The tolerance 1
JF-Expert Member
- Sep 10, 2022
- 404
- 517
Sio wote wanapasha kiporo,nakataaShida inakuja kwa single maza ni kupasha viporo na maex wao,,,,
Mkuu hapo nimekupata comments yako hii kwakweli ina uzito sana MUNGU TUSAIDIE
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio wote wanapasha kiporo,nakataaShida inakuja kwa single maza ni kupasha viporo na maex wao,,,,
Mkuu hapo nimekupata comments yako hii kwakweli ina uzito sana MUNGU TUSAIDIE
1. Haya ni matokeo ya kuharibika kwa family structure. Hakuna malezi, ujuaji mwingi, yakiwakuta ndipo kutukana wanaume.Hao single mothers ni kwa sababu wanaume tumekuwa wapumbavu na haujielewi kuwazalisha ni uhuni wa kishamba then tunapotea
Ni watu ila wahuni ingawa sio woteJamani kwani bodaboda sio watu[emoji23]
📌📌Behind every single mother, there is a man like baba ommy dimpoz
Raia msiniue, natania tu 😁
Ulikulia katika familia ya Kilokole. Unajua wengi wanatazama walokole kama ni watu wa karibu na Mungu, lakini ukweli ni kwamba wengi ni wanadamu tu kama wengine. Kuwa mwana wa Mungu ni kuikimbia duniani na fahari zake, kulishika neno lake tu.Habari za Jumapili wakuu! Hongereni kwa Ibada kwa wale mlioenda ibadani👋👋
Lengo la mada hii,ni kukushauri na kukutia Moyo wewe Single mother uliejikatia tamaa.
Mimi ni miongoni mwa single mother. Nilipata ujauzito nikiwa Form 4 nina miaka 17 tu! Nililelewa katika Familia ya kilokole na hata haya mambo ya kujiingiza kwenye Mahusiano ya kimapenzi sikuyataka kabisa but makundi& mzazi ndo vilisababisha hivi(nikipata muda nitaleta mada kuhusu hiki) Basi,Baada ya Kujigundua ni mjamzito niliomba Rehema sana nikatubu Kwa Mungu ninakaendelea na masomo. Namshukuru Mungu mimba haikuonekana hadi Siku najifungua zilibaki siku 3 nianze Necta. Nakumbuka nilijifungua Ijumaa then j3 nikaingia Chumba Cha mtihani nikafanya paper nikatoka na 4 mbaya but Cheti nilipata.
Baada ya Hapo nilinuniwa na Mzee karibu Mwaka,nikaishi Maisha ya tabu sana Kiasi kwamba nilitamani kunywa Sumu nife ila nikawaza,kwani mm ndo nimekuwa wa Kwanza?? Nikaamua kutokujichukia na kutokulia tena Nikaamua kuanza kufanya biashara na nikawa najiamini sana kama hakijatokea chochote,then Mzee akashauriwa akanipeleka Chuo but ile Caring haikuwepo! Namshukuru Mungu nilifanikiwa kumaliza,nikatafuta Kazi na nikaamua kujisimamia mwenyewe,nikajithamini na Nikapata Kibali sanaa!!.
NINACHOTAKA NIKWAMBIE NI HIKI:- Wewe bado ni wa thamani hata kama una mtoto! Usijirahisirahisishe kwa Wanaume,eti Kisa ulishazaa!! Uthamani wako uko palepale
🖍️Usikate tamaa kwa Maneno yao au Kejeli zao,Focus kuitengeneza ile future uliyoipoteza hapo Awali.
🖍️Mrudie Mungu na uweke tumaini Kwake kikamilifu. Nina Uhakika atakupa Nafasi tena kama hautakuwa na Mchanganyo!! Kuwa na Msimamo Mungu atakupatia wa kwako!! .
Mwisho,Achana na Uzinzi! Subiri Mume mwema Kutoka kwa Mungu( but kama utakuwa serious na Mungu)
....Subiri Mume mwema Kutoka kwa Mungu (but kama utakuwa serious na Mungu)
🙏🙏Nimekupenda,umelenga mule mule,,Yani tunasimangwa utafikiri tumejizalisha wenyewe
Single father ndio nini tena? Naona msamiati mpya.ah sema kwa wanaowasimanga mi naona sio kitu kizuri coz kila mtu ana sababu yake ya kuwa single mother sasa wanawachukulia kama vile wamevunja sheria ya nchi,mi nnaposhindwa kuelewa mbn sisi tukiwa single father(s) huwa hakunaga maneno ila ikiwa upande wao inachukuliwaga yan kiviiiiiiiiiiiiiile....
aSingle mzaza huwa watulivu Sana wakipata ndoa kuliko hivi vi graduate ambavyo haviambiliki
Shida inapokuja kwa single maza Ni kupasha viporo na maex wao
Single mother kipaumbele chao kiwe single father wenzao ili wale wasio na watoto waoane wenyewe tatizo single mother wako mstari wa mbele kutaka kuolewa na wasio single fatherHi great thinkers
Nawapa pole single Mothers wote wanaosimangwa. Si wote wamependa iwe hivyo. Wengine walisubiri wachumba mpaka dakika ya 90 bilabila.
Nawashauri single mothers kuweni wema leeni watoto wenu vizuri na mpunguze stress.
Wanaume ni wachache.
ebu niweke sawa mkuu ili siku nyingine nisikoseeSingle father ndio nini tena? Naona msamiati mpya.
Amen🙏🙏Najaribu kufikiria,kwa mfano kama baadhi ya sisi wanaume humu tungezaliwa kama huyu Dada inawezekana kungekuwa na sio single mothers(mlea peke)tu bali na watoto wakutosha 😀😀, Mungu ni wa rehema sana na ni fundi kuliko fahamu zetu.
Unajua nini?Sio wote wamependa na hata kama was planned,yasiyowezekana kwa mwanadamu na kwa mila na mifumo kuonekana sio rahisi sana kwa Mungu yanawezekana.
Mcheni Mungu kwa dhati ya mioyo yenu kama Dada ali vyosema,stand firm,jiaminini mnaweza kufanya vitu vikubwa na vya heshima.
Mimi ninawapenda and value you as per the God's love.
Wonderful
AmenUlikulia katika familia ya Kilokole. Unajua wengi wanatazama walokole kama ni watu wa karibu na Mungu, lakini ukweli ni kwamba wengi ni wanadamu tu kama wengine. Kuwa mwana wa Mungu ni kuikimbia duniani na fahari zake, kulishika neno lake tu.
1. Ulipata mimba kwa sababu hukumjua Mungu bali ulitumainia ulokole wako.
2. Nakushauri UACHE KABISA kuwanyooshea kidole wazazi wako, kwa sababu walijitahidi kukukanya wala hukuwasikia. Ndio maana baba yako alivunjika moyo juu yako.
3. Kama unadhani kuna eneo wazazi wako hawakutenda vema, basi uwasamehe, ufanye toba kwa ajili yako na kwa ajili yao pia. Uwe na moyo wa kushukuru japo kwa ajili ya jambo moja tu, kwamba walikuzaa, basi uwashukuru kwa ajili hiyo tu.
4. Kuwa single mother SIO sifa njema hata kidogo, bali kutubu dhambi na kumrejea Muumba ni jambo jema kuliko yote hapa duniani. Kumbuka hata Yesu Kristo amesema wazi kuwa mbinguni hakuna wala Krismasi, wala Pasaka, wala mwaka mpya, bali sherehe pekee huko ni pale mwenye dhambi mmoja anapotubu, basi mbinguni huangushwa pati la nguvu kwa ajili yake.
5. Ukiisha kumjua Mungu unafanyika kuwa kiumbe kipya, si kwa kurejeshewa bikira, bali kwa kupewa fikra mpya. Hutamani tena chipsi kuku, pati, mambo ya beach nk, bali kuishi kwako sasa ni Kristo tu. Ukiwa hivyo unatembea katika uwepo wa Mungu na huko utakutana na wana wa Mungu wenye fikra sawa na zako, wote mkinia mamoja. Katika hilo utakuwa na bikra ya roho, ukiwa na roho mpya, ukiua kabisa mwili wa nje usitumikie tamaa za mwanzo.
6. Baada ya hayo epuka kamwe kurejea kwenye uharibifu wa kwanza, kutumikia kwa siri tamaa za mwili kwani utajiangamiza mwenyewe. Mungu ni mwaminifu kwa neno lake:
2 Petro 2
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁸ Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
¹⁹ wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.
²⁰ Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
²¹ Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
²² Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
Kumbuka rehema za Mungu ni nyingi, hivyo tumrudie kwa kurarua mioyo yetu.
Hao wanaoenenda katika udanganyifu ni wale waabuduo upuuzi wa MWANAMKE JASIRI, SUPER WOMAN nk, wakiwadanganya wanawake kwamba watawaweka huru. Kama kweli umemjua Mungu utawakimbia wadanganyifu hawa ambao wamefikisha dunia hapa ilipo kwa kukaidi mpangilio wa kiungu (divine order). Kuwa mwanamke kamili ukijinyenyekesha kwa Mungu na wazazi wako, naye Mungu aonaye sirini atakujalia haja ya moyo wako. Lakini ukitumainia ujasiri wako, kwamba wanawake mnaweza strong woman, basi Mungu hukaa kando akikuacha upigane vita vyako mwenyewe.
Ni neno jema kwamba sasa umeijua kweli, nawe utawekwa huru kabisa mbali ni uharibifu wa dunia hii.
Amina
Kwa akili yako unataka bodaboda azae na mbuzi?Wataalam uchwara ndio wanasababisha single mothers, utasikia "MWANAMKE AKIFIKISHA MIAKA 30 HAWEZI TENA KUZAA AU KUSHIKA MIMBA". Dada zetu wakisikia hivyo wanapaniki wanaanza kuzaa na yoyote atakayetokea mbele zao hata BODABODA!
Seriously, naomba nieleweshe jinsi unavyoelewa. Si kwa ubayaebu niweke sawa mkuu ili siku nyingine nisikosee