Pongezi kwa Rais Magufuli kusitisha Bomoa Bomoa kwa kuongeza kigezo cha "Human Face". He's so Human!

Pascal unakumbuka alivyoingia alichowafanya wamachinga wa dar? But when the same force was applied kwa wamachinga wa mwanza akasema wamachinga waachwe wasisumbuliwe. Kwanini tamko la huruma mara zote linatoka wanapoguswa wasukuma? Same tu bashite na kalimani
 
Eti human face ! Kuna double standard nyingi nchi hii. Wakati watu wengine wengi hawana makazi,hawajui waelekee wapi alafu unafika sehemu moja bila aibu unasema eti ni human face tena anakwenda mbali anasema human face inatoka CCM kanakwamba waliovuja nyumba katika maeneo mengine ni watu wabaya au wapinzani wake.
Rais Kama taasisi anapaswa kushauriwa kabla au baada ya mambo fulni hayaja fanyika kwa kupima impact yake.Iwezekani watendaji na wasaidizi wake wa Mwanza wawe na makosa kwa kile alichodai " wakati watu wanajenga seriali ilikuwa wapi?" Lakini swali hilo haliulizwi kwa watendaji ktk sehemu nyingine za nchi ambapo bomoa bomoa zilitokea au zinakoendelea.

Ninachoona ni Rais anacheza na akiri za wanyonge wa nchii kwa kile ninachoweza kusema ni kupoza machungu na malalamiko ya wananchi.
 
Ukiwa mwanasiasa ili ukiki ujulikane...unamwambia wa chini yako atengeneze tatzo..alafu wewe unakuja unalitatua unalipga marufuku...aisee utakiki miaka buku
 
Hii njemba siku za karibuni imeweka juhudi kubwa za kutafuta teuzi kwa nguvu zote kwa kumsifia uchwara pamoja na kuwa hastahili sifa yoyote. Bila shaka njaa inazidi kuwa kali na hakuna dalili ya ahueni ya kutibu njaa yake.

Inasaidia nini wakati mpaka sasa kuna watu hawana makazi tena licha ya mhakama kuzuia inamaana kauli ya raisi ina maana na nguvu kuliko mahakama?
Mkuu we mwenyewe najua huwwzi kuelewa ulichoandika

Mkuu huyo jamaa anamapungufu mno
Kwenye ukweli usemwe tu
Mada zako kama hizi zinakupunguzia heshima
 
Paskali, Raisi Magufuli anatawala au anaongoza binadamu,binadamu ana roho,na matendo ya binadamu ndio yanampa mtendaji utu au vinginevyo.
Kauli yoyote ya Raisi inapewa uzito mkubwa sana.
Hivi Paskali ungekuwa umebomolewa nyumba yako Kimara harafu unasikia Mkuu wa nchi akisema Mwanza wasibughudhiwe waangaliwe kwa jicho la huruma,kwa sababu walinipigia kura?
Yapo mambo mengi mazuri anayofanya raisi wetu,lakini kwa hili ametugawa na kusambaratisha mshikamano wa kitaifa.
Zipo kumbukumbu za Human face hizi:
Kurasini/Shimo la Udongo miaka ya 80 Mwalimu Nyerere aliwalipa na kuwapa viwanja vingine wajenge na wakapewa muda wa kutosha kuhama,walikuja wadaku wakasema Mwl mbona wanaishi kinyume cha sheria na wapo waliolipwa enzi za mkoloni?Nyerere alijibu Mswahili hajui sheria.
 
DC Arumeru
 
Yaleyale huyu lazima atakuwa anatoka kanda ya ziwa, kwa mafuta aliyopaka asubiri uteuzi
 
Roho wa ubaguzi si roho wa Mungu, ni roho wa shetani!
Mwalimu aliwahi kusema ukishatenda dhambi ya ubaguzi huwezi kuacha ni sawa na kula nyuma ya mtu!
 
Tatizo kalisababisha mwenyewe

Halafu anakuja kutaka kulitatua mwenyewe

Chama cha mizimu na ulozi
 
Wakati bomoa bomoa imekithiri nchi nzima !! Wajane wameachwa hawana pa kuishi na yote yalikua yafanywa na media wanaonyesha live alikaa kimya!! Leo Mwanza anakataza !! Lo!!! Inasikitisha
 
Paskali na wewe mbona huwa hueleweki mbona hiviiiiiiiiiii
Tupongeze kauli ipi?
Amedhihirisha yeye ndio alitoa amri nyumba za Kimara zibomolewe vile ni jimbo la upinzani au tumueleweje?
Leo tumpongeze kwa kauli mbofumbofu za Mwanza? Are you being serious?
Huyu mtu analigawa taifa kwa maneno matendo mawazo kipi usichokiona hapa Paskali!
 
Ndo lengo lako! Kila kitu unajipendekeza! Bro, kiufupi mi huwa sikufagiliii kabisa! Nitakufagilia pale tu kuna siku utaacha kutaja jina LA JPM kwenye thread zako! UDC hupati, na kujipendekeza kote huko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…