Daniel Adrian
JF-Expert Member
- Jan 1, 2019
- 311
- 326
Kwa mtu mwenye malezi mazuri hawezi kukurupuka kupenda kwa sababu ya sifa za nje. Wako wanawake wengo warembo lakini si kila mwanamke ni wife material, wengine wameumbwa kuipamba dunia tu.
Ama ulikuwa umelewa, ama hujui mke w ndoa anapatikanaje.
Hujui kuwa thamani ya mwanamke ni bikira yake? Sasa huyo aliyezalishwa akaachwa unadhani anajiona mwenye thamani tena? Mbona hata wahuni husema mwanamke akijidai mjanja mzalishe tu, ndio mwisho wa kuringa?
Halafu unaomba namba tu hapo ulevini anakupa!! Wife materiak hawi cheap namna hiyo mkuu, hapo wewe ndio dhaifu wala si yeye. Kacheza na saikolojia yako tu, kakumaliza. Ushahidi ni hapo unaposema ulipojilinganisha naye ulijiona sio wa hadhi yako, tena uliishiwa hata pumzi ya kutongoza, hivyo hukusimama kwenye nafasi yako kama mwanamume.
Huyo alishakubali, ila alihitaji kukufanyia hivyo baada ya kukuona ni mgeni wa mapenzi. Hakuna jipya hapo. Hiyo kutaja taja mistari ya kidini ilikufanya uamini ni mcha Mungu, lakini kuna tatizo kubwa. Mcha Mungu asingekubali kukutana nawe baa!! Afu huyo Mungu alimjua kabla ama baada ya kupata mimba? Huyo alikuwa desperate wa kupata ndoa, alikuwa akitafuta mwanamume yeyote amuoe.
Ni hatari kubwa kuoa mke mwenye uzoefu wa maisha. Aliupata wapi huo uzoefu? Halafu kukulipia bia ndio sifa ya mke wa ndoa?
Yaani baada ya kuonana wiki moja tu, unapangandoa!! Nadhani tatizo lakk ni kubwa zaidi. Wewe ni dhaifu wa mapenzi. Wife material haswaa kwa mahusiano ya wiki moja, hujajua hata habari zake mwenyewe, alipataje huyo mtoto, kwa nini baba wa mtoto alimtosa, wazazi wake ni kin nani, anafanya shughuli gani haoo mjini n.k. Wife material unamwita saa nane usiku anakuja, hii ni zaidi ya hatari!! Halafu hiyo shape ya Wema ndio uchafu gani? Ni heri basi ungemsaka wema tu awe mkeo, yaani wewe umedata kwa Wema kuliko huyo mkeo, jitafakari utagundua hilo. Unampima mkeo kwa kupitia Wema, yaani huyo ndio SI unit yako!!
Miaka mitatu single mama alikuwa anasubiri mwanamume wa aina yako, hongera mkuu. Hakika umepata mke, nikutakie maisha marefu kwenye ndoa yako.
Huko ni kukurupuka kwenye mapenzi kwa kiwango cha SG, bado unahitaji mwongozo zaidi kujua mapenzi ni nini. Ama umri wako ni mdogo bado, ama hukuwa na maelekezo mazuri kuhusu maisha.
Asiyejua maana haambiwi maana, hongera kwa kutoka kwenye upumbavu na kuingia kwenye daraja la werevu. Hongera pia kwa mtoto wa nyongeza, uzazi mgumu siku hizi.
Jifunze kuyatawala mapenzi, usiwe mtumwa wa papuchi. Hapo hakuna cha mapenzi wala nini, ni tamaa tu ama lust. Unahitaji msaada kabla hujapotea kabisa.
Na hizo mbinu ndio zimekunasa, umepoteza hadhi yako kama mwanamume sasa wewe ndio unaolewa hapa.
Story yako wala haisadifu hoja, ingawa unajitahidi kujenga mazingira ya kuoa single mother. Jaribu utunzi wenye ubunifuzaidi ya hiki kituko ulichoandika. Hakuna anayekashifu single mother ila ukweli utasemwa. Nakushauri usome thread inayosema wanaume walioharibika akili, itakupa mwanga kidogo.
Kwahiyo ndugu unahisi nimepotea. Nikuulize swali: Ushawahi kupenda achana na kutamani kutokana na sifa za nje kupenda ishawahi kukutokea ?