Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Pengine hii ni child/ human trafficking.

Hilo basi lishikwe. Dereva na konda ilibidi wawe wa kwanza kurespond
 
Ubarikiwe sana kiongozi. Tupo pamoja katika ujenzi wa taifa.
 
😅Hujambo? Heri ya siku ya leo huko uliko
Sijambo kabisa Mheshimiwa na shikamoo sanaa.sisi huku ni kwema kabisa. Naomba mwakani uchukue Fomu ya Ubunge .tutapiga kampeni sana kwa ajili yako Mheshimiwa. Wewe ni Mfano wa kuigwa sana. Unawakosha sana watanzania bila kujali vyama vyao.
 
Nakushauri tu Kwa utendaji wako wa kazi usije kuthubutu kujidhalilisha kama JENISTA
 
Sijambo, hofu kwako mh.

Hii ni sawa na kuwasha chainsaw ukaukata mgomba kisha unataka usifiwe.

Sote hiyo hatari tumeiona, hakukuwa na haja ya kuja hapa kupongezaaana, ungekaa kimya ingekuwa hajafanya kazi? Ama wewe ungekuwa hujafanya kazi, una mazuri mangapi hujawahi jitangaza, je hili ndio la kwanza ama kubwa zaidi?
Hapa kilichofanyika ni tangazo la kwamba kazi inafanyika.

Kwenye mfano wako wa dk 85, mtu afunge goli 2, inategemea na situation kama mlikuwa mnaongoza 7, hizi mbili hazina maana, kama mlikuwa mnaongozwa au bila bila, hizi 2 ukifunga utapongezwa mnooo, sababu itakuwa jambo la maana saaana umefanya,
Sasa nataka kukuuliza mh. Je, huyo mkuu wa mkoa hili ndio la maana sana kuwahi kufanya kiasi jambo kama hili mumpe pongezi utafikiri kaliokoa taifa kwenye midomo ya madhalimu.

Ushawahi kuona mume anapewa pongezi kwa kumtia mimba mkewe? Kama ambavyo mwanamke anavyopewa pongezi baada ya kujifungua? 😂

Mimi sijambo, we haujambo huko uliko?
 
Nakushauri tu Kwa utendaji wako wa kazi usije kuthubutu kujidhalilisha kama JENISTA
Bora umsihi mapema, hawachelewi kujitoa ufahamu ili yao yawaendee.. Mwishowe tunakuwa taifa la hovyo kabisa, taifa la kujipemdekeza ili upate nafasi, watu hawatizami utendaji wako ni unajipemdekeza kiasi gani kwa mkubwa wa cheo.
 
Kazi nzuri, je una mkakati gani juu ya vijana ambao whereabouts zao hazijulikani yapata siku 40 sasa?

Hapa namzungumzia Soka, Chaula na wengineo wengi.

Huoni nao kutoonekana kwao imeacha majonzi na sintofahamu kwa familia zao ?
 
Apongezaye hutia moyo na kuhamasisha na kutangaza jambo ambapo, watu wengi huja pia kuangalia kulikoni🥹🥹🥹 nao hupata na taarifa kuwa jamani kaeni chonjo kuna haya nayo. Hivyo, pongezi Zina faida Sana kimtazamo ilimradi tu ziwe za haki. Naendelea kuwapongeza na kukupongeza na wewe uliyetembelea mjadala. Naomba waambie wa kwenye mtaa wako kuwa, wawe makini na usafirishaji haramu wa watoto na pia wawe macho safarini kuna mengi
 
Dr Gwqjima anafanya kazi nzuri sana. Ni miongoni mwa mawaziri ambao wanatoa majibu kwa wakati.

Hongera sana mama
Yuko kama Jerry Silaa! Mungu azidi kuwalinda na husuda za wanadamu,maana ukisimamia haki nchi hii unakua na maadui wengi wasiopenda haki itendeke!!
 
Mheshimiwa Dr Dorothy Gwajima, ninaomba tujadili masuala yafuatayo kuhusu mikopo inayotolewa na halmashauri nchini

1. Uratibu wa Mikopo:
Je, wizara yako inahusika katika uratibu wa mikopo hii? Kuna mchakato wowote ambao wizara inashiriki katika kuhakikisha mikopo hii inawafikia watu walio kusudiwa?

2. Mikopo kwa Walemavu:
Ikiwa walemavu watapewa mikopo na kisha kushindwa kuirejesha, ni hatua gani zitachukuliwa dhidi yao? Je, kuna mpango wowote wa kuwasaidia ili waweze kurejesha mikopo hiyo?

3. Chanzo cha Mikopo:
Mikopo hii ni ya halmashauri pekee au inahusisha fedha kutoka kwa Rais Samia? Kuna tofauti yoyote katika vigezo vya mikopo hii kulingana na chanzo chake?

4. Uhusiano wa Kisiasa:
Je, kuna uhusiano wowote kati ya mikopo hii na siasa? Walemavu na vijana wa vyama vya upinzani wanaweza kunufaika na mikopo hii? Ni vigezo gani vinatumika katika kutoa mikopo hii?

5. Madiwani wa Viti Maalum: Madiwani wa viti maalum wanapata faida gani kutokana na mikopo hii? Je, ni wajibu wao kuhamasisha au ni wanufaika?

6. Mbinu za Wizara:
Ikiwa wizara yako inahusika, ni mbinu gani zitakazotumika kuwafikia na kuwajua walemavu wa vijijini ili waweze kunufaika na mikopo hii? Je, kuna mipango maalum ya usajili ambayo itatekelezwa?

7.Je, kuna mipango ya kutoa mafunzo kwa walemavu kuhusu jinsi ya kutumia mikopo hiyo?

8.Wizara ina mpango gani wa kufuatilia matumizi ya mikopo na matokeo yake?

9.Ni vigezo gani vinatumika katika tathmini ya athari za mikopo?

10.Je, walemavu wanaweza kupata mikopo ya bajaji ambayo sasa imekuwa kama kausha damu kwa vijana na walemavu? Hii inaonyesha kwamba mikopo hii inatoa msaada mkubwa kwa kundi hili, ikiwasaidia kujipatia kipato na kuboresha maisha yao. Bajaji zimekuwa na umuhimu mkubwa katika jamii, na kutoa mikopo kwa walemavu ni hatua ya kuunga mkono juhudi zao za kujitegemea na kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Maswali haya yanahusisha masuala muhimu yanayohusiana na mikopo na jinsi inavyoweza kuwafaidi walemavu na jamii kwa ujumla.

Ningependa kupata ufafanuzi kuhusu jinsi wizara inavyopanga kutekeleza mipango hii na kuhakikisha kwamba rasilimali zinawafikia wahusika.
 
Sasa ndg yangu issue ikisha fika kwa RC,hiyo automatically ishaingia chini ya Wizara ya mambo ya ndani, maana pale kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa yupo pia RPC!!
 
Hujambo? Ahsante kwa swali zuri. Naomba tuandae vema wasilisho eneo hili tutakuwa na thread yake maalumu tafadhali nakuahidi. Shukrani
 
Upya wake nini?

Huyo binti alikuwa anapelekwa wapi kama siyo utumwani?
Hapo bado haijajulikana bibi. Subiri kwanza vyombo vya ulinzi vikamilishe upelelezi. Walimwengu wana mambo mengi sana.
 
Sasa ndg yangu issue ikisha fika kwa RC,hiyo automatically ishaingia chini ya Wizara ya mambo ya ndani, maana pale kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa yupo pia RPC!!
Tatizo lilolopo na ambalo ninahitaji kutatuliwa na kulifuta, ni RC na DC kuwa wajumbe wa kamati za siasa za chama mkoa na wilaya!

Ikitokea chama cha upinzani kimechukua mkoa mzima na halmashauri zote za huo mkoa RC na maDc Huwa wanapoteza uelekeo kiutendaji.
 
Sasa ndg yangu issue ikisha fika kwa RC,hiyo automatically ishaingia chini ya Wizara ya mambo ya ndani, maana pale kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa yupo pia RPC!!
Hakika, mkuu wa mkoa ma wilaya wanazo sekta zote chini yao tofauti na wizara zilivyo. Hivyo, madaraka yalipogatuliwa kwenda chini karibu na wananchi yalienda na nguvu kubwa chini yao. Hili nalo somo la mjadala siku ingine kuhusu DxD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…