Pongezi kwa Rais Magufuli kusitisha Bomoa Bomoa kwa kuongeza kigezo cha "Human Face". He's so Human!

Human face. Mwanza tumekusikia,, tumekufikia.
Dar piga makofi ya utukufu kwa pinduapindua.
Maendeleo hayana chama
 
Kilichosemwa huko Mwanza ni indefinsible. Bomoabomoa haijanza jana huko Mwanza, kwanini jana ndio kakumbuka kuna human face. This is the definition of tribalism..... Kama anaguswa na hali za Watanzania wanaobomolewa nyumba zao aguswe kwa nchi nzima, kwanini Mwanza wanapewa preferential treatment. Mpaka viongozi wanaagizwa kutafuta namna ya kuwa-accomodate watu.

This is shameful
 
Kuna haja ya kumsamehe Pascal Mayala. tofauti yake na Jerry Muro ni sifuri. simply Njaa ni mbaya sana.

Pascal tofauti yake ni kuwa yeye ni Msukuma .. na katika pita pita .. wasukuma wachache sana wana neno na mkulu. Kuna kaji affinity fulani. Labda hii ni kwa makabila yote yaani .... mtu kwao ...
 
Mayalla ni Ng'wana wa nyumbani itakuwa kamwelewa kutokana na ujuzi wa lugha ileeeeeeeeee ila kwani kubomoleshwa ndo nini Na kama kubomoleshwa kupo je kupo kisheria au ni matakwa ya huyu Mayalla wa ikhulu?
 
Pongezi kwa kudhihirisha ukabila na ukanda kwa vitendo
 
Human face with demonic possessed heart????
 
msome vizuri Pascal bwana kilokiki utamuelewa!
Pascal anatafuta ugomvi kihekima ,pascal pascal utapimwa kimiminika chako!
Hahahahaha! Tatizo baadhi ya member humu wanachangia kwa mihemuko bila kufikirisha kichwa,ila ukituliza kichwa vzuri utamuelewa paskali kama ulivyomuelewa wewe na Mimi.Alichokifanya paskali ni kung'ata na kupuliza.Ameogopa kung'ata moja kwa moja asije pimwa kimiminika.
 
Labda niseme hivi, kama kweli mheshimiwa Rais wangu ametamka hayo maneno najua itakuwa ni kwa nia njema ila bado haijakaa vizuri kwa yeye kulitamka akiwa Mwanza nyumbani kwao na ikiwa sasa hivi kuna bomoabomoa maeneo mbalimbali ya nchi. Naamini wapiga kura wake hawaishii mwanza tu maana yeye ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Sijui kwa nini huyu mzee anashindwa kutafuta kauli fulani ambazo zitamtoa kwenye kuonekana negative. Ni lini atafikia kutoa speech ambayo haitwabakiza watanzania kwenye mshangao??? Naamini nia yake ni njema lakini kauli zake mara zote zimekuwa na ukakasi sana Rais wangu tunakuomba basi usiwe unatuacha kwenye njia panda namna hii.
 
Mkuu we mwenyewe najua huwwzi kuelewa ulichoandika

Mkuu huyo jamaa anamapungufu mno
Kwenye ukweli usemwe tu
Mada zako kama hizi zinakupunguzia heshima
Mkuu afadhali umetangulia kumjibu huyu Pascali kwa sababu hizi njaa zinawaondolea watu heshima zao.Sasa huyu kwa maneno yake ya kizungu anataka kubadilisha kauli ya rais iwe anavyotaka yeye!
Halafu hata kama ni hivyo!alikuwaga wapi sikuzote watu wakibomolewa na kuachwa wakimbizi ktk nchi yao?Au tuseme badao anajaribu kila kitu kama alivyojaribu kuomba urais akasokomezewa!
Tumshauri tu Pascal na wale wengine wenye tabia kama yake kuwa huu unafiki hautawafikisha popote kwani nafsi zao zitaendelea kuwasuta usiku na mchana!
 
Alikuwepo wapi wakati watu wa dar es salaam wanabomolewa nyumba zao na serikali hiyo hiyo ikazarau amri ya mahakama hapa ni ticket ya ukabila tu ndiyo iliyotumika tukitaka tuctake.
 
Kwa jinsi unavotumia njia hii kuhadithia ndo mana sizonje anakuweka poozz hakuteuwi mpaka ujirekebishe
 

Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi mzuri, ila kutokana na hali ilivyo, raisi wetu ni makabila full...! Ni watu wangapi wamelala nje na watoto wamekosa kwenda shule kisa hawana makazi, na aliona na kusikia maumivu waliyopata. Mh raisi wangu ni mkabila, na Mungu amhurumie tu na huu ukabila wake.

Paskal, mcheza kwao hutuzwa kaka. Tunachofanyia affirmation, hasa mimi ni kuona matunda ya huu ukabila unaopandwa ndani ya nchi yangu. Wewe ni muumini mzuri wa sheria ya karma, niliijua hii sheria kupitia wewe. So tuache muda ufike utaamua kwamba apandacho mtu ndicho atakachovuna bro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…