Wanabodi,
Hili ni bandiko la matumizi ya kauli kuumba jambo jema kwa kutumia kitu kinachoitwa affirmation kwa kutumia the power of speech kuumba mema ya kila kinachozungumzwa na rais, hata kiwe kibaya vipi, unatumia nguvu ya kauli, kwa kuindia wema kupitia kanuni ya affirmations kutumia affirmatives kupongeza kauli ya rais Magufuli kusimamisha bomoa bomoa ya nchi mzima, kabla bomoa bomoa yoyote haijatekelezwa, upembuzi yakinifu kwa kutumia kigezo kipya kiitwacho a human face, lazima kitumike kwanza, ili zile nyumba zitakazo bomolewa ni zile tuu ambazo zina ulazima wa kubomolewa. (Hata kama rais alidhamiria ni Mwanza tuu, affirmations na affirmatives, zinaigeuza kauli hii kuwa ni nchi nzima, kauli huumba!)
Jee ni Kweli Kauli Huumba?.
Wajameni ni kweli kabisa, kauli huumba, ukitoa kauli mbaya au ukitamka jambo mbaya, kauli ile inakuwa imeliumba hilo jambo baya na kweli linatokea, ukitoa kauli njema, au ukitamka jambo jema, then kauli hiyo, inaliumba jambo jema, hivyo jambo jema kutokea, hivyo kauli hii ya rais Magufuli kusitisha bomoa bomoa na badala yake kutumia human face, ni jambo jema, tuiumbie wema, itelelezwe kwa Tanzania nzima.
Jee Kauli Hii ni Kwa Mwanza Tuu au Nchi Mzima.
Japo kauli hii ameitolea Mwanza ambako ni Usukumani, na yeye kujinasibu ni Msukuma na kusemekana ni Msukuma, hivyo kauli hiyo kuchukuliwa au kutafsiriwa wrongly kuwa rais Magufuli ni mkabila na mbaguzi kwa kuzuia bomoa bomoa kwa kabila lake tuu, mimi napongeza uamuzi huu kwa hoja kuwa kauli hiyo ni applicable national wide and not necessarily Mwanza tuu, hivyo kwa kauli hiyo, rais Magufuli atakuwa amesitisha bomoa bomoa zote nchi nzima, hivyo naomba wasaidizi wake wa jitokezeni, mlifafanue hili ili rais watu aeleweke asitafsiriwe vibaya huku nyinyi mpo.
Jee Rais Anaweza Kulazimishwa Kufanya Jambo Lolote?
Kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977, rais ndiye mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, japo anakuwa na washauri, lakini katiba imempa rais mamlaka mamlaka ya kufikia maamuzi yoyote yeye mwenyewe, kwa kufanya jinsi ile anaona inafaa, bila kufuata ushauri wa mtu yoyote, lakini kuna maeneo Fulani Fulani, rais analazimika kufuata maelekezo ya katiba, sharia, taratibu na kanuni, na kuna maeneo rais analazikika kuchukua maamuzi Fulani kutokana na trends za public opinions, hivyo kwa kutumia kanuni inayoitwa assertiveness, kwa kutumia kitu kinachoitwa precedence, tunaweza kabisa kumlazimisha rais, kutumia precedence ya kanuni hiyo ya human face katika bomoa bomoa nyingine zote zilizobakia, kwa hoja kuwa kama human face imeweza kutumika Mwanza, kwa nini isitumike maeneo mengine yote ya Tanzania nzima
Justification ya Pongezi.
Naendelea kusisitiza kuwa kila jambo zuri linalofanywa na rais wetu, la kustahili pongezi, apongezwe, na kila baya, alaumiwe, akosolewe au arekebishwe, hili la kuzuia bomoa bomoa kwa kutumia kigezo kipya cha human face, kinastahili pongezi kwa sababu kinafanywa ina good faith, kwa nia njema ya kuwasaidia wananchi wake wasidhurike na bomoa bomoa.
Declaration of interest.
Kumezuka mtindo humu jf, mtu akipongeza jambo lolote zuri linalofanywa na rais Magufuli anaambiwa anatafuta U-DC, naomba kushikilia msimamo wangu wa kuunga mkono katiba ya Warioba katika hili la ma DC kuwa ni posts za kikoloni tuu ambazo kwa sasa ni redundant ambazo ni only wastage of money and resources, saves for, kutumika ku maintain status quo ya serikali iliyopo madarakani kama mkoloni alivyowatumia ku maintain his status quo.
Kauli za Rais Zisitafsiriwe Literally Bali The Motive Behind.
Sio kila rais anachosema kutafsiriwe direct or literally bali baadhi ya kauli hizo, ziangaliwe kwa dhana ya rais alidhamiria kusema nini na sio kuangalia tuu rais ametamka nini, sometimes ni tatizo la matamshi, sometimes ni kuteleza tuu ulimi kama ile ya Saa hivyo kuangalia kauli hizi zimedhamiria nini. Mfano aliposema wasibomolewe kwa sababu wamenipa urais, hapa naamini ni kuteleza tuu ulimi, rais akiishatangazwa kuwa ndie ameshinda uchaguzi, then anakuwa amechaguliwa na wote waliomchagua, wote wasio mchagua, wote kura zao zilizoharibika, hata wale ambao hawakupiga kura, hivyo ni rais wa wote, ndie rais wa CCM, ndie rais wa Chadema, ndie rais wa CUF, ndie rais wa Watanzania wote, waliomchagua na wasiomchagua, hivyo huu upendeleo wa wazi wa kabila lake, au waliomchagua, au chuki ya wazi kwa kabila Fulani, ni human weaknesses, human mistakes. tutumie affirmatives kulirekebisha hili, Magufuli nae ni binadamu tuu kama sisi na sio malaika, hivyo kuteleza ulimi, sio jambo la ajabu!.
Hitimisho.
Watanzania wazalendo wenzangu, tuungane name katika matumizi ya kauli kuumba jambo jema kwa kutumia kitu kinachoitwa affirmation kwa kutumia the power of speech kuumba mema ya kila kinachozungumzwa na rais wetu, hata kiwe kibaya vipi, tutumie nguvu ya kaul zetu kuzigeuza kuwa jambo jema kupitia kanuni ya affirmations kutumia affirmatives , hivyo kujenga Tanzania njema
Paskali