Tajiri Kichwa
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 9,021
- 22,016
Uzuri jf itadumu milele tunasubiri mrejesho wako ..tena na utabiri utakuwa kwa ID mpya ahaha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni Single parent not single mother. Kwani kuna double mother?Sasa si ni mother, na ni single...
Saw saw mwambiee... By kaka mkubwaa.Mkuu mbona inaonekana umependa sana then kwa kasi ya 4G, kiwango cha upendo ulichonacho kwa sasa je na uyo singo maza wako amefikia kiwango cha upendo ulichonacho ww kwa sasa isije ukachukua maamuz ya haraka alaf mwenzako yupo 2G, utateseka
Kwan being single kuna ubaya? Just ca her a Mother its very enough!!Sasa si ni mother, na ni single...
Kaka singo maza hata ukikaa nae miaka mitatu na zaidi, hao wakinamama wana uzoefu wakuficha makucha yao akitimiza analo taka atakuonyesha "her true colour" ndo utajua kwanini mwanaumme mwezio alimzalisha alafu akamuacha, singo maza ni balaa wengi have "hidden habits"Huwez fanya maamuz kwa muda mfupi hv, wanawake ni wajanja sana wakat wa kubembeleza ndoa, ukishamwoa anabadilika kiwango kikubwa mpk utashangaa, nakushauri kaa naye kwa angalau miaka miwili ukimjua in and out (toa mahari, mchumbie), baada ya kuish miaka kadhaa ndyo ufanye maamuzi, vngnevyo utasaga meno.
Kwanini uende kwa "second hand material " wakati kuna 'first hand material kibao' kijana hao ma resisters wa kwenye ndoa ni hatari, kwanini alifaili mara ya kwanza jiulize?All the best mwaya…..
Kuzaa mtoto hakukufanyi ubadilishe personality yako ..ukimpata mtu unampenda ..unaona mnaendana vitu vingine don't matter..
Ukizaa hugeuki kuwa Zimwi mla watu
Kwanini uende kwa "second hand material " wakati kuna 'first hand material kibao' kijana hao ma resisters wa kwenye ndoa ni hatari, kwanini alifaili mara ya kwanza jiulize?
Tumesha kusamehe kwa maneno mengi .by the way umeandika ili iweje labda.maana nimesoma mpka mwisho sioni kitu unachoomba ushauriweHabari za saa hizi Wanajamvi.
Leo kuna jambo fulani nataka kushare nanyi, jambo ambalo huenda mnalifahamu au hamlifahamu lakini kwa vyovyote najua kwa mjadala huu mtafahamu zaidi.
Tunatofautiana mitazamo. Kuna mitazamo tofauti tofauti kuelekea swala la kuoa Singo maza (naomba nitohoe najua inapaswa kuwa 'Single mother' ila sipendi kuchanganya lugha).
Kuna watu tumejizatiti hatutaoa singo maza ila hii kitu ni rahisi zaidi kuzungumza kuliko kuweka katika matendo. Kwanini ?
Mara nyingi kumpenda mtu hutokea bila hiari. Bila kuamua na kupatanisha maamuzi yako na mtazamo wako hiyo ndiyo sababu baadhi yetu tumejikuta tukienda kinyume na mitazamo yetu linapokuja swala la kuoa singo maza.
Acha nieleze jinsi nilivyozama kwa Singo Maza na kujikuta napuuza mtazamo wangu.
Mwishoni mwa mwezi wa tisa nilipewa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za harusi fulani ya swahiba wangu sana.
Ilikuwa siku ya Jumamos usiku wa hiyo sherehe, wakati sherehe inaendelea na sisi (mimi na kampani fulani ya rafiki yetu) tumekaa kwenye meza ile kwenye meza jirani palikuwa na msichana fulani. Mweupee, mzuri kweli kweli, shape kama la Wema Sepetu. Nilipomuona nikamstua nikampa hi kisha nikakausha maana niliamini sio hadhi yangu ile . Najijua life langu 'dongotee' kula kwa kuunga unga na mishe ziende vizuri ndo nivae. Watoto wazuri kama wale wanataka matunzo.
Basi nikiwa naendelea kushusha bia, nikapaliwa. Bia ikanimwagikia kwenye shati. Shati likachafuka, miongoni mwa watu waliniona hili likitokea ni yule mrembo, rafiki zangu walipoona hili walinicheka sana ila yule mrembo (acha nimwite Asha) aliinuka alipokuwa na kunifata akanipa pole akatoa kitambaa chake akanipa nijifute. Nikakataa akanibembeleza nikaona sooo nikachukua ila sikujifutia chake niliinuka nikaenda msalani. Ila mpaka hapo akawa amenigusa kwa kiasi fulani nikaanza kumuona wife material.
Niliporudi nikamuomba namba akanipa. Niliporudi home nilimpigia simu aiseee! tulizungumza mpaka asubuhi, akanambia anaomba alale nikamuacha ila nikamuomba tukutane siku hiyo hiyo (jumapili) akasema sawa tutakutana jioni. Kweli jioni hiyo tukaweza kukutana maeneo fulani hivi ya ubungo tukaenda Bar fulani hivi. Kwanza kujiamini kuliniisha maana toto zuri vile linakubali appointment na mie tena sehemu km ile ila nikajikaza mpaka nikafanikiwa kumtongoza.
Hakukataa wala hakunambia chochote ila akasema ntakujibu siku nyingine. Nikaona 'Sawa.' mazungumzo yakaendelea ila sasa katika mazungumzo yake alikuwa mwepesi sana kusema maneno fulani yakuonesha kuwa yeye ni mtu wa dini. Lakini pia alikuwa mwenye ushauri chanya sana na kuonesha uzoefu mkubwa wa maisha jambo ambalo lilinifanya nione huyu ni 'wife material.' Istoshe hakuaguza pombe wala soda ila maji tu na akanambia atalipia yeye, nikasema mke si ndo huyu sasa.
Baada ya kama wiki moja hivi toka tuanze kuwasiliana mahusiano yakawa yameanza rasmi na kwakuwa nilishazama na KUDATA kwake sana nikaona sasa ni wasaa rasmi wa kupanga maswala ya harusi maana ni wife material haswa: hana lawama, hana mizinga, ata ukimwambia njoo saa nane usiku anaweza akaja, mshauri mzuri na mzoefu sana wa maisha istoshe ni MZURI MNO wa muonekano mpaka shape yaani kama ya wema.
Waswahili wanasema usione vyaelea vimeundwa, tukiwa katika mazungumzo akanambia kuna kitu nataka nikwambie, nikamwambia niambie, basi nilijua anaomba hela(maana hivyo ndivyo nnavowajua wanawake kwa uzoefu wangu) kumbe na tofauti kabisa na hilo. "Mimi nna mtoto," unasemaje ? niliuliza "Nna mtoto ana miaka mitatu, Nimeona bora nikwambie mapema kabla hatujaingia kwenye ndoa".
Sasa ndo tunarudi kwenye mada hii, unaweza kuwa na mtazamo fulani kuhusu wanawake wenye watoto, kwamba labda hutooa mwanamke mwenye mtoto katika maisha yako lakini mi nakwambia mwanaume mwenzangu unasema hivyo kwa sababu hujawai PENDA mwanamke mwenye mtoto.
Mimi nilikuwa na mtazamo huo huo lakini mpaka kufikia hatua hii ambayo nimependa kiasi hiki, mtazamo wangu nauona wa Kipumbavu sana, najiuliza kwanini nilikuwa naona si vizuri kuoa mwanamke mwenye mtoto ? Hapa saa hizi nawaza namna maisha yatakavyokuwa nitakapokuwa na familia yangu mpya na mtoto wa nyongeza, nna mtazamo mzuri sana kuelekea singo maza wangu na nataka nimpende mwanae kama mwanangu wa kumzaa kwa sababu sasa nimebaini nguvu ya upendo.
Kama hupendi kuoa singo maza sawa huo ni mtazamo wako, ila Mtazamo wako waweza badilika siku moja ukikutana na mwanamke utakaempenda kweli kweli kama mimi ilivonitokea kwahiyo nikushauri usiseme wala kukashifu watu waliooa masingo maza kama hujui nguvu ya upendo, huenda nawe ukajikuta katika njia hii hii.
Singo maza wote jamani nyie watu mna mbinu sana maana leo nimejikuta nakana nilichokishikilia kwa mda mrefu.
Mnisamehe wote niliowakwaza kwa kushea swala hili lililonikuta kwa kweli acha tu nikiri kuwa nimedata, na nimebadili mtazamo wangu.
Ila ushauri kwa wanaume wenzangu, usikashifu wala usiweke itikadi ya SITAOA singo maza, maana utajikuta unakana mtazamo wa kukolea kwa singo maza fulani, hii imenitokea kama mipango itakwenda vizuri basi tutaalikana kwenye harusi.
Mnisamehe kwa kuandika maneno meengi. Karibuni kwa mchango wenu.
A single parent can be a single father or a single mother.Ni Single parent not single mother. Kwani kuna double mother?
Neno halina shida mkuu kwa sababu anakuwa anamlea mtoto kama mzazi pekee.
Niwe mkwel silipend hili neno "Single Mother" nahis kama ni kuwapa ulemavu usiostahili.
Thats exactly my point.Kwan being single kuna ubaya? Just ca her a Mother its very enough!!
Mtu alio toka bush hivi karibuni kuja Town, utamjua tu kwa ushamba wake uitwao 'rural urban excitement'
Kuna watu wameshusha injini mpaka anaona, dah!!Siku zote naamini single mother ni bora kuliko msichana aliyetoa mimba nyingi ili aendelee kuitwa msichana. Single mother hakutaka kubeba dhambi ya kuua .hivi binadamu angekuwa hermaphrodite (jinsia mbili)ni wanaume wangapi wangepona usingle father?