KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,456
- 5,462
Paskali, I know you know what you have written. It is in a satirical way. You have to read between the lines to understand him.msome vizuri Pascal bwana kilokiki utamuelewa!
Pascal anatafuta ugomvi kihekima ,pascal pascal utapimwa kimiminika chako!
completely i agree with u!Paskali, I know you know what you have written. It is in a satirical way. You have to read between the lines to understand him.
Mkuu Kilokiti, Msimamo wa Pascal Mayala ni tofauti na anavyouleta ujumbe wake. Irudie mara mbili hiyo thread yake utaelewa ninachokisemaMkuu we mwenyewe najua huwwzi kuelewa ulichoandika
Mkuu huyo jamaa anamapungufu mno
Kwenye ukweli usemwe tu
Mada zako kama hizi zinakupunguzia heshima
Moja ya mambo ninayojivunia ni kuifahamu vema lugha ya Kiswahili kwa sababu, hii ndio lugha yangu ya kwanza! Katika kumsikiliza Mheshimiwa rai, sina japo chembe shaka ikiwa kweli nimemuelewa pale aliposemaJee Kauli Hii ni Kwa Mwanza Tuu au Nchi Mzima.
Japo kauli hii ameitolea Mwanza ambako ni Usukumani, na yeye kujinasibu ni Msukuma na kusemekana ni Msukuma, hivyo kauli hiyo kuchukuliwa au kutafsiriwa wrongly kuwa rais Magufuli ni mkabila na mbaguzi kwa kuzuia bomoa bomoa kwa kabila lake tuu, mimi napongeza uamuzi huu kwa hoja kuwa kauli hiyo ni applicable national wide and not necessarily Mwanza tuu, hivyo kwa kauli hiyo, rais Magufuli atakuwa amesitisha bomoa bomoa zote nchi nzima, hivyo naomba wasaidizi wake wa jitokezeni, mlifafanue hili ili rais watu aeleweke asitafsiriwe vibaya huku nyinyi mpo.
Kweli hii ni Human Face manake kwa mara ya kwanza namsikia JPM huku pia akionesha (from facial expression) ni namna gani yupo concerned na watu waliojenga pahala ambapo mamlaka zingine zinasema hao wamevamia!!Na moja nafikiri linahusu wananchi waliojenga eneo la Kigoto. Wengine wana miaka karibu 30. Nasikia wanaambiwa wamevamia eneo la Jeshi la Polisi na wanatakiwa waondoke. Na eneo lingine ni la Muhoze, ambako wamevamia eneo la uwanja wa ndege pamoja na eneo la jeshi. Sasa kwa sababu hili nimeliona leo, na mimi natakiwa nilifanyie uchambuzi... vizuri, ili nipate maelezo ya kutosha; niwaombe, viongozi wa mkoa wa Mwanza. Niwaombe, viongozi wa uwanja wa ndege. Niwaombe, viongozi wengine wa maeneo hayo ambayo yamevamiwa, wasubiri kwanza wasiwabomoleshe hawa watu mpaka nitakapotoa maamuzi mengine.
Ninaambiwa kule Muhoze kuna nyumba zaidi ya nyumba 2000. Naambiwa Kigoto, nyumba napo zipo nyingi. Tumewatazama watu wakajenga. Wakaweka investment yao. Sasa leo tukiwafukuza... tusubiri kwanza. Kwa sababu ardhi zote za nchi hii, kwa mujibu wa Sheria Namba 4 ya mwaka '99 na kwa mujibu wa Sheria ya Vijiji Na. 5 ya mwaka '99, na kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji na Matumizi Bora ya Ardhi ya mwaka 2007, ardhi zote msimamizi wake ni rais. Na mimi hawa hawa wa Kihoto, na wa wapi... Muze, ndio walinipa urais. Inawezekana walifanya makosa lakini kwa sababu serikali yangu ina huruma, ndio maana nasema wazi ndugu zangu, musiwabomoleshe.
Huwezikuficha ukweli kuwa rais ni mkabila na wewe unamuunga mkono sababu unatokeo huko kambashite na polepole. Kimara imebomolewa kwa vile wengi ni wachaga. Ushamba utawamaliza na kuwaumbuaWanabodi,
Hili ni bandiko la matumizi ya kauli kuumba jambo jema kwa kutumia kitu kinachoitwa affirmation kwa kutumia the power of speech kuumba mema ya kila kinachozungumzwa na rais, hata kiwe kibaya vipi, unatumia nguvu ya kauli, kwa kuindia wema kupitia kanuni ya affirmations kutumia affirmatives kupongeza kauli ya rais Magufuli kusimamisha bomoa bomoa ya nchi mzima, kabla bomoa bomoa yoyote haijatekelezwa, upembuzi yakinifu kwa kutumia kigezo kipya kiitwacho a human face, lazima kitumike kwanza, ili zile nyumba zitakazo bomolewa ni zile tuu ambazo zina ulazima wa kubomolewa. (Hata kama rais alidhamiria ni Mwanza tuu, affirmations na affirmatives, zinaigeuza kauli hii kuwa ni nchi nzima, kauli huumba!)
Jee ni Kweli Kauli Huumba?.
Wajameni ni kweli kabisa, kauli huumba, ukitoa kauli mbaya au ukitamka jambo mbaya, kauli ile inakuwa imeliumba hilo jambo baya na kweli linatokea, ukitoa kauli njema, au ukitamka jambo jema, then kauli hiyo, inaliumba jambo jema, hivyo jambo jema kutokea, hivyo kauli hii ya rais Magufuli kusitisha bomoa bomoa na badala yake kutumia human face, ni jambo jema, tuiumbie wema, itelelezwe kwa Tanzania nzima.
Jee Kauli Hii ni Kwa Mwanza Tuu au Nchi Mzima.
Japo kauli hii ameitolea Mwanza ambako ni Usukumani, na yeye kujinasibu ni Msukuma na kusemekana ni Msukuma, hivyo kauli hiyo kuchukuliwa au kutafsiriwa wrongly kuwa rais Magufuli ni mkabila na mbaguzi kwa kuzuia bomoa bomoa kwa kabila lake tuu, mimi napongeza uamuzi huu kwa hoja kuwa kauli hiyo ni applicable national wide and not necessarily Mwanza tuu, hivyo kwa kauli hiyo, rais Magufuli atakuwa amesitisha bomoa bomoa zote nchi nzima, hivyo naomba wasaidizi wake wa jitokezeni, mlifafanue hili ili rais watu aeleweke asitafsiriwe vibaya huku nyinyi mpo.
Jee Rais Anaweza Kulazimishwa Kufanya Jambo Lolote?
Kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977, rais ndiye mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, japo anakuwa na washauri, lakini katiba imempa rais mamlaka mamlaka ya kufikia maamuzi yoyote yeye mwenyewe, kwa kufanya jinsi ile anaona inafaa, bila kufuata ushauri wa mtu yoyote, lakini kuna maeneo Fulani Fulani, rais analazimika kufuata maelekezo ya katiba, sharia, taratibu na kanuni, na kuna maeneo rais analazikika kuchukua maamuzi Fulani kutokana na trends za public opinions, hivyo kwa kutumia kanuni inayoitwa assertiveness, kwa kutumia kitu kinachoitwa precedence, tunaweza kabisa kumlazimisha rais, kutumia precedence ya kanuni hiyo ya human face katika bomoa bomoa nyingine zote zilizobakia, kwa hoja kuwa kama human face imeweza kutumika Mwanza, kwa nini isitumike maeneo mengine yote ya Tanzania nzima
Justification ya Pongezi.
Naendelea kusisitiza kuwa kila jambo zuri linalofanywa na rais wetu, la kustahili pongezi, apongezwe, na kila baya, alaumiwe, akosolewe au arekebishwe, hili la kuzuia bomoa bomoa kwa kutumia kigezo kipya cha human face, kinastahili pongezi kwa sababu kinafanywa ina good faith, kwa nia njema ya kuwasaidia wananchi wake wasidhurike na bomoa bomoa.
Declaration of interest.
Kumezuka mtindo humu jf, mtu akipongeza jambo lolote zuri linalofanywa na rais Magufuli anaambiwa anatafuta U-DC, naomba kushikilia msimamo wangu wa kuunga mkono katiba ya Warioba katika hili la ma DC kuwa ni posts za kikoloni tuu ambazo kwa sasa ni redundant ambazo ni only wastage of money and resources, saves for, kutumika ku maintain status quo ya serikali iliyopo madarakani kama mkoloni alivyowatumia ku maintain his status quo.
Kauli za Rais Zisitafsiriwe Literally Bali The Motive Behind.
Sio kila rais anachosema kutafsiriwe direct or literally bali baadhi ya kauli hizo, ziangaliwe kwa dhana ya rais alidhamiria kusema nini na sio kuangalia tuu rais ametamka nini, sometimes ni tatizo la matamshi, sometimes ni kuteleza tuu ulimi kama ile ya Saa hivyo kuangalia kauli hizi zimedhamiria nini. Mfano aliposema wasibomolewe kwa sababu wamenipa urais, hapa naamini ni kuteleza tuu ulimi, rais akiishatangazwa kuwa ndie ameshinda uchaguzi, then anakuwa amechaguliwa na wote waliomchagua, wote wasio mchagua, wote kura zao zilizoharibika, hata wale ambao hawakupiga kura, hivyo ni rais wa wote, ndie rais wa CCM, ndie rais wa Chadema, ndie rais wa CUF, ndie rais wa Watanzania wote, waliomchagua na wasiomchagua, hivyo huu upendeleo wa wazi wa kabila lake, au waliomchagua, au chuki ya wazi kwa kabila Fulani, ni human weaknesses, human mistakes. tutumie affirmatives kulirekebisha hili, Magufuli nae ni binadamu tuu kama sisi na sio malaika, hivyo kuteleza ulimi, sio jambo la ajabu!.
Hitimisho.
Watanzania wazalendo wenzangu, tuungane name katika matumizi ya kauli kuumba jambo jema kwa kutumia kitu kinachoitwa affirmation kwa kutumia the power of speech kuumba mema ya kila kinachozungumzwa na rais wetu, hata kiwe kibaya vipi, tutumie nguvu ya kaul zetu kuzigeuza kuwa jambo jema kupitia kanuni ya affirmations kutumia affirmatives , hivyo kujenga Tanzania njema
Paskali
Pascal tofauti yake ni kuwa yeye ni Msukuma .. na katika pita pita .. wasukuma wachache sana wana neno na mkulu. Kuna kaji affinity fulani. Labda hii ni kwa makabila yote yaani .... mtu kwao ...
wengi wamefeli kabisa kumsoma Paskali Mayalla.Mkuu Kilokiti, Msimamo wa Pascal Mayala ni tofauti na anavyouleta ujumbe wake. Irudie mara mbili hiyo thread yake utaelewa ninachokisema
ungetafakari kidogontubungejua kuwa paskali na wewe mumeandika sawa ila wewe umeshutumu paskali mayala kabeza(na atapimwa mkojo wakimng'amua)Moja ya mambo ninayojivunia ni kuifahamu vema lugha ya Kiswahili kwa sababu, hii ndio lugha yangu ya kwanza! Katika kumsikiliza Mheshimiwa rai, sina japo chembe shaka ikiwa kweli nimemuelewa pale aliposema Kweli hii ni Human Face manake kwa mara ya kwanza namsikia JPM huku pia akionesha (from facial expression) ni namna gani yupo concerned na watu waliojenga pahala ambapo mamlaka zingine zinasema hao wamevamia!!
Hii ni Human Face manake, mimi binafsi, hii ni mara ya kwanza kumsikia JPM akitishika na idadi kubwa ya nyumba zilizo kwenye hatari ya kubomolewa!!
Hii ni absolute Human Face manake, mimi binafsi, hii ni mara yangu ya kwanza kumsikia JPM akiueleza umma ni namna gani wahusika wapo kwenye eneo husika kwa miaka kadhaa!!!
NI Human Face manake pia, angalau kwa upande wangu, hii ni mara yangu ya kwanza kumsikia JPM akiwa pamoja na wananchi linapokuja suala la ujengaji holela na kupeleka lawama kwa vyombo vya serikali kwa kuwaacha watu wakijenga na kuwakekeza kwenye maeneo husika!
Hakika hii ni Human Face manake kwa mara ya kwanza, mimi binafsi namsikia JPM akijitishwa zigo yeye mwenyewe kwamba lazima akafanye uchambuzi wa kutosha kwanza ili hatimae ajiridhishe ikiwa hao wamevamia (au ikiwa hamna namna ya kuwanusuru?)!!!
Hii ni total Human Face manake, mimi binafsi, ndo namsikia JPM kwa mara ya kwanza akitaja mlolongo wa sheria si kwa sababu ya kuhalalisha serikali na taasisi zake zifanye kazi zake bila kusumbuliwa bali ili kuonesha ni namna gani yeye kama Rais alivyo na mamlaka juu ya ardhi ya Tanzania kiasi kwamba, ana uwezo wa hata kubadili matumizi ya ardhi husika!!
Hii ni complete Human Face, manake JPM yule yule ambae bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno, aliwahi kuwaambia waathirika wa tetemeko la ardhi kwamba tetemeko halikuletwa na serikali lakini leo anaonekana wazi yupo very concerned na wananchi ambao, mamlaka halali zinasema wahusika wamevamia maeneo!!!
Ndugu yangu Pascal Mayalla, unabadilisha vipi kauli kama hizo ili hatimae ziwe ni kauli za kuvutia na kutoa faraja kwa Watanzania wote hasa ukizingatia historia ya JPM ambae alitishia kubomoa hadi jengo la TANESCO pale Ubungo?!
Bora basi mtu aandike 1+1=II na hapo tutasema labda amezoea namba za Kirumi na kwahiyo amepatia kwamba ni mbili lakini mtu bila kuogopa anaandika 1+1=11 ili eti tuseme amemaanisha moja jumlisha moja ni sawa sawa na moja moja ambayo ni mbili?! How?!
Itoshe tu kusema kwamba, sidhani ikiwa kauli ile ya JPM ina-qualify kuwa Presidential Decree inaypaswa kufuatwa nchi mzima! The decree was very locational specific.
Rais akisema ".....waacheni Wamachinga waendelee kufanya biashara zao Kariakoo" hilo haiwezi kuwa ni agizo kwa niaba ya Wamachinga wote wa Tanzania mzima kwa sababu, rais tayari ameshataja ni Wamachinga wa wapi wanaotakiwa kuachwa!!!
Mmachinga wa Tandika kama amechoka kusumbuliwa sumbuliwa pale Tandika, anaweza kufungasha virago na kwenda Kariakoo kwa sababu agizo la rais limetoa ruhusa ya wao kujinafasi Kariakoo!!