Habari za Jumapili wakuu! Hongereni kwa Ibada kwa wale mlioenda ibadani👋👋
Lengo la mada hii,ni kukushauri na kukutia Moyo wewe Single mother uliejikatia tamaa.
Mimi ni miongoni mwa single mother. Nilipata ujauzito nikiwa Form 4 nina miaka 17 tu! Nililelewa katika Familia ya kilokole na hata haya mambo ya kujiingiza kwenye Mahusiano ya kimapenzi sikuyataka kabisa but makundi& mzazi ndo vilisababisha hivi(nikipata muda nitaleta mada kuhusu hiki) Basi,Baada ya Kujigundua ni mjamzito niliomba Rehema sana nikatubu Kwa Mungu ninakaendelea na masomo. Namshukuru Mungu mimba haikuonekana hadi Siku najifungua zilibaki siku 3 nianze Necta. Nakumbuka nilijifungua Ijumaa then j3 nikaingia Chumba Cha mtihani nikafanya paper nikatoka na 4 mbaya but Cheti nilipata.
Baada ya Hapo nilinuniwa na Mzee karibu Mwaka,nikaishi Maisha ya tabu sana Kiasi kwamba nilitamani kunywa Sumu nife ila nikawaza,kwani mm ndo nimekuwa wa Kwanza?? Nikaamua kutokujichukia na kutokulia tena Nikaamua kuanza kufanya biashara na nikawa najiamini sana kama hakijatokea chochote,then Mzee akashauriwa akanipeleka Chuo but ile Caring haikuwepo! Namshukuru Mungu nilifanikiwa kumaliza,nikatafuta Kazi na nikaamua kujisimamia mwenyewe,nikajithamini na Nikapata Kibali sanaa!!.
NINACHOTAKA NIKWAMBIE NI HIKI:- Wewe bado ni wa thamani hata kama una mtoto! Usijirahisirahisishe kwa Wanaume,eti Kisa ulishazaa!! Uthamani wako uko palepale
🖍️Usikate tamaa kwa Maneno yao au Kejeli zao,Focus kuitengeneza ile future uliyoipoteza hapo Awali.
🖍️Mrudie Mungu na uweke tumaini Kwake kikamilifu. Nina Uhakika atakupa Nafasi tena kama hautakuwa na Mchanganyo!! Kuwa na Msimamo Mungu atakupatia wa kwako!! .
Mwisho,Achana na Uzinzi! Subiri Mume mwema Kutoka kwa Mungu( but kama utakuwa serious na Mungu)
Ulikulia katika familia ya Kilokole. Unajua wengi wanatazama walokole kama ni watu wa karibu na Mungu, lakini ukweli ni kwamba wengi ni wanadamu tu kama wengine. Kuwa mwana wa Mungu ni kuikimbia duniani na fahari zake, kulishika neno lake tu.
1. Ulipata mimba kwa sababu hukumjua Mungu bali ulitumainia ulokole wako.
2. Nakushauri UACHE KABISA kuwanyooshea kidole wazazi wako, kwa sababu walijitahidi kukukanya wala hukuwasikia. Ndio maana baba yako alivunjika moyo juu yako.
3. Kama unadhani kuna eneo wazazi wako hawakutenda vema, basi uwasamehe, ufanye toba kwa ajili yako na kwa ajili yao pia. Uwe na moyo wa kushukuru japo kwa ajili ya jambo moja tu, kwamba walikuzaa, basi uwashukuru kwa ajili hiyo tu.
4. Kuwa single mother SIO sifa njema hata kidogo, bali kutubu dhambi na kumrejea Muumba ni jambo jema kuliko yote hapa duniani. Kumbuka hata Yesu Kristo amesema wazi kuwa mbinguni hakuna wala Krismasi, wala Pasaka, wala mwaka mpya, bali sherehe pekee huko ni pale mwenye dhambi mmoja anapotubu, basi mbinguni huangushwa pati la nguvu kwa ajili yake.
5. Ukiisha kumjua Mungu unafanyika kuwa kiumbe kipya, si kwa kurejeshewa bikira, bali kwa kupewa fikra mpya. Hutamani tena chipsi kuku, pati, mambo ya beach nk, bali kuishi kwako sasa ni Kristo tu. Ukiwa hivyo unatembea katika uwepo wa Mungu na huko utakutana na wana wa Mungu wenye fikra sawa na zako, wote mkinia mamoja. Katika hilo utakuwa na bikra ya roho, ukiwa na roho mpya, ukiua kabisa mwili wa nje usitumikie tamaa za mwanzo.
6. Baada ya hayo epuka kamwe kurejea kwenye uharibifu wa kwanza, kutumikia kwa siri tamaa za mwili kwani utajiangamiza mwenyewe. Mungu ni mwaminifu kwa neno lake:
2 Petro 2
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁸ Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
¹⁹ wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.
²⁰ Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
²¹ Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
²² Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
Kumbuka rehema za Mungu ni nyingi, hivyo tumrudie kwa kurarua mioyo yetu.
Hao wanaoenenda katika udanganyifu ni wale waabuduo upuuzi wa MWANAMKE JASIRI, SUPER WOMAN nk, wakiwadanganya wanawake kwamba watawaweka huru. Kama kweli umemjua Mungu utawakimbia wadanganyifu hawa ambao wamefikisha dunia hapa ilipo kwa kukaidi mpangilio wa kiungu (divine order). Kuwa mwanamke kamili ukijinyenyekesha kwa Mungu na wazazi wako, naye Mungu aonaye sirini atakujalia haja ya moyo wako. Lakini ukitumainia ujasiri wako, kwamba wanawake mnaweza strong woman, basi Mungu hukaa kando akikuacha upigane vita vyako mwenyewe.
Ni neno jema kwamba sasa umeijua kweli, nawe utawekwa huru kabisa mbali ni uharibifu wa dunia hii.
Amina