Hongera tajiri, linaitwaje na linaenda wapi nataka niwe abiria wako siku moja
Bado sijawa tajiri nadaiwa asilimia 40 sijamaliza deni la kuinunua, alafu nisije kutaja jina kumbe nimezinguana na RTO kwa jeiefu akaanza kunipiga vyeti huko barabarani
 
Basi Mungu akusaidie upate hiyo cancer
 
Bado sijawa tajiri nadaiwa asilimia 40 sijamaliza deni la kuinunua, alafu nisije kutaja jina kumbe nimezinguana na RTO kwa jeiefu akaanza kunipiga vyeti huko barabarani
Nitajie route basi unanukia kuwa tajiri kumiliki basi unadhani kitu kidogo?
 
Salute to all strong women who dare to stand by their kids!! Irresponsible men stand somewhere insulting the women taking care of the kids they abandoned!! Shame on them!!!
 
Naomba nirudie sentence yenye utukufu hapo, "Maisha yapo kwaajiri ya watu wenye discipline". Dah maneno mazito sana haya. [emoji25][emoji25][emoji25][emoji25]
 
sasa kama wa kumuoa hamna, ina maana asizae?? huu ni ujinga.
Nionyeshe mwanamke ambaye tokea kuzaliwa hajawahi kufuatwa na wanaume serious waliotaka kumuoa kati ya umri wa miaka 16 hadi 25,nikukutanishe na wadada waliochezea usichana wao hadi muda umeenda wameona hawana jinsi wala namna ya kupata mwanaume serious wanaishia kuzaa na wahuni au wanaume za watu.
 
📖Mhadhara wa 22:

Ni kama zimeanza kujengeka fikra na hisia mbaya za kudhani kwamba kuwa SINGLE MOTHER ni kufeli maisha, au ni maumivu makubwa kuliko maumivu mengine yoyote hapa duniani. Kama una fikra hizo achana nazo zitakuchelewesha.

Kuna baadhi ya wanawake baada ya kujikuta wamekuwa SINGLE MOTHERS wanatumbukia kwenye msongo mkubwa wa mawazo. Pengine unakuta mwingine ana kazi nzuri, biashara nzuri, n.k, lakini anajikuta anaharibu biashara yake, ajira yake, mtaji wake kwasababu kutwa yupo ndani anawaza.

Ni kweli kuna maumivu fulani ya kulea mtoto bila uwepo wa karibu wa baba yake, au labda ulidata na penzi la baba wa mtoto. Lakini hebu fikiria kama ulifika muda ukatengana na wazazi wako ukaenda kutafuta maisha pekee yako, kwanini unaharibu maisha yako kwasababu ya msongo wa mawazo ya kutengana na mtu uliyekutana nae ukubwani? - Acha maisha mengine yaendelee.

Wale mnaodhani kuwa SINGLE MOTHER ni maumivu makali sana kuliko maumivu yoyote duniani basi umefeli kufikiria, amka ufikirie tena. Hebu mtafute mwanamke mwenzako ambaye anaishi na mume (ameolewa) lakini hakubahatika kupata mtoto na hana dalili ya kupata mtoto, halafu uketi nae sebuleni ili akwambie ile hali anayopitia yeye ikoje - Hapo ndipo utagundua kwamba Mwenyezi Mungu amekupendelea kwa kukupa neema kubwa sana.

Kuhusu kuwa SINGLE MOTHER na masuala ya kiuchumi:- Usilinganishe neema ya kupata mtoto na vitu vya Mzungu ambavyo vinatafutwa. Ukishakuwa na uwezo wa kudaka ujauzito hakika mwambie Mungu "asante" kwa sababu umepata neema kubwa sana, hayo mengine ambayo bado hukuyapata yanasubiri juhudi zako na utulivu wako.

NB: "Sio lazima kuwa Single mother, lakini ikibidi; yaache maisha mengine yaendelee"

Right Marker
Dar es salaam
Sept 27, 2024.
 
Wadau huwa unanipa wakati mgumu hili swala ni kweli ukioa singo mama yule jamaaa wake anauwezakano mkubwa wa kutembea na mkeo ambae ni mzazi mwenzake?
 
Kwani imeandikwa lazima mzazi mwenzie awe anaishi mkoa mmoja na mnaoishi nyie kwa sasa...

2..je vipi mke akiwa anagongwa na wengine na sio mzazi mwenzie..


3..hivi vitu kwa sasa ngumu kuvikwepa kugongewa kupo ni kuomba tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…