Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Hongera sana Mheshimiwa.huna makuu wala baya na mtu.wewe ni kazi tu. Kagombee ubunge Mwakani tuje kukupigia kampeni bure kabisa .
Shida yako wewe ni uchawa na kulamba viatu. Toa hoja yenye kujenga badala ya kuwa 🥾👅 bootlicker muda wote. TAIFA letu linachelewa kupiga hatua Kwa sababu ya kuendekeza uchawa badala ya weledi
 
Pongezi ziwafikie raia mwema (jina kapuni) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Timu yake ya Usalama kwa ushirikiano wao jana 5 Oktoba, 2024 ambapo, Saa 9.56 jioni nilipokea ujumbe wa simu kutoka kwa raia mwema mzalendo (jina kapuni) kuwa kwenye gari la abiria (bus) linalojulikana kama Kisbo lenye namba za usajili T408EFH lililokuwa linatokea Kahama kuelekea Dar es Salaam kulikuwa na abiria binti mdogo aliyekuwa akilia na kuhangaika kwamba ateremshwe maana hajui anakoenda na amepakiwa tu kwenye gari na mtu ambaye hakusafiri naye.

Mara baada ya kupokea taarifa hizi, niliwasiliana na Mheshimiwa Paul Chacha, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili afahamu na kuchukua hatua zake ambapo, mara moja alichukua hatua za kuwaelekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua na kufikia majira ya saa 10.30 jioni bus hilo likiwa ndiyo linaingia stendi ya Nzega lilisimamishwa na kukaguliwa na Askari wakiwa na Mhe Mkuu wa Mkoa na binti huyo kubainiwa na mahojiano stahiki kufanyika. Pia rejea video fupi ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Tabora hapa chini.

Binti huyo sasa yuko mikono salama chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku hatua zaidi za kubaini kisa mkasa zikiendelea.

PONGEZI; narudia tena kutoa Pongezi kwa raia mwema aliyejali na kuthubutu kutoa taarifa kwa kunitumia ujumbe huo. Hakika mlinzi wa kwanza wa jamii ni jamii yenyewe. Pongezi ziende kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa wepesi wake kwenye kuitikia taarifa niliyompa na kuchukua hatua mara moja. Pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kwa kutekeleza jukumu lao kikamilifu na kumuokoa binti huyu mdogo na kwa hatua wanazoendelea nazo.

WITO KWA JAMII; tuendelee kushirikiana kwenye kubaini na kutoa taarifa za matukio ambayo hayaeleweki na yanaleta maswali kwenye maisha ya jamii kila siku kwani, ni kwa jamii kuwa macho na kutoa ushirikiano ndiyo tunaweza kuwadhibiti wafanya uovu kwa watoto wetu kabla ya kutimiza nia zao ovu.

WITO KWA WAHUDUMU WA USAFIRI; kuwa makini na abiria hususan watoto wadogo wanaopakizwa kwa maelekezo kuwa huko waendako watapokelewa na mtu fulani kwani, tunaishi kwenye nyakati ambazo watoto ni wahanga wakubwa wa ukatili mbalimbali ikiwemo kutoroshwa na kwenda kutumikishwa kinyume na umri wao.

Jumapili njema kwenu wote🇹🇿

View attachment 3116555
Pamoja na kwenda shule,
Pamoja na kuwa na cheo kikubwa,
Pamoja na kuwa mtu "mkubwa"
Haujausahau wito wako wa "umama"
Hongera sana Dk. Gwajima G.
Hii ndiyo Tanzania tuitakayo!
 
Siyo takataka, wananchi wengi sana hawajui itifaki za kiutumishi so Waziri amefanya sawa kumpa elimu kiduchu 😂😂😂
 
Attachments

  • IMG-20240924-WA0033.jpg
    IMG-20240924-WA0033.jpg
    101.2 KB · Views: 1
Chacha tunampongeza kivipi? Yaani anapongezwa mtu kwa kutimiza wajibu wake, tena kwa issue kama hiyo ambayo ilitakiwa imalizwe na trafiki tu
Kwamba alitoka Tabora kwenda Nzega(km 120) kwa ajili hiyo au issue ilimkuta akiwa Nzega?
Acha kujiaibisha
 
Issue ndogo saana hiyo, ilifaa kumalizwa na trafiki huko barabarani... Mnakaa mnasifiaaana, mnapeana pongezi, utafikiri labda mmezuia kitu gani labda.
Hujambo? Sasa kama haikumalizwa huko iliko na ikafika kwa mwingine, naye asiimalize? Na kama katika kumaliza huko umetumika utaratibu ambao ni WA kujiongeza, watu wasipewe maua yao? Maana kuna hard infrastructure na kuna soft infrastructure. Kuwepo kwa miundo mbinu migumu bila laini kufanya kazi siku zote ni mtihani..... Wanastahili PONGEZI maana wangeweza pia kuamua liende kwenye huo utaratibu mwingine ingekuwa dakika tu chache mtoto ashushwe mahali ambapo, mimi na wewe tusingejua mengi. Naendelea kuwapongeza mimi ambaye niliiona hiyo hatari.....

Ukipiga mpira dakika za majeruhi mfano dakika ya 85 ukafunga mawili ya haraka haraka hupongezi?

Hujambo lakini huko uliko 🥹🇹🇿
 
Trafiki wawajibishwe.....pia dereva na konda wawajibishwe bila kusahau kisbo company...

Hao wote walikuwa kwenye mfereji wa hyo biashara haramu.

Yaani fimbo ya mbali ije iue nyoka wakati fimbo za karibu zipo....wachukuliwe hatua hao iwe fundisho
 
Pongezi ziwafikie raia mwema (jina kapuni) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Timu yake ya Usalama kwa ushirikiano wao jana 5 Oktoba, 2024 ambapo, Saa 9.56 jioni nilipokea ujumbe wa simu kutoka kwa raia mwema mzalendo (jina kapuni) kuwa kwenye gari la abiria (bus) linalojulikana kama Kisbo lenye namba za usajili T408EFH lililokuwa linatokea Kahama kuelekea Dar es Salaam kulikuwa na abiria binti mdogo aliyekuwa akilia na kuhangaika kwamba ateremshwe maana hajui anakoenda na amepakiwa tu kwenye gari na mtu ambaye hakusafiri naye.

Mara baada ya kupokea taarifa hizi, niliwasiliana na Mheshimiwa Paul Chacha, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili afahamu na kuchukua hatua zake ambapo, mara moja alichukua hatua za kuwaelekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua na kufikia majira ya saa 10.30 jioni bus hilo likiwa ndiyo linaingia stendi ya Nzega lilisimamishwa na kukaguliwa na Askari wakiwa na Mhe Mkuu wa Mkoa na binti huyo kubainiwa na mahojiano stahiki kufanyika. Pia rejea video fupi ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Tabora hapa chini.

Binti huyo sasa yuko mikono salama chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku hatua zaidi za kubaini kisa mkasa zikiendelea.

PONGEZI; narudia tena kutoa Pongezi kwa raia mwema aliyejali na kuthubutu kutoa taarifa kwa kunitumia ujumbe huo. Hakika mlinzi wa kwanza wa jamii ni jamii yenyewe. Pongezi ziende kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa wepesi wake kwenye kuitikia taarifa niliyompa na kuchukua hatua mara moja. Pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kwa kutekeleza jukumu lao kikamilifu na kumuokoa binti huyu mdogo na kwa hatua wanazoendelea nazo.

WITO KWA JAMII; tuendelee kushirikiana kwenye kubaini na kutoa taarifa za matukio ambayo hayaeleweki na yanaleta maswali kwenye maisha ya jamii kila siku kwani, ni kwa jamii kuwa macho na kutoa ushirikiano ndiyo tunaweza kuwadhibiti wafanya uovu kwa watoto wetu kabla ya kutimiza nia zao ovu.

WITO KWA WAHUDUMU WA USAFIRI; kuwa makini na abiria hususan watoto wadogo wanaopakizwa kwa maelekezo kuwa huko waendako watapokelewa na mtu fulani kwani, tunaishi kwenye nyakati ambazo watoto ni wahanga wakubwa wa ukatili mbalimbali ikiwemo kutoroshwa na kwenda kutumikishwa kinyume na umri wao.

Jumapili njema kwenu wote[emoji1241]

View attachment 3116555
Asante sana Muheshimiwa ubarikiwe sana kwa kazi nzuri kwa watanzania wenzako,Mungu akutangulie kwa kila jambo, na Mkuu wa Mkoa Tabora namuamini sana na namkubali,yuko very active kwenye kuhudumia watanzania, safi sana nae Mungu amtangulie kwa kila jambo!![emoji1431]
 
namba alipata wapi uyo mwamba.
 
Chacha tunampongeza kivipi? Yaani anapongezwa mtu kwa kutimiza wajibu wake, tena kwa issue kama hiyo ambayo ilitakiwa imalizwe na trafiki tu
Kwamba alitoka Tabora kwenda Nzega(km 120) kwa ajili hiyo au issue ilimkuta akiwa Nzega?
Achaa kina Chacha waingie site,huko chini kumeoza,bila ya wakubwa kushuka huku chini watu wengi watakua wanaumizwa sana bila kupata mtetezi!!
 
Baadhi ya watanzania wamekuwa wabaya sana.

Dr Gwajima siyo kwamba wanaenda kutumikishwa bali wanaenda kutolewa viungo for rituals. Uchaguzi umekaribia, tuwe tuwalinde watoto na ndugu zetu. Inaonekana albino si sili tena bali viungo vya binadamu wadogo ndo vinatakiwa.

Pambana mpaka kieleweke.
Hao wadogo wengine hawana unajisi wowote
Ni muhimu sana
 
Back
Top Bottom