Pongezi kwa Rais Samia na Dr Hussein Mwinyi Kuifanya Tanzania Bara na visiwani kuwa Salama na Tulivu na kutujengea Matumaini


Sina shaka na wizi wa kura uliofanyika. Kwa taarifa yako hata wakoloni walijenga reli na tuliona ni zetu. Wewe na chawa wenzako ndio unaona mnashirikishwa, na sio kila mtu.
 

Unadhani hayo mauaji na kuacha wetu na vilema vya maisha ni jambo la siri? Umeona wakifidia mauji na ukatali wa kwenye uchaguzi ule?
 
M
Umekuwa chawa kuliko ata wale waliokutangulia
Mambo yanayofanywa na viongozi wetu Hawa Ni makubwa Sana na hauwezi kuyamaliza kuyaelezea hapa, kwa kuwa kila eneo linalo mgusa mwananchi limefanikiwa kuguswa na viongozi wetu hawa
 
Sina shaka na wizi wa kura uliofanyika. Kwa taarifa yako hata wakoloni walijenga reli na tuliona ni zetu. Wewe na chawa wenzako ndio unaona mnashirikishwa, na sio kila mtu.
Ndio wakoloni walijenga miundombinu Kama shule,reli, barabara na hata ofisi nzuri lakini tukadai Uhuru wetu na kuwafukuza, hii Ni kwa kuwa tulihitaji kuwa huru na kujiamulia Mambo yetu wenyewe na kujipangia mipango yetu,

Kwa Sasa hayo yote yanafanywa kwa kiwango kikubwa na kwa Kasi kubwa huku sisi wananchi tukishiriki katika ujenzi wa Taifa letu, miradi yote inayojengwa lazima watanzania utawakuta wakishiriki, ajira zinaendelea kutolewa kupitia miradi hiyo bila ubaguzi,

yoyote pia anaweza kuwa kiongozi au kuchaguliwa kuwa kiongozi bila ubaguzi Wala kubaguliwa, kinachoangaliwa Ni sifa alizonazo mtu na Kama anaweza akayamudu majukumu ya kazi husika

Chini ya viongozi wetu Hawa nchi yetu Ina amani na utulivu mkubwa Sana, nchi inasonga mbele kwa Kasi, wananchi wanajiona fahari kuitwa watanzania na wanajivunia kuzaliwa Tanzania
 

Narudia tena, miradi ya wakati wa wakoloni wananchi walikuwa hawashiriki?
 
Kwani umesahau habari za utumwa? Pia Ni miradi iliyojengwa kimkakati katika kuhakikisha inamsaidia na kumnufaisha mkoloni katika kutunyonya na kujipa faida yeye

Ni miradi iliyokuwa mahususi katika kuzifyonza Rasilimali zetu kutoka mahali zilipo, ndio maana uliona Barabara zikijengwa kuelekea huko,

Hawakujenga ili sisi watanzania tunufaike nayo Bali iwanufaishe wao na mataifa yao kwa jasho letu wenyewe

Lakini Leo hii miradi inajengwa kila Kona ya nchi kwa manufaa yetu wenyewe baada ya kufanyika tathimini ya N
Mahitaji ya huduma fulani, ndio maana unaona kila eneo likijengwa Miundombinu mbalimbali bila ubaguzi

Hata hivyo sijuwi Kama unaweza ukaelewa kwa hayo machache niliyo kueleza maana mawazo na fikira zako bado zimetawaliwa na wakoloni, bado unaishi miaka ya 20 wakati sisi tupo 2022, bado kwako kumbe akili yako inapenda kutawaliwa kuliko kujitawala na kujiongoza, bado akili yako inataka ufungwa minyororo miguuni na kuchapwa mijeredi, bado kumbe akili yako inatamani ukauzwe sokoni Kama mnyama, bado unataka maisha Yale ya kikoloni ya kudhalilishwa utu wetu Kama wanyama

Kiufupi huwezi ukaturudisha huko Tena maana Babu zetu walipigana kutukomboa sisi zidi ya utumwa huo
Narudia tena, miradi ya wakati wa wakoloni wananchi walikuwa hawashiriki?
 

Hata sasa tuko chini ya wakoloni weusi, ni bora mkoloni mweupe maana alitoa elimu Bora.
 
Hata sasa tuko chini ya wakoloni weusi, ni bora mkoloni mweupe maana alitoa elimu Bora.
Basi wewe unatatizo mahali, maana Kama unatamani ukoloni katika Karne hii bila shaka unahitaji ushauri wa kisaikolojia, maana Hakuna binadamu mwenye akili ya kawaida anayeweza kutamani kuyaona Tena machungu na mateso ya ukoloni
 
Bila Shaka huna hoja ndio maana umeshindwa kuiweka hapa hoja inayopingana na niliyo yaelezea
Sasa hiyo hoja nitaitoa wapi na wakati wewe mwenyewe ulichokiandika hapo juu unakijua mwenyewe!

Unatahadharishwa kuchukua hatua ili usije kuchanganyikiwa kabisa! Unakaza fuvu!! Shauri yako mwenyewe. Wewe endelea tu kujitoa ufahamu, huku ukisifia vitu vya kijinga.
 
Mimi nimeongea na kuandika ukweli juu ya Yale wayatendayo viongozi wetu Hawa wakuu
 
Unatumia mbinu za kizamani katika utafutaji wa uteuzi na nyie ndo mkipewa nafasi mko radhi kujidharilisha ili kumlidhisha mteuzi.
 
Unatumia mbinu za kizamani katika utafutaji wa uteuzi na nyie ndo mkipewa nafasi mko radhi kujidharilisha ili kumlidhisha mteuzi.
Mimi natumia Uhuru wangu kueleza maoni yangu ya ukweli juu ya viongozi wetu Hawa waliotokea kukubalika na kuaminika na watu wengi wa vyama tofauti tofauti, ndio maana unaona kwa Sasa wakiungwa mkono kwa kiwango Cha hali ya juu
 
Tupunguze kusifia watanzania
Kiongozi anayefanya vizuri lazima apongezwe muda wote kwa kufanya vyema, hakika viongozi wetu Hawa Ni wachapa kazi na wenye dhamira ya dhati katika kutukwamua kimaisha wananchi
 

Tanzania bara ni nchi gani Na Tanzania visiwani ni nchi gani ?

Wacheni kuandika ujinga na matango pori kuwapotosha watu .Mnaona aibu gani kusema Tanganyika Na Zanzibar ?
 
Tanzania bara ni nchi gani Na Tanzania visiwani ni nchi gani ?

Wacheni kuandika ujinga na matango pori kuwapotosha watu .Mnaona aibu gani kusema Tanganyika Na Zanzibar ?
Hatuna hizo nchi kwa sasa, kwanini usijivunie kile kilichotokana na fikira zako mwenyewe, Tanzania Ni zao la fikira zetu wenyewe juu ya Taifa Tulilolitaka, Sasa wewe naona unamawazo ya enzi za ukoloni ndio yametawala fikra zako ndo maana unatamani fikra za kikoloni ziendelee kutuongozo Hadi Sasa, hiyo haiwezekani na tulishapita huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…