Pongezi kwa Rais Samia na Dr Hussein Mwinyi Kuifanya Tanzania Bara na visiwani kuwa Salama na Tulivu na kutujengea Matumaini

Pongezi kwa Rais Samia na Dr Hussein Mwinyi Kuifanya Tanzania Bara na visiwani kuwa Salama na Tulivu na kutujengea Matumaini

Umesahau kuweka picha yako ndugu..... Italeta maana zaidi....
 
Basi wewe unatatizo mahali, maana Kama unatamani ukoloni katika Karne hii bila shaka unahitaji ushauri wa kisaikolojia, maana Hakuna binadamu mwenye akili ya kawaida anayeweza kutamani kuyaona Tena machungu na mateso ya ukoloni

Nipe tofauti ya Mkoloni mweupe na huyu mkoloni mweusi, au kwakuwa ww uko kwenye mlo? Kwa taarifa yako hata wakati wa mkoloni mweupe kuna watu walikuwa kwenye mlo kama ww, na waliona mkoloni yuko sahihi.
 
Nipe tofauti ya Mkoloni mweupe na huyu mkoloni mweusi, au kwakuwa ww uko kwenye mlo? Kwa taarifa yako hata wakati wa mkoloni mweupe kuna watu walikuwa kwenye mlo kama ww, na waliona mkoloni yuko sahihi.
Unanishangaza unapohitaji ukoloni hapa nchini kwetu katika nchi iliyo huru na inayojiamulia Mambo yake, huku kila mtanzania akishiriki katika ujenzi wa Taifa letu, Sasa wewe upo unaishi katika fikira za kikoloni katika miaka hii, hivyo Ni ngumu kuelewana maana hapo Ni kichuguu na mlima, wewe Ni kichuguu na Mimi ni mlima
 
Kiongozi anayefanya vizuri lazima apongezwe muda wote kwa kufanya vyema, hakika viongozi wetu Hawa Ni wachapa kazi na wenye dhamira ya dhati katika kutukwamua kimaisha wananchi
Utahangaika sana. Lkn wenye macho hawaambiwi tazama.
 
Unanishangaza unapohitaji ukoloni hapa nchini kwetu katika nchi iliyo huru na inayojiamulia Mambo yake, huku kila mtanzania akishiriki katika ujenzi wa Taifa letu, Sasa wewe upo unaishi katika fikira za kikoloni katika miaka hii, hivyo Ni ngumu kuelewana maana hapo Ni kichuguu na mlima, wewe Ni kichuguu na Mimi ni mlima

Toka lini chawa akawa mlima?
 
Hatuna hizo nchi kwa sasa, kwanini usijivunie kile kilichotokana na fikira zako mwenyewe, Tanzania Ni zao la fikira zetu wenyewe juu ya Taifa Tulilolitaka, Sasa wewe naona unamawazo ya enzi za ukoloni ndio yametawala fikra zako ndo maana unatamani fikra za kikoloni ziendelee kutuongozo Hadi Sasa, hiyo haiwezekani na tulishapita huko
Wewe usiye na mawazo ya kikoloni niambie , mafia, ukerewe na visiwa vingine vya Tanganyika , hivyo utaviita Tanzania bara ? Au visiwani?
 
Wewe usiye na mawazo ya kikoloni niambie , mafia, ukerewe na visiwa vingine vya Tanganyika , hivyo utaviita Tanzania bara ? Au visiwani?
Naona bado unakuwa mbishi tu kwa kutaka kutamani ukoloni na Mambo yake, Nimekwambia kwanini usijivunie kitu au Jambo lililofanikiwa unalojuwa limetokana na fikra zako mwenyewe
 
Ndugu zangu ,muunganiko wa Mh mama Samia suluhu Hassani Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na Dr Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar umejenga Taswira ya kipekeee ya kiuongozi na namna ya kuongoza kwao,

Ndugu zangu, kwanza wote wawili Ni viongozi wanaoamini katika Maridhiano na mshikamano, Hii ndio sababu utaona namna pande zote mbili yaani Bara na visiwani kukiwa salama na tulivu, Ni viongozi wanaoamini kuwa watanzania wote Wana nafasi sawa katika ujenzi wa Taifa Hili na Wana haki sawa katika nchi yetu,

Viongozi wetu Hawa wote wanaamini kuwa tunaweza tukawa tunatofauti zetu za kisiasa katika nchi lakini tukawa wamoja katika ujenzi wa Taifa letu na tukamkabili kwa pamoja adui yoyote Yule na kumshinda na ushindi ukawa wetu sote

Ni viongozi wenye kutumia hekima na busara kubwa Sana katika kauli zao na hata matendo yao, huwaoni wakimuumiza mtu kwa kauli au matendo ili wajipatie sifa binafsi, Ni viongozi wenye utulivu wa kifikra na kimaamuzi, Ni viongozi wanaopenda kuelekeza na kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yao

Ni viongozi wanaoamini katika umoja wa kitaifa na mshikamano wa watanzania, ndio maana kwao kukaa na mpinzani meza moja siyo shida Wala ajabu, Jambo hili limewasaidia katika kuongoza Taifa letu, kwa kuwa Hali hii imepelekea kupandwa mbegu ya kuaminiana na kusikilizana, ndio maana huoni mavurugu Wala makauli mazito mazito ya kuombea mabaya nchi yetu toka kwa viongozi wa upinzani

Hii inatokana na ukweli kwamba hata viongozi wa upinzani wamejenga Imani kubwa na kuwa na matumaini makubwa wa kauli zitokazo katika ndimi za viongozi Hawa

Ni viongozi wenye hofu kubwa Sana ya Mwenyezi Mungu na wamejawa na mioyo ya huruma na upendo kwa wananchi, Ni viongozi wenye macho ya huruma na wanaotamani kumgusa kila mwananchi mwenye shida ili waweze kumsaidia, siyo viongozi wenye uchu wa madaraka Bali madaraka na uongozi huwafuata wao kutokanaa na kibali walichokipata kutoka kwa Mwenyezi Mungu,

Mimi Lucas Mwashambwa naweza kusema Hawa viongozi wetu wameinuliwa na Mwenyezi Mungu ili kuja kutuinua sisi watanzania,wametuunganisha Kama Taifa, wametujengea matumaini makubwa Sana Kama nchi

Rai yangu kwa watu wanaotamani siku moja kuwa viongozi, Wana mengi Sana ya kujifunza kutoka kwa viongozi wetu hawa, kuwa unaweza kuwa kiongozi bila kuumiza wengine, unaweza kupendwa na kuheshimika na watu bila kuwadhalilisha wengine, unaweza kuinuliwa bila hata kuwashusha wengine, unaweza kukaa katika ofisi kuu bila kufunga ofisi za watu wengine na unaweza kufanikiwa kiuongozi bila kukwamishwa wengine, inua walioanguka maana wanaweza kuja kukusaidia utakapoelemewa na mzigo kuliko ukiwaacha nyuma kwa kutamani kuwahi mbele

Hakika Tanzania itakuja kusimulia kwa vizazi vijavyo juu ya muunganiko huu wa Mh mama Samia suluhu Hassani pamoja na Dr Hussein Ali Mwinyi kwa namna walivyo ituliza nchi yetu na kujenga umoja na mshikamano wetu

Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki Sana, azidi kuwajalia Afya njema na nguvu za kututumikia watanzania, Najuwa wapo wachachee wasio penda namna wanavyoendelea kuungwa mkono na watanzania, maana unaweza kuta wapo wanaoombea waone wakihalibu na kuchukiwa na watanzania , Lakini kwa bahati nzuri maombi ya mamillioni ya watanzania yamekuwa makubwa Sana kwa viongozi wetu Hawa na Mungu amekuwa upande Wao muda na wakati wote, Ndio maana unaona utulivu na Amani iliyo Tamalaki katika nchi yetu, Asante
Walikuja wengi sana kama wewe..ila walikimbia wenyewe baada ya wao kutumika kama toilet pepa..

Uvccm huwa ni toilet pepa mwisho wenu ni kwenye tundu la choo.

Pole sana endelea kutumia ukiamini watakuona uteuliwe huo muda ungeenda kufanya hata vibarua ili kusaidia ndugu zako ili waondeokane kwenye lindi la umasikini.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom