshiriki, mambo ni mengi, vigumu kuanzisha. Sasa ukipata muda uka share moja tu watu baadhi wanadhani ni hilo hilo tu 🥲

Hawa wabeba nyoka nao mbona nimepambana nao tu.

Anyway, Raha ya uongozi ni ufanye kwa dhati halafu ulaumiwe ilimradi tu, moyo wako ushuhudie vinginevyo na kuungoja wakati useme.
 
Hili tukio limetengenezwa!
Mkuu wa wilaya ya Nzega alikuwa wapi wakati bus linapita nzega?
RC Tabora ofisi yake iko tabora mjini au ipo nzega?
Je Kuna umbali Gani tangu tabora mjini hadi Nzega?
 
Hili tukio limetengenezwa!
Mkuu wa wilaya ya Nzega alikuwa wapi wakati bus linapita nzega?
RC Tabora ofisi yake iko tabora mjini au ipo nzega?
Je Kuna umbali Gani tangu tabora mjini hadi Nzega?
Swali zuri. Mkuu wa Mkoa alikuwa ziara nzega, Mimi nilikuwa Dar, mtoa taarifa alikuwa kwenye gari. Bahati nzuri simu nilikuwa nayo mkononi najibu sms za watanzania. Kwa ngazi yangu mimi ilikuwa nianze na mkuu wa mkoa kwanza na ningemkosa ningeshuka wilayani Hadi kwa OCD ningefika. Ningekosa hata mtendaji wa Kijiji ningefika.

Kuna swali lingine?

Ila je na la morogoro juzi kuhusu msichana kusafirishwa kwenye happy nation bus akiwa amefungwa kamba ambalo alitoa taarifa Maria Sarungi huko x nikalipokea nikapiga mkoa wa Dodoma na Morogoro wapige stop gari hilo na Binti akabainiwa na kupelekwa hospitali, hili nalo alitengeneza nani?
 
Kwanini hakushirikisha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Nzega?

Je likitokea tukio kama hilo lotasubiri mkuu wa mkoa wakati mkuu wa wilaya Yuko eneo la tukio?

Kwahiyo unataka kuniambia RC alifanya kazi hiyo na OCD wa Nzega au na RPC wa nzega?

Nikikuambia kuwa DC Nzega ni Ke ,na RC hamtaki kwa sababu Fulani utakataa?
 
Shikamoo Mama yetu mpendwa sana. Mimi binafsi nakupongeza sana kwa kazi nzuri unazofanya. Ili tuweze kuendeleza kazi hii nzuri naomba namba yako.
 
Ni sawa na mimi uniletee changamoto hapa ya kijamii nikuambie kuwa, kwa nini huko uliko hujashirikisha mtendaji wako wa serikali za mtaa wako wakati hilo jambo ni la dharura na mimi nipo hapo kwenye access yako. Mfano mtoa taarifa ningemwambia wewe mtafute waziri wa mambo ya Ndani mwenye trafiki kisha mtafute wa Tamisemi mwenye wakuu wa mikoa halafu mtafute na wa uchukuzi? Hapo ndiyo tunaokoa mtoto na dharura zake?

Nimesema, nilipopokea hilo jambo, nilimtafuta kwanza mkuu wa mkoa, ningemkosa ningeshuka chini kwa mkuu wa wilaya. Bahati nzuri mkuu wa mkoa alikuwa ziara nzega, na si ajabu walikuwa wote na mkuu wake wa wilaya, ndiyo wakaenda hapo.

Ni sawa na kuuliza mfano ningemtafuta mkuu wa wilaya Bahatu nzuri nikampata, si ungejiuliza mbona hakuanza na mkuu wa mkoa?

Unaweza kuteremsha mguu ngazi ya nne chini kabla ya walau kukanyaga ya tatu? Uongozi ni itifaki na pia kuna mazingira ya dharura ambapo itifaki hukaa pembeni kwanza kutegemeana na scene. Sawa au kuna swali bado ndugu yangu🇹🇿
 
Ni sawa na mimi uniletee changamoto hapa ya kijamii nikuambie kuwa, kwa nini huko uliko hujashirikisha mtendaji wako wa serikali za mtaa wako wakati hilo jambo ni la dharura na mimi nipo hapo kwenye access yako.

Nimesema, nilipopokea hilo jambo, nilimtafuta kwanza mkuu wa mkoa, ningemkosa ningeshuka chini kwa mkuu wa wilaya. Bahati nzuri mkuu wa mkoa alikuwa ziara nzega, na si ajabu walikuwa wote na mkuu wake wa wilaya, ndiyo wakaenda hapo.

Kwa upande mwingine pia, ni sawa na kuuliza mfano ningemtafuta mkuu wa wilaya Bahati nzuri nikampata, si ungejiuliza mbona hakuanza na mkuu wa mkoa?

Hivi unaweza kuteremsha mguu ngazi ya nne chini kabla ya walau kukanyaga ya tatu? Uongozi ni itifaki na pia kuna mazingira ya dharura ambapo itifaki hukaa pembeni kwanza kitegemeana na scene. Husika.
 
Kwa wanao mfahamu Paul chacha ni mchapakazi ,msikivu,mnyenyekevu,muungwana Sana, anasaidia ame saidia watu wengi Sana anao wajua na asio wajua pia hongeraaaa sanaa kwako muheshimiwa wazir gwajima.
 
Shikamoo Mama yetu mpendwa sana. Mimi binafsi nakupongeza sana kwa kazi nzuri unazofanya. Ili tuweze kuendeleza kazi hii nzuri naomba namba yako.

Ahsante Sana kwa ushirikiano wako. Namba zangu huwa ziko hewani miaka yote nazo ni 0765345777 na copy 0734124191. Andika ujumbe usipige nitapiga mwenye ikibidi.

Za kituo cha wizara nazo zipo nitakutumia bango ukinitumia sms. Shukrani 🙏🏽
 
Nimeguswa na utendaji wako Shem Mhe. Dr. Doro. Hongera sana kwa jinsi unavyojitoa kuwahudumia Watanzania. Ni Mungu tuu atakulipia. Ubarikiwe sana. Salaam kwa Kaka.
P
 
Maswali mengine siwezi kuyajibu ila nitajibu yangu haya kuwa namba zangu mimi kunitumia ujumbe ni 0734124191 na 0765345777. Halafu sifanyi kazi za maonesho kwa kuwa kutangaza namba zangu kwa umma nilianza tangu mwaka 2003 nikiwa intern bungando hospitali mwanza na nimeendelea hivyo hatua zote za utumishi wangu Hadi nitakapostaafu. Sema sikuwaga online humu.

Mwenyewe nabarikiwa kuMoyo😘

Una swali jipya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…