Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Hujambo? Ahsante kwa swali zuri. Naomba tuandae vema wasilisho eneo hili tutakuwa na thread yake maalumu tafadhali nakuahidi. Shukrani
God bless you Dr D. G!
Nitakuwa Jf online 24hrs/7days nikisubiri hili jibu lako nzuri.
 
Asante Sana Dkt. Gwajima D, endelea kuchapa kazi, Wizara ya Afya wanakukumbuka Sana, hadi "incinerator" zilifanyiwa usafi, ila sasa hivi mambo yamedorora Hadi kichefuchefu!
Wachapa kazi, wafuatiliaji wanaojali raia wa kawaida kwenye nchi hii wamebaki wachache ukiwemo wewe!

Mbegu unayoipanda itaota na kustawi Sana, usikate tamaa!
 
Hili tukio limetengenezwa!
Mkuu wa wilaya ya Nzega alikuwa wapi wakati bus linapita nzega?
RC Tabora ofisi yake iko tabora mjini au ipo nzega?
Je Kuna umbali Gani tangu tabora mjini hadi Nzega?
Sasa unaleta hoja za mahakamani kwenye emergency ya kumuokoa mtoto!? Unajiona kama uko kwenye cross examining na Muheshimiwa Dr Gwajima siyo!? Tulia watu wapige kazi,kama kuna issue ya mahakamani mtakutana huko,lakini kwa sasa msitari ni mmoja tu, nao ni kumuokoa mtoto kwanza, na mengine yatafuata!!
 
Asante Sana Dkt. Gwajima D, endelea kuchapa kazi, Wizara ya Afya wanakukumbuka Sana, hadi "incinerator" zilifanyiwa usafi, ila sasa hivi mambo yamedorora Hadi kichefuchefu!
Wachapa kazi, wafuatiliaji wanaojali raia wa kawaida kwenye nchi hii wamebaki wachache ukiwemo wewe!

Mbegu unayoipanda itaota na kustawi Sana, usikate tamaa!
 

Attachments

  • VID-20241001-WA0024.mp4
    9.9 MB
Lucas wa Jf, Dr angalia asikusifie humuJf:
Atakuharibia CV mazima!
Ni ushauri tu.
 
Siyo takataka, wananchi wengi sana hawajui itifaki za kiutumishi so Waziri amefanya sawa kumpa elimu kiduchu 😂😂😂
Wanakera bwana! Wanaona kila anayeandika humu ananifurahisha na ni rika lao! Atasemaje tukio limetengenezwa hilo?
 
Dr.Gwajima hongera sana tulizitambu juhudi zako. Inshallah mungu akupe maisha marefu yenye fanaka.
 
Pongezi ziwafikie raia mwema (jina kapuni) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Timu yake ya Usalama kwa ushirikiano wao jana 5 Oktoba, 2024 ambapo, Saa 9.56 jioni nilipokea ujumbe wa simu kutoka kwa raia mwema mzalendo (jina kapuni) kuwa kwenye gari la abiria (bus) linalojulikana kama Kisbo lenye namba za usajili T408EFH lililokuwa linatokea Kahama kuelekea Dar es Salaam kulikuwa na abiria binti mdogo aliyekuwa akilia na kuhangaika kwamba ateremshwe maana hajui anakoenda na amepakiwa tu kwenye gari na mtu ambaye hakusafiri naye.

Mara baada ya kupokea taarifa hizi, niliwasiliana na Mheshimiwa Paul Chacha, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili afahamu na kuchukua hatua zake ambapo, mara moja alichukua hatua za kuwaelekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua na kufikia majira ya saa 10.30 jioni bus hilo likiwa ndiyo linaingia stendi ya Nzega lilisimamishwa na kukaguliwa na Askari wakiwa na Mhe Mkuu wa Mkoa na binti huyo kubainiwa na mahojiano stahiki kufanyika. Pia rejea video fupi ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Tabora hapa chini.

Binti huyo sasa yuko mikono salama chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku hatua zaidi za kubaini kisa mkasa zikiendelea.

PONGEZI; narudia tena kutoa Pongezi kwa raia mwema aliyejali na kuthubutu kutoa taarifa kwa kunitumia ujumbe huo. Hakika mlinzi wa kwanza wa jamii ni jamii yenyewe. Pongezi ziende kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa wepesi wake kwenye kuitikia taarifa niliyompa na kuchukua hatua mara moja. Pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kwa kutekeleza jukumu lao kikamilifu na kumuokoa binti huyu mdogo na kwa hatua wanazoendelea nazo.

WITO KWA JAMII; tuendelee kushirikiana kwenye kubaini na kutoa taarifa za matukio ambayo hayaeleweki na yanaleta maswali kwenye maisha ya jamii kila siku kwani, ni kwa jamii kuwa macho na kutoa ushirikiano ndiyo tunaweza kuwadhibiti wafanya uovu kwa watoto wetu kabla ya kutimiza nia zao ovu.

WITO KWA WAHUDUMU WA USAFIRI; kuwa makini na abiria hususan watoto wadogo wanaopakizwa kwa maelekezo kuwa huko waendako watapokelewa na mtu fulani kwani, tunaishi kwenye nyakati ambazo watoto ni wahanga wakubwa wa ukatili mbalimbali ikiwemo kutoroshwa na kwenda kutumikishwa kinyume na umri wao.

Jumapili njema kwenu wote🇹🇿

View attachment 3116555
 

Attachments

  • 5843973-2cd4b00bedf7abcddbfd063a298341c1.mp4
    68.8 MB
Hongera mama unafanya kazi kweli, hakuna cha zaidi ya uhai na usalama wa wananchi unaowaongoza mungu akusaidie kila ufanyalo tuwalinde watoto.
 
Hapa nikisema unaupiga mwingi hata Mungu wangu hawezi kunipa dhambi.. Ila kuna viongozi wengine kusema wanaupiga mwingi ni DHAMBI kubwa kwa Mungu.
Hongera sana Mama Gwaji
 
Huyu mama angebaki tu kwenye nafasi ile ya waziri wa Afya, nadhani mazuri zaidi yangelikuwepo katika wizara hiyo. Hongera sana mama Gwajima kwa kazi nzuri.
 
Dr D G. Yuko vizuri.
PhD Holder,sio zile zingine PhD njugu.
CCM iwe makini ituletee hili.jembe!
 
Kuna haja ya kuwauliza vizuri wazazi wake. Inawezekana kabisa kuwa wao ndio waliosababisha kila kitu. Wakimrudisha binti kwao wanaweza kujaribu kumuuza tena maana watakuwa bado wana deni. Na kuna jamii zetu ambazo zinaona mtoto wa miaka 13 kama mtu mzima.

Amandla...
 
Safi sana Dkt. Gwajima D kwa kuchukua hatua kwa uharaka ,hakika unaitendea haki JF na unastahili tuzo nyingine mwaka mwingine.

Hao Mawakala inatakiwa washitakiwe kwa kesi kama ya Pdiddy Human Trafficking na wazazi wa hao walioruhusu mtoto mdogo wa 13yrs akafanya kazi za ndani nao wafungwe.

Tukitaka tukomeshe hayo matukio Tusicheke na nyani usoni , kwa kifungo cha maisha walichokula kina NYUNDO na wenzake sidhani kama kuna wanaume wanaweza kufanya ubakaji wa kikundi au wa single kwa wanawake maana washaaona impact yake.
 
Back
Top Bottom