Pongezi kwa Rais Magufuli kusitisha Bomoa Bomoa kwa kuongeza kigezo cha "Human Face". He's so Human!

Baada ya watu walio athirika na kufa kwa pressure ndo anashtuka!!! Kweli bwana mkubwa, tunae...utu umemjia baada ya kufika Mwanza?
 
mbona paskali unawaogopa sana vijana wa chadema kwani ukipongeza si ni maamuzi yako na wao wanayo yao,kwani ukipewa u-dc utaukataa mbona mangu amekubali kuwa balozi japo umri umekwenda,umeeleweka kauli ya rais ni sheria!
 
Mayala Mbona kama heshima yako uliyoijenga hapa jukwaani mda mrefu unaanza kuishusha kwa kasi sana... Hivi neno mwanza siku hizi lina wakilisha neno Nchini... acheni kutonesha vidonda Vya watu Jamani Kuna Watu mpaka Sasa wako nje na mvua za sasa zinawatesa.
 
Kwani Rais alishindwa kusema nasitisha bomoabomoa nchi nzima, kama kweli alimaanisha hivyo? Ni mbinafsi, mbaguzi, mkabila na mtu wa visasi. Amedhihirisha kuwa yeye ni anaendesha nchi kwa misingi ya ubaguzi wa kivyama, kikabila na kikanda full stop.

Umesahau na kidini pia
 
Mimi nasubiri msemaji wa serikali aje kuhalalisha maneno yako haya ....

Maana umeshamtafunia tayari.
 
Nimekuelewa sana Pascal andiko lako ni fikirishi ukilisoma juu juu unaweza usinga'mue kitu lakini pia Nikukumbushe unakumbuka ile kauli ya "fyatueni watoto nitasomesha bure" waziri alikuja kusema Rais aliongea na watani wake unakumbuka kauli ile ya hawa "Vilaza" Je unadhani Rais alimaanisha nchi nzima au ni watu wa eneo flani tu.

Kiukweli ni shida sana kumtetea kwa sababu leo atasema hili kesho atasema lile nadhani ipo haja ya kuundwa chombo au wizara maalum ya kufafanua kauli za Rais katika awamu hii.
 
Kaka Pascal Mayalla hupati shida kumtetea mtu mwenye nguvu na sauti kama Rais? Wewe tetea wasiokuwa na sauti huko chini, hawa wakubwa watajitetea wenyewe...
Hivi Pascal anapata wapi ujasiri huu..!
Nadhani/nafikiri bado ana amini kuwa, siku aliyo tolewa nishai pale IKULU, mbele ya Waandishi na Wahariri wa habari wenzie, anachukulia ulikuwa UTANI ule...!!

Huyu Mtu akiongea AMEMAANISHA.
Waulize vizuri wanao kaa nae karibu..!
 
Pascal acha kujitoa ufahamu. Alisema hawavwatu wa kigoto na sehemu nyingine jina limenitoka msiwabomoleee. Sio nchi nzima. Unataka ukuu wa wilaya na wewe.
 
Mbona haujamalizia sentensi zima kwamba "hawa walinipa uraisi" thread zako za sarakasi za uteuzi wa uDC au uRC ndo hizi aisee kama kawaida yako njaa si mchezo
 
Mkuu kwani wewe ni Msigwa hadi uwasaidie kutafsiri matamko ya Rais?
Na hili la kusema Mwanza wasibomolewe kwa vile ndio waliompa Urais has sent shock waves around the country.
Sisi wapenzi wa CCM hatutoki Mwanza.
Sasa waliobomolewa bila machungu kama Kimara, walimpinga Rais?
Na hao wa Mwanza sasa si ni kiburi juu kwa vile "wao ni wa Rais".
Viashiria ya maamuzi ya kibaguzi, kikabila , kidini au vinginevyo haviashiri umoja katikaTaifa.
 
amesema wale wa mwanza walimpigia kura, kwahivyo kwa lugha nyepesi tu ni kwamba wa kimara hawakumpigia kura ndyo maana wakabomolewa
 
Katika viumbe wasio na aibu nchi hii huyu jamaa namba moja, kauli zake anaongea Utadhani kimara haikuwa Tz, Utadhani waliobomolewa Kwingine hawakuwa watanzania,
 
Hivi Mbona Paskali anapenda sana,kumsemea rais Wetu MPENDWA? Wamesema na anamanisha kabisa,na ni kweli alichosema,au wewe ndo unamuelewa tofauti na wengine?
 
2025??? Unajielewa kweli? Kuna kutokuchaguliwa tena 2015 na pia kuna kuachia ngazi kwa kuona nchi imemshinda. Miaka hii miwili inadhibitisha hilo.
Endeleeni kuota!
Hii ngoma inatoka 2025, sijui kwa nini tuwe na uchaguzi wa urais 2020, ni kupoteza pesa tu! WATANZANIA KAMA 2015, TUTAMCHAGUA TENA JEMBE JPM, MAFISADI MA WAZEE WA KITONGA LAZIMA MUMCHUKIE.
Bavicha walivyo nyumbu humu jf wasikupofushe akili.
Bavicha wa humu ni 1/50 ya watamzania wote.
 
Huuy ni ubaguzi mtupu kwann asitishe ubomoaji sasahivu? Kwann au kwasababu kule kwao ndio waliomchagua? Je ni rais wa mwanza tu? Mbona kimara mbezi ipo karibu kabisa na ikulu lakini kabomoa? Je,ni kipi hasa kilichomsukuma na jusitisha ubaguzi huo
 
hamjamuelewa muandishi nyie mnaomponda,makala yake ni mtego mkubwa sana.someni tena alafu mtafakari na sio msome ili mjibu
Hapo ndipo kwenye shida humu jukwaani watu hawasomi kutafuta mantiki au maana nzima ya bandiko hili Pascal Mayalla katumia weledi mkubwa na nilitaraji kuna watu watashindwa kumuelewa .
Si kila mtu unaweza kumnyamazisha asiseme ,nu vigumu kumfunga mdomo mtu mjanja kama Mayalla atakusema tu kiujanja ujanja!
 
paskali huwa nakukubali uandishi wako ni wachache tunaweza kukuelewa. ila mhshimiwa kateleza aliposema "msibomolewe kwa kuwa ndo mlinipa uraisi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…