Habari wanajamii wenzangu!
Kuna wimbi kubwa sana katika jamii hasa hapa Jf kuwaona single mother kama watu waliopoteza dira, wasiotakiwa kuolewa tena. Kumetokea mada mbalimbali ndani ya hili jukwaa kuhusiana na hawa wanawake wa aina hii!
Hakuna sababu ya kuwadharau hawa watu wa jinsi hii. Waliwapata hao watoto kwa kukutana na wanaume wasiokua waaminifu. Kabla hujamtupia kombora jua kuna Mwanaume nyuma ya huo usingle mother tena niseme mwanaume dhalimu.
Na mbaya zaidi kuna hadi wanawake wanaowaponda single mother. Unamponda single mother aliyekubali kulea mimba wakati wewe umechoropoa mimba kibao? Au pengine hata hiyo mimba huna uwezo wa kuibeba?
Tuwe na usawa hapa, na kwa wewe unayeomba ushauri wa kuoa single mother ndani ya hili jukwaa, jitathmini sana, kama hutafanya hivyo kwasababu ni single mother make sure unayekuja kumuoa ni bikra. Kama sio na wewe jua tu umeoa single mother indirect way.
Wanawake wengi wanapitia madhila/mazingira mbalimbali, ikiwemo kudhulumiwa, kudanganywa n.k
Dhana ya kwamba ukioa single mother ni lazima achepuke na mzazi mwenzake haina mashiko, inakuwaje sasa ukioa asiye single mother lakini ana ma ex kibao? Mara ngapi zinakuja hoja hapa za wanaume kutembea na ma ex wao ambao wako ndani ya ndoa?
Let Love lead, hayo mengine yasiadhiri mahusiano ya watu.
Stop hatred to single mothers, wanahitaji kupendwa, wanahitaji kuheshimiwa. Nawasihi sana wasiwe waoga wala kuwaficha watoto wao kwa vigezo vya kutendwa, kuachwa au kubaguliwa.